Ikikutokea hii HALI NA MKEO/MPENZIO how i'd u react? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikikutokea hii HALI NA MKEO/MPENZIO how i'd u react?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NGULI, Jun 4, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Umejitihadi ukamtimizia haja yake ya kumpeleka out kwenye concert ya maisha yake kumwona mwanamuziki aliyetamani maisha yake yote kumwona/kuwaona. Mara anatambulishwa mwanamuziki jukwaani zinapigwa fataki pale za kuonyesha star anaingia mara anaanza kulia akimwona tu anazimia mfano mzuri cheki clips za Michael Jackson. Akizinduka anang'angani kwenda mbele kucheza naye anazuiwa na walinzi anaforce kwa kujigaragaza chini mpaka star/mwanamuziki anasema mwacheni aje akifika pale jukwaani anamkumbatia na kuanza kulia. hivi uta react vipi katika hali kama hii. Akirudi toka jukwaani utaendelea kutabasamu na kucheza naye tuu??? Ni swali tu tu shee mawazo labda mimi nakuwa mshamba hapa.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nguli uliiona kwenye concert ya Fally Pupa nini maana kuna mdada huwa anaonekana alivyong'ang'ania kupanda jukwaani hadi nguo ikamchanika.

  BTW: Kusema ukweli si kwenye concert tu bali popote mie nafikiri wapenzi tunatakiwa kuwa na staha japo kidogo hata kama mziki unaupenda kiasi gani au mwanamuziki unampenda kiasi gani si vema kufanya vitu ambavyo unajua vitamkwaza mwenzio. Maaana utakuta mwingine ametoka na Mr. kwenda mziki sasa kisa anaupenda basi atanyanyuka kwenda cheza na yeyote mradi kacheza- saa nyingine tunakaribisha vishawishi wenyewe.

  ingekuwa mimi- pale alipozimia tu ningemrudisha nyumbani na kama angeng'ang'ania na kupanda jukwaani basi mara atakaposhuka jukwaani angenikuta nimeshatangulia nyumbani.
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapa kuna mawili..maana kuna mtu inatokea tu anapenda kumuona mtu fulani kutokana may be umaarufu wake na hii haimaanishi ana hisia za kimapenzi.....we nenda tu siku Brazili wanapotua uone watu watakavyomshadadia Kaka....
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Gosh ni kweli usemayo Sio njema kabisa Nguli haileti picha nzuri katika mahusiano ..Ila siku akija Denzel Washington nitaomba muzee anipe chance nikamkumbatie kidogo tu .....sijui mapromota watamleta lini ?
  Pole Nguli kama yamekukuta..
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wewe ni mwema sana mimi hata nyumabani asingenikuta....najiuliza swali hivi kuna siku aliwahi kuzimia kwa kuniona??

  umenipa angalizo lingine siiajabu mpaka wake za wakubwa wakazimia unakumbuka enzi za kanda bongo man pale Nairobi?

  ha ha ha halijanikuta nilikuwa saloon jana nikaona vedeo ya mkongo aliekuja da kufanya shoo......
   
 6. Mwazani

  Mwazani Member

  #6
  Jun 4, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! shoga kumbe na wewe ni wale wale!
   
 7. RR

  RR JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Nguli na we ukipata chansi ya kum-hug Beyonce itakuaje?
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  sasa kumbe nifanyeje Mwazani nimesema nitaomba ruhusa,ruhusa yenyewe kuna kukataliwa na kukubaliwa ,,......
   
 9. Kakungulume

  Kakungulume JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2010
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 212
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Haivutii hata kidogo kuona mpenzio akimuhusudu mtu mwingine tofauti na wewe ambaye anasema ni wake wa maisha............
  HAIVUMILIKI HATA KIDOGO....ni KOVU TAYARI.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Jun 4, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Kwa ishu hii, ni kumchukua juu kwa juu na kurudi nyumbani sidhani kama furaha ya mtoko itakuwepo tena hapo.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nguli .........mwanamke anaweza kufikiri anatamani kumuona mtu fulani sana lakini naamini kama anakupenda wewe na hana mawazo ya kitoto mtakapomuona huyo mtu mwengine wala hatang'ang'ania kumgusa, kumkumbatia wala kucheza nae
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  wengine wanaweza kushusha makonde hapo hapo...Ila huyu dada wa kwenye Fally Ipupa alivuka mipaka
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Moyo utapoa ghafla na naamini njia za kurudi zitakuwa mbili
  Moja yangu nyingine ya kwake na huyo staa wake...
  Huyo ni staa...wangapi anawahusudu kimyakimya...na kujirahisi...
  TAFAKARI...
   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Itakuwa kawaida sana, infact mimi sizimii wanamuziki hata kidogo wala wacheza cinema nna appreciate kazi zao na vipaji vyao. Mimi napenda kuwa karibu na interlectualz kama akina Moyo alieyeandika kitabu kile cha madeni ya afrika akina Mandela tuta discuss kile kitabu chake cha mwendo mrefu kuelekea Uhuru/long walk to freedom. Au mtu kama Kiranga wa JF tuta discuss mambo ya poet kidogo na kuumiza vichwa katika kujibizana.
   
 15. RR

  RR JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Beyonce ilikua mfano tu mkuu, namaanisha mwanamke unayemhusudu sana.
  Hata hivyo wanaume ni rahisi kudhibiti hisia kuliko wanamama
   
 16. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #16
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja FL1 na mimi ningependa kumhug ila si kwa nia ya mapenzi ila ni kwania ya kuwa fun wake that's all
   
 17. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mbona hiyo afadhali...
  Vipi ikiwa atapanda jukwaani na kuanza kumsasambulia mwanamuziki huyo?
   
 18. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu ndo maana nikasema anamuhusudu kivip?
   
 19. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hili linahitaji special thread
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jun 4, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli nitavunjika moyo na sidhani kama uhusiano wetu utakuwa kama ulivyokuwa zamani. Kwa mke kukufanyia hivyo ni kukuonesha dharau na kutokukuheshimu. Pia tendo lake hilo ni ishara tosha kuwa ni mtu mdhaifu na asiye na msimamo. Sitashangaa tendo hilo kuwa ndio mwanzo wa mfarakano wa ndoa yetu (kama kabla yake kila kitu kilikuwa poa). Na sijui nitalichukuliaje lakini ninachojua sitalifurahia hata kidogo. Nitahoji pia maadili yake, busara zake, akili pamoja na hekima zake kwani wanandoa wanaopendana na kusheshimiana hawawezi kamwe kufanyiana hivyo. Ndio maana moja ya kanuni zangu ktk mahusiano ya kimapenzi ni kumheshimu mwenzako popote pale:alipo na asipo.
   
Loading...