Ijue RAMIA kwa kiasi ilivyotengenezwa.

Ijue RAMIA kwa kiasi ilivyotengenezwa.

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,494
300px-Bullet.svg.png

Ramia ya kisasa huwa na: 1) risasi yenyewe 2) ganda la ramia; mara nyingi ni ya metali 3) baruti au kemikali yenye uwezo wa kuwaka haraka mara moja ikitoa gesi 4) mguu wa ganda ni pana kwa kushikilia ramia kwenye chemba ya silaha 5) kiwashio ni kemikali linalowaka ikipigwa na moto yake inawasha baruti

Ganda la ramia

Ganda hili mara nyingi ni ya metali ama shaba nyeupe au feleji. Kwa mazoezi kuna pia maganda ya plastiki. Ramia ya bunduki ya marisau huwa pia na ramia ya karatasi ngumu kwa sababu hapa risasi ni ya vipande vingi kidogo isiyobanwa na ganda bali viko ndani ya ramia.

Baruti
Baruti ni kiasi kinachohitajika kwa kurusha risasi kulingana na uwezo wa silaha. Baruti ina uwezo wa kulipuka yaani ya kuchomeka haraka na ghafla iikitoa gesi zinasopanua na kusukuma risasi. Lakini baruti haitakiwi kuwa nyororo mno; ramia sharti ni kuvumulia pigo na mishtuko bila kulipuka. Aina kali sana za baruti zinafaa kwa mlipuko katika uwindo wa mawe bali si kwa ramia.

Kiwashio cha ramia
Kazi ya kuwasha baruti hutekelezwa na kiwashio ambacho ni kiasi kidogo cha kemikali kinachowaka moto ikipigwa vikali. Hufungwa katika silinda ndogo ndani ya mguu wa ramia. Mguu huu unapigwa na msumali wa bunduki na kuwaka moto inayowasha baruti.

Mengineyo
Ramia kwa ajili ya mazoezi kwa mfano kuzoea makelele au kwa matumizi katika filamu hukosa risasi lakini zinatoa kelele na moto kama ramia ya kawaida.

Ramia kubwa za mzinga mara nyingi huitwa "kombora" lakini neno hili latumiwa pia kwa "roketi".
 
View attachment 697403

Nyie ccm kwa kupost ujinga mnaongoza ...Juzi tu mmemuua mwanafunzi wetu .
 
Hakuna CCM hapo....mwanafunzi ameuwawa kweli lakini ni tukio la bahati mbaya hakuna aliyekusudia kusababisha mauaji.
 
Upuuzi unawasumbua mnajiona Mungu watu...Endeleeni nakuwauwa watu mje muone mwisho wake.
 
we. jamaa ujitambui...unaona kukatisha uhai wa binadamu mwenzio ni big deal.
Umeambiwa ni bahati mbaya imetokea tatizo lako ni nini sasa.Wangapi wanakufa au kupoteza maisha kwa bahati mbaya katika kazi zetu za kila siku.

Au hujui kuna wengi sana wanapoteza maisha kwa hali kama hiyo ya bahati mbaya duniani?
 
Na wasiwasi na Jinsia yako? naweza kuwa nabishana na mtu ambaye siyo ridhiki.
 
Hakuna CCM hapo....mwanafunzi ameuwawa kweli lakini ni tukio la bahati mbaya hakuna aliyekusudia kusababisha mauaji.
Usitetee ujinga hakuna bahati mbaya hapo hiyo ilipangwa lasivyo mrudishwe CCP mkafunzwe tena kutumia silaha
 
Acha ubaguzi wewe mwanaume au mwanamke si watu kama watu wengine nyumbani kwako huna kaka zako au dada zako.Au unataka mpaka umwagiwe mayai ndiyo upunguze kuongea.
 
Usitetee ujinga hakuna bahati mbaya hapo hiyo ilipangwa lasivyo mrudishwe CCP mkafunzwe tena kutumia silaha
Silaha ina kazi moja tu kuuwa haijatengenezwa kwa kazi nyingine fahamu hilo kwanza...Tukio umeshaelezwa ni bahati mbaya na wahusika wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua zaidi kwanini walitumia silaha za moto? watatoa maelezo yao then wataalam wataangalia uzito wa tukio na silaha za moto na kuamua nini kifanyike.
 
Sasa kama imeshaua sasa unaweka neno bahati mbaya la nn??Sasa kwanini washikiliwe huku silaha imetimiza kazi yake??
 
Hakuna CCM hapo....mwanafunzi ameuwawa kweli lakini ni tukio la bahati mbaya hakuna aliyekusudia kusababisha mauaji.
Hivi ukipiga risasi kwenye kundi la watu mtu akafa unaweza kusema ni bahati mbaya??

Kabla ya kujibu jitoe upumbafu wote na mihemko na ushabiki wa chama alafu unijibu..

Risasi ingekuwa imejifyatua hio ni bahati mbaya au dada angekuwa amepit kwenye uwanja wa range wa jeshi hio ni bahati mbaya..
Sasa risasi iliyopigwa uraiani ni bahati mbaya kumpiga raia..
 
Hizi zikiingia kwa wingi na raia tukazipata nadhani itapendeza, huo mdundiko tutakaoucheza mtaupenda maana mnachokifanya kwa raia wasio na hatia kitahamia na kwenu pia.
 
Umeambiwa ni bahati mbaya imetokea tatizo lako ni nini sasa.Wangapi wanakufa au kupoteza maisha kwa bahati mbaya katika kazi zetu za kila siku.

Au hujui kuna wengi sana wanapoteza maisha kwa hali kama hiyo ya bahati mbaya duniani?
Hiyo sio bahati mbaya, hakukua na ulazima wa kutumia silaha za moto kwa watu ambao hawakua na chochote wala kuonyesha vurugu. Tatizo ni kuonyesha ubabe na kila mmoja hataki kujishusha.

JK aliwahi kusema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala. Waache wazunguke weee mwisho watatulia wenyewe. Hii nchi tatizo kuna watu wanajiona ni bora na wengine ni takataka
 
Back
Top Bottom