Ikifika mwisho wa sinema hii ukaona JWTZ na TAKUKURU wanarejesha bakaa nchi kwisha

Thomas Sankra Jr

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
418
128
Wanajukwaa.

Siku ya jana tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) imerejesha bakaa ya fedha zilizosalia wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana. Hatua hii kweli inawalakini, kwani tume hii imekabidhiwa jukumu kubwa na watanzania kwa kuendesha uchaguzi wa wazi, haki na amani.

Tume ya uchaguzi ilishindwa kufanya uchaguzi wa haki na wazi hatua hiyo, imesababisha malalamiko mengi, kwanza watu kutojiandikisha kwa wakati na pia wengi wao kutopiga hata kura. Pia tume imeshindwa kuendesha uchaguzi wa haki na wazi licha ya kuwa kulikuwepo amani na utulivu.

Haki huinua taifa, hofu ubomoa taifa.. Jana tume ya uchaguzi imelejesha fedha baada ya kumaliza uchaguzi mkuu uko nyuma tume hii ilishindwa kazi kutokana na kukosa fedha za kuendeshea majukumu yao yaliyopangwa kwa mwaka husika mbaya na ni vyema ..

Kesho ukisikia jeshi la wananchi wa Tanzania na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wamepeleka au kurejesha bakaa za fedha basi nchi imekwisha na taifa limeangamia kwani JWTZ na TAKUKURU ndio taasisi pekee za serikali zinazotekeleza kazi zake bila kuingiliwa, upendeleo, hofu ama woga taasisi izi ni imara na zakizalendo zenye nidhamu, uti na kwa kiasi furani haki inaonekana kutendeka.

Tunaziomba zisifanye kazi kwa kufuata upepo wa hofu.
 
Waliopewa dhamana wanaishi kwa hofu kuu hakuna mwenye uhakika na wadhifa wake kwa staili ya uongozi wa MwendoKasi.

Kujihami kila mmoja anajaribu kujipendeza awezavyo hata kwa kufanya kituko cha kurudisha fedha Kisha kuomba fedha za kujengea kama huyu mzee lubuva

Sitashangaa hata Ndalichako akarudisha bakaa

SYCOPHANTS
 
Wanajukwaa.

Siku ya jana tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) imerejesha bakaa ya fedha zilizosalia wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana. Hatua hii kweli inawalakini, kwani tume hii imekabidhiwa jukumu kubwa na watanzania kwa kuendesha uchaguzi wa wazi, haki na amani.

Tume ya uchaguzi ilishindwa kufanya uchaguzi wa haki na wazi hatua hiyo, imesababisha malalamiko mengi, kwanza watu kutojiandikisha kwa wakati na pia wengi wao kutopiga hata kura. Pia tume imeshindwa kuendesha uchaguzi wa haki na wazi licha ya kuwa kulikuwepo amani na utulivu.

Haki huinua taifa, hofu ubomoa taifa.. Jana tume ya uchaguzi imelejesha fedha baada ya kumaliza uchaguzi mkuu uko nyuma tume hii ilishindwa kazi kutokana na kukosa fedha za kuendeshea majukumu yao yaliyopangwa kwa mwaka husika mbaya na ni vyema ..

Kesho ukisikia jeshi la wananchi wa Tanzania na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wamepeleka au kurejesha bakaa za fedha basi nchi imekwisha na taifa limeangamia kwani JWTZ na TAKUKURU ndio taasisi pekee za serikali zinazotekeleza kazi zake bila kuingiliwa, upendeleo, hofu ama woga taasisi izi ni imara na zakizalendo zenye nidhamu, uti na kwa kiasi furani haki inaonekana kutendeka.

Tunaziomba zisifanye kazi kwa kufuata upepo wa hofu.

Labda JWTZ, hao wengine mbona Kiongozi wao Mkuu alishawahi lalamika kuwa anashikwa mikono, akiwasilisha mafaili sehemu fulani yanakaa muda mrefu au kutotoka kabisa.
 
Sitaki kuamin kama kweli iyo pesa iliyorudishwa ipo, isije ikawa sanaa!!

Sanaa kama ya balehe?! Ha ha ha!

Zamani za kale wakati balehe zinasumbua, ilikuwa kawaida yetu kuwakoga wasichana kwa sanaa ya kibunda cha fedha. Tuliwatoa out wasichana na kufanya meza kuubwa ya duara na kuanza kuagiza round. Fedha zote tulizokuwa nazo tunakusanya pamoja, wa kwanza kulipa round anapitiziwa kwa chini, anatoa kibunda na kulipia round yake. Salio anapewa wa pili kulipia, naye anatoa hadhari kibunda ili 'watoto' waone. Hivyo hivyo sanaa inaendelea kiasi watoto wakitoka hapo lazima wakubali kuwa wale jamaa wako safi.

Sasa naona na CCM nayo inatuletea sanaa ya kibunda.
 
Si kipindi wanaandikisha walisema hawana hela za kununulia vifaa vya BVR hadi wakataka kukodi vya kenya?

Ngoja namie nijipange nirejeshe kamshahara kalikobaki
 
Sanaa kama ya balehe?! Ha ha ha!

Zamani za kale wakati balehe zinasumbua, ilikuwa kawaida yetu kuwakoga wasichana kwa sanaa ya kibunda cha fedha. Tuliwatoa out wasichana na kufanya meza kuubwa ya duara na kuanza kuagiza round. Fedha zote tulizokuwa nazo tunakusanya pamoja, wa kwanza kulipa round anapitiziwa kwa chini, anatoa kibunda na kulipia round yake. Salio anapewa wa pili kulipia, naye anatoa hadhari kibunda ili 'watoto' waone. Hivyo hivyo sanaa inaendelea kiasi watoto wakitoka hapo lazima wakubali kuwa wale jamaa wako safi.

Sasa naona na CCM nayo inatuletea sanaa ya kibunda.
hahahaaa mkuu umenikumbusha Mbali sana, haya maccm ni yakuyaogopa kama ukoma yan ni maongo sana
 
Back
Top Bottom