Ikithibitika kimantiki raisi kadanganya taifa adhabu yake nini

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,984
2,587
Watanzania wenzangu, jana maaskofu wamemwambia raisi wa Jamhuri na Mwenyekiti wa wavua magamba kuwa awataje wanaohusika na madawa la sivyo atakua mwongo.

Kwa jinsi nnavyomfahamu huyu jamaa hatataja maana nna hakikika ni mwendelezo wa propaganda ya udini ambayo mpaka leo ameshindwa kuthibitisha. Na kama hatataja kwa mujibu wa watumishi hawa atakua MWONGO.

Je muongozo wa katiba unatuambiaje?
 
huyu mbona ni muongo toka zamani tu...kwani unadhani hawamjui kuwa ni muongo?
 
Watanzania wenzangu, jana maaskofu wamemwambia raisi wa Jamhuri na Mwenyekiti wa wavua magamba kuwa awataje wanaohusika na madawa la sivyo atakua mwongo. Kwa jinsi nnavyomfahamu huyu jamaa hatataja maana nna hakikika ni mwendelezo wa propaganda ya udini ambayo mpaka leo ameshindwa kuthibitisha. Na kama hatataja kwa mujibu wa watumishi hawa atakua MWONGO. Je muongozo wa katiba unatuambiaje?


Katiba ya nchi inampa mamlaka makubwa sana rais na wala hawezi kushtakiwa.
 
Hizo ni propaganda za 'diversion of thoughts', toka kujivua vita dhidi ya ufisadi kwenda vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Bado anzo zingine zingi tu atakuja nazo siku za mbele.
Huyo ndiye jk mlopokaji.
 
Mhhhhhhh, mi naona kama ameingia CHOO CHA KIKE katika hilo.
 
Mbona huyu ni muongo tu sikuzote....so hakutakua kuwa na jipya lolote lile
 
Mbona huyu ni muongo tu sikuzote....so hakutakua kuwa na jipya lolote lile

Hivi alivyosema viongozi wa dini wanafanya biashara ya madawa ya kulevya alikuwa na maana ya viongozi wa dini gani? Sikuisikia hotuba yake japokuwa najua alikuwa kwenye sherehe za kumsimika Askofu Ndimbo wa kanisa Katoliki.

Hapa nashindwa kuelewa kama alikuwa anawaambia Wakatoliki ama wakiristo ama dini zote waislamu, wakiristo, wabudha, wabahai, wa dini za asili, n.k. Huenda kuna siku atawaambia viongozi wa serikali yake pia kwamba waache kufanya biashara ya madawa ya kulevya ka kuwa hii trend inaonyesha viongozi ndio washiriki wa biashara hii
 
SWALI KWA WANAJAMIIFORUM=Ikithibitika kimantiki raisi kadanganya taifa adhabu yake nini




Adhabu yake ni "KUDHARAULIWA" By Askofu Mokiwa
Nimepata au nimekosa?
 
Hiyo inazidi kumtafuna yeye na chama chake. Kikatiba hatashtakiwa ila kisiasa amekwishajishtaki kwa wananchi. CCm inakufa kifo asilia (Natural death)
 
Watanzania wenzangu, jana maaskofu wamemwambia raisi wa Jamhuri na Mwenyekiti wa wavua magamba kuwa awataje wanaohusika na madawa la sivyo atakua mwongo. Kwa jinsi nnavyomfahamu huyu jamaa hatataja maana nna hakikika ni mwendelezo wa propaganda ya udini ambayo mpaka leo ameshindwa kuthibitisha. Na kama hatataja kwa mujibu wa watumishi hawa atakua MWONGO. Je muongozo wa katiba unatuambiaje?

Mokiwa yeye mwenyewe kwenye hiyo biashara yumo. Ukimuona mtu anakimbilia kujitetea kama Mokiwa ujue anataka kujisafisha !
 
Huyu hana jipya tumeshamzoea badala amseme mwanaye RIZ waache kuwaibia watanzani mali zao
 
Mokiwa yeye mwenyewe kwenye hiyo biashara yumo. Ukimuona mtu anakimbilia kujitetea kama Mokiwa ujue anataka kujisafisha !

Na nyie ndio mnaoficha waharifu, kama unajua Mokiwa yumo si umpeleke katika vyombo vya dola achukuliwe hatua
 
Viongozi wa dini wako sahihi kuhitaji ufafanuzi na uwazi ni wa kina nani alikusudia kuwasema mathalani kama kuna kiongozi wa dini fulani basi amtaje! Ikumbukwe kuwa maelezo yake yanaashiria wahusika wanatumia dini kama kivuli kufanikisha hiyo biashara haramu.

Unajua raisi ni taasisi kubwa na nyeti (Kwetu TZ ni taasisi iliyotibuka) ambayo hutarajii kiongozi wake atakuwa anatemebea mitaani na kutoa kauli zisizo na mashiko. After all JF hizo tuhumu kwa viongozi wa dini ni kubwa kuliko maelezo, jamani raisi alizungumzia viongozi wa dini sio wa vyama vya mpira.... watu ambao wanapashwa kuwapa watz msaada wa kiroho ndio wawe wanauza madawa ya kulevya sijui mmepata raisi au mlimsikiliza kama mnavyomsikiliza Ngeleja, ndio najua manamjua raisi wetu kuwa ni mtu ambaye hayuko serious lakini pamoja na hayo anao wajibu wa kuwaeleza watz ukweli.
 
Watanzania wenzangu, jana maaskofu wamemwambia raisi wa Jamhuri na Mwenyekiti wa wavua magamba kuwa awataje wanaohusika na madawa la sivyo atakua mwongo. Kwa jinsi nnavyomfahamu huyu jamaa hatataja maana nna hakikika ni mwendelezo wa propaganda ya udini ambayo mpaka leo ameshindwa kuthibitisha. Na kama hatataja kwa mujibu wa watumishi hawa atakua MWONGO. Je muongozo wa katiba unatuambiaje?
By default yeye ni mwongo. kwa hiyo kama amesema uongo ndivyo alivyo hatutashangaa. Itashangaza sana kama aliyoyasemani kweli, atakuwa ametoka kwenye reli zake (uongo)!
 
Mbona tayari ameshajibu kwa kukwepa kama kawaida yake baada ya kubanwa:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa za Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, ni kauli ya kusikitisha na ambayo haikutegemewa kutoka kwa viongozi hao wa dini.

Viongozi wa dini ni watu wa kutumainiwa sana katika jamii yeyote, lakini ikizingatiwa kuwa wao sio malaika ama watakatifu hapa duniani, kwani nao wanatumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa kabisa.

Katika Hotuba yake kwenye sikukuu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga, Rais Kikwete alitoa ombi ambalo si geni kwani alishalitoa katika hafla zingine pia zilizohusisha viongozi wa dini.

Katika sherehe hiyo Rais alitoa ombi la kuwataka viongozi wa dini wajihusishe kwa ukamilifu katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Rais Alisema, "Ni tatizo linalozidi kukua pamoja na jitihada za Serikali kupitia vyombo vya usalama kuwabana, kuwawajibisha watumiaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Athari zake kwa jamii zinaeleweka hivyo haihitaji kuzirudia" Rais alieleza, "Hata hivyo niruhusuni niseme tu kwamba tusipofanikiwa kulidhibiti tatizo hili, hasara yake ni kubwa mno. Watoto wetu wengi wataharibika, uhalifu, hasa wa wizi na mauaji utaongezeka. Taifa litaharibikiwa." Amesema Rais na kuendelea kueleza kuwa,

"Siku hizi kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya. Inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama, Lakini inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaostahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa, Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya". Rais alisema.

Kwa maneno haya, tunategemea viongozi wa dini kuchukua onyo hili la Rais kama ishara (Clue) na kuanza kuifanyia kazi.

Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama kweli, ni wa rangi gani? Unatakiwa kushtuka na kuweka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumuondosha nyumbani kwako hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako. Rais ana nia njema sana katika kulielezea jambo hili na mwenye nia njema haumbuki.

Hivi karibuni wapo viongozi wa dini wamekamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili yasiyo tegemewa na jamii kwa ujumla, wapo ambao wameshakamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, wapo wanaochunguzwa, tumeshawashuhudia na bado wataendelea kushuhudiwa. Hili si jambo dogo la kujitetea kwa kauli nyepesi kutoka kwa watu wanaotegemewa na jamii kwa kumpa Rais saa 48.

Anaejishuku ajisalimishe mwenyewe, anaeshukiwa na jamii afichuliwe ili afanyiwe uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake lakini msisubiri Rais awataje hadharani ndiyo muanze kuchukua hatua.

Mnategemewa muweke mikakati na vipaumbele vya kufanyia kazi changamoto hiyo, na sio kuaihirisha tatizo hili ambalo linazidi kuwa kubwa. Kazi hii ya kupambana na madawa ya kulevya haimhusu Rais peke yake inamhusu kila Mtanzania, popote alipo katika nafasi yake na viongozi wa dini wananafasi kubwa sana kwa sababu wao wanasikilizwa, wanatoa ushauri na wanategemewa kuwa na maelekezo yanayompendeza Mungu.

Mwisho.

Imetolewa na:

Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
Dar-Es-Salaam.

07 Juni, 2011

 
Rais asipowataja basi Obama atawataja. Juzi amewataja Wakenya wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Rusubiri Obama awataje kisha awahitaji huko Marekani kwenda kujibu mashitaka halafu tuseme Marekani inaingilia mambo ya ndani ya Nchi huru!!
 
Mokiwa yeye mwenyewe kwenye hiyo biashara yumo. Ukimuona mtu anakimbilia kujitetea kama Mokiwa ujue anataka kujisafisha !

Kama Mokiwa yumo na Rais anajua hivyo na bado hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yake(MOKIWA) basi Rais ni mshiriki kwenye biashara hiyo haramu.Au labda wamedhulimiana ( si unajua mambo ya kimjini mjini?)
 
Back
Top Bottom