Wapenzi wana wa MMU
Wewe ni mume, umejaaliwa kipato cha wastani. Umekopa fedha benki, ukajenga nyumba, ukanunua shamba na ukanunua gari la kutembelea. Mke wako ni mama wa nyumbani.
Siku moja ukabaini mkeo ana uhusiano na mwanaume mwingine. Mkaingia ktk mgogoro na hatimaye mkaamua kuivunja ndoa yenu na mali kugawana.
Katika mgao, mke akapata nyumba na gari (vilivyotokana na mkopo uliokopa na ambao bado benki wanaendelea kukukata), na wewe ukachukua shamba.
Siku chache baada ya mchakato huo kukamilika, ukagundua kuwa, yule mwanaume uliyekuwa ukimtuhumu kuwa ana uhusiano na mke wako, amehamia katika nyumba uliyompa mkeo, na pia anatumia gari ulilomuachia mkeo wa zamani. Na wakati mwingine, anakupita mitaani na kukutimulia vumbi wakati wewe, unasubiri daladala au boda boda.
Je, utafanyaje? Mali uliyochuma, inatumiwa na mwanaume mwingine asiyejua uchungu wake? Anamgegeda mkeo ktk nyumba uliyoitolea jasho na bado unaendelea kuitolea jasho (maana, benki bado wanakukata).