El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 538
Kama ungewatafuta watu ambao ni ngumu sana kuwakuta wanashabikia watu hivi hivi ( sycophancy) mie ni mmoja wao. Nina tabia ya kuunga mkono watu wenye kitu( substantive).
Katika mizunguko yangu ya maisha, nimewahi kukutana na huyu bwana mdogo Said Mtanda.
Bila hata kumngunya maneno huyu bwana mdogo ni mtu mnyoofu, anajua uongozi na ni mtu wa matokeo.
Ukikutana nae, utamuona jinsi alivyo na hekima na alivyokua kisiasa. Anajua siasa za maendeleo, anafuata sheria na ni muwazi.
Nakumbuka siku Moja akiwa anaendesha gari mwenyewe alikamatwa na askari trafiki ambaye alikuwa Bado hamfahamu kuwa yeye ndo alikuwa mkuu wa wilaya.
Alijitetea kama watu wengine ambavyo hufanya ili wasamehewe. Yule Traffic alikataa kumsamehe na akampeleka kituo kikuu cha polisi. Mara baada ya kufika kituoni yule Traffic alishangaa kuona maaskari wengine wakimpigia saluti. Alipgopa sana baada ya kuambiwa kuwa alikuwa amemkamata mkuu wa wilaya.
Yule Traffic alitaka kuacha kumuandikia notification ya faini yake. lakini Jinsi Mtanda anavyojua uongozi kuwa dhamana na jinsi anavyofuata Sheria, alikataa kusamehewa na alilipa faini na kuondoka.
Huyu ni kiongozi mwadilifu, anajielewa na anajali nafasi na majukumu ya watu wengine.
kwa sifa za uchapakazi, uadilifu na ujana wake kwa maana ya umri, huyu ni kiongozi Bora na ni maombi yangu apandishwe cheo na apewe nafasi ya ukuu wa mkoa na kwa maana hiyo, ikimpendeza Rais, mkoa wa Shinyanga.
Nasikia kahamia wilaya ya Ikungu kama DC, Namuombea sasa asogee Shinyanga.
My disclaimer, huyu bwana hatutoki mkoa mmoja, siyo kabila langu, na siyo hata dini yangu. Hatutoki hata kanda moja.. Ni sifa zake tu za uongozi ndo zimenifanya nimuombee ili afikiriwe !!.