Prince Naahjum_
Senior Member
- Jun 13, 2016
- 139
- 125
Hitaji la asili la kila mwanaume ni kuwa na busara, hekima, utashi, akili na uelewa. Haihitaji kuwa na shahada ya uzamili, au uzamivu ili kuwa na hivyo vitu. Ni uamuzi tu kutoka ndani ya kilindi cha moyo wako.
Ndoa na mahusiano mengi yanavunjika kwa vile wanawake wameolewa au wana date na wavulana na sio wanaume, na kuna tofauti kubwa kati ya 'mvulana' na 'mwanaume' sababu ambazo nimekwisha ziainisha huko nyuma.
Wewe kama mwanamke umeumizwa sana na mapenzi basi omba Mungu akupe mwanaume mwenye busara, utashi na hekima. Kilio na maumivu ya kihisia hayawezi kuwa sehemu ya maisha yako.
Na wewe kama mwanaume omba sana kwa Mungu akujalie hekima zaidi, utashi, akili na maarifa. Nina uhakika hata wanawake ambao wanajifanya ni matapeli wa mapenzi hawataweza kukukaribia.
Maana utakuwa sript writter na director mwenyewe na hivyo rahisi kimgundua kuwa huyo ni msanii na kumpeleka fasta akajiunge na Ray Kigosi akaonyeshe usanii wake huko.
"An intelligent man will open your mind, a handsome man will open your eyes but a gentleman will open your heart and keep it"
Nimezungumza vyema?