Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Je, na wewe ni miongoni mwa wanaoamini kuwa Serikali au Mahakama zetu hazitambui uchawi? Basi badili mtazamo kuanzia sasa.
Serikali inautambua uwepo wa uchawi kisheria. Hii ni kwa kuwa Sheria ya kudhibiti uchawi (Witchcraft Supression Act) inampa mamlaka Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa au Rais kumpeleka uhamishoni mtuhumiwa wa uchawi ambao umethibitika.
Hata hivyo, sheria hiyo hiyo inalifanya tendo la kumtuhumu mtu kwamba ni mchawi kuwa ni kosa la jinai. Huu ni mkanganyiko wa kisheria unaohitaji kurekebishwa.
Naileta Sheria hii Namba 12 ya Mwaka 1998 kuhusu Uchawi (The Witchcraft Act) ili wanasheria waliopo nasi hapa JF watusaidie kuitafsiri na kuichambua kwa lengo la kukuza na kusambaza uelewa kwa raia, sambamba na kupendekeza marekebisho pale ambapo imeonesha mapungufu.
Hapo chini nimeweka link na PDF kwa ajili ya kuisoma na kuipakua.