Ijue Taasisi ya Pondeza Foundation

Ijue Taasisi ya Pondeza Foundation

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,429
Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundation, Mhe. Ussi Salum Pondeza ametoa ufafanuzi mfupi kuhusu malengo na safari ya kuianzisha wa Taasisi ya Pondeza Foundation ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo ameianzisha mwaka 2014 ikiwa na lengo la kuisaidia jamii kwa wale wenye uhitaji.

Aidha, Mhe. Ussi Salum Pondeza ameeleza kuwa lengo la kuanzisha Pondeza Foundation si kwa ajili ya maslahi yake binafsi bali ni kuleta maendeleo kwa jamii na matokeo yanakwenda taratibu kutokana na nguvu iliyopo ni ndogo, wadau ambao wamejaaliwa lolote ili kuiunga mkono basi wajitokeze ili waweze kufika kwa haraka zaidi.

Mhe. Ussi Salum Pondeza ameeleza kuwa Pondeza Foundation kwa sasa bado haijakuwa na nguvu kubwa kusaidia wanafunzi wa Elimu ya juu kwa wingi japokuwa wapo ambao wananufaika na mikopo ili kujiendeleza na masomo.

"Serikali yetu ya awamu ya nane imeweka kipaumbele katika kusaidia wanafunzi wa Elimu ya juu ili kuwapunguzia changamoto mbalimbali katika masomo yao, ambapo kwa zaidi ya asilimia 75 wanafunzi hao wanapatiwa mikopo Zanzibar" - Mwenyekiti wa Taasisi ya Pondeza Foundation, Mhe. Ussi Salum Pondeza

Mhe. Ussi Salum Pondeza ameeleza kuwa Pondeza Foundation imekuwa ikisaidia baadhi ya wagonjwa ambao wamekumbwa na maradhi mbalimbali lakini wanakosa pesa ya kujikimu katika matibabu hasa kupitia kampeni ya Afya ya mama na mtoto na pia wenye uhitaji wa kufanyiwa upasuaji mbalimbali japokuwa si kwa wingi ila si haba.

Screenshot 2025-06-09 at 16-15-21 Instagram.png
 
Back
Top Bottom