Ijue mbinu ya kijasusi 'honeytrap'

Ijue mbinu ya kijasusi 'honeytrap'

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
680
Mbinu hii ya 'Honey trap' pia hutumika katika kuwatafuta maadui wanaokimbia mkono wa taasisi ya intelijensia. Mfano Mordecai Vanunu (pihani - katikati) ni mmoja kati ya watu waliodakwa kwa mbinu hii. Akiwa nchini Uingereza baada ya kukimbia Israel, Mordecai alipanga kuvujisha siri za mradi wa nyuklia wa Israel kwa vyombo vya habari vya Uingereza, lakini intelijensia ya Israel iliweza kumkamata kabla hajatekeleza lengo lake.

Mwanadada Cheryl Bar-Hanin, myahudi aliyezaliwa Marekani aliteuliwa rasmi kumlaghai Mordecai aliyekuwa akijilinda sana mjini London. Cheryl Bar - Hanin alijitambulisha kama Cindy, na kujilegeza kwa Mordecai Vanunu lakini hakuonesha kiu ya mapenzi. Mashushushu wa kingono wa jinsia ya kike kama Cindy wamebobea katika kuwalaghai wanaume ili wajiongeze mwenyewe. Wakati wa mafunzo yao, hupatiwa zaidi mafunzo ya saikolojia na sayansi ya tabia.

Hata hivyo, Mordecai mwenyewe alikuwa mdhaifu kwa wasichana warembo, na siku moja kabla ya kuchapisha habari ya mradi wa nyuklia wa Israel kupitia gazeti la Sunday Times, alimuomba Cindy watoke kujivinjari. Cindy alimshawishi Mordecai Vanunu wasafiri hadi mjini Roma, Italia na kumuahidi kuwa wakifika Roma watakula raha zao. Mordecai Vanunu alikubali bila hiana. Hakujua ni mtego.

Huko mjini Roma, timu ya majasusi wa Mossad ilikuwa tayari inasubiri Mordecai atie mguu, ndipo wakamtia nguvuni Mordecai na kumrudisha nchini Israel kwa ajili ya mashitaka. Mpaka wakati huo anakamatwa na hata baada ya kushatakiwa, Mordecai hakujua kama Cindy alikuwa ni msichana aliyetumwa na Mossad, hadi alipomaliza kifungo chake miaka 18 baadaye.

Ushushuhu huu wa kingono umekuwapo tangu zamani za kale wakati Delila alipomlaghai Samson, na hata katika ulimwengu wa leo mashirika ya kijasusi hutumia mbinu hiyo dhidi ya serikali au mashirika mengine.

Mathalani kuanzia miaka ya 2000 hadi 2010, shirika la kijasusi la MSS la Uchina liliwatuma mabinti warembo wa kichina wapatao 600 katika nchi za Ulaya, hususani Uingereza kwenda kutafuta mwanya wa kuanzisha mahusiano ya kimahaba na maofisa mbalimbali wa taasisi binafsi na za kiserikali, kwa lengo la kuwalaghai na kuwashawishi wafanye maamuzi yanayosaidia maslahi ya China, sambamba na kuchota taarifa zinazoweza kusaidia serikali ya China katika maamuzi yake.

Kunako Afrika, nchi ya Rwanda imekuwa ikifanya ushushushu wa kingono kwa mataifa mengini yakiwemo mataifa jirani ya Afrika mashariki na kati. Tangu mwaka 2013, mashushushu wa kike wa Kinyarwanda takribani 1300 walisafiri kwa awamu na kwa nyakati tofauti kutoka Rwanda...

Kitabu kinaitwa 'ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA'.

Nunua usome zaidi:
Bei ni Tsh. 35,000/= tu popote Tanzania.

Piga simu:
0713933736
0745830775
0713606062

Dr. Chris Cyrilo
 
Rwanda mwaka huu inamake headline Sana hasa KWENYE hili lengo lake
 
Hii mbinu inatumika kwa mtu unaemjua na kumsoma kwamba ni mlevi wa wanawake. Hakuna anaemjua kigogo kama ni Me au Ke.
Hahahaa kweli ukiwa mlevi wa wanawake lazima udakwe kama kuku mwenye kideri.
 
Tatizo huyo jamaa alikosa focus...wee umeenda uk kwa jambo lako unaziba mambo mengine yote...huyo hakiwa serious
 
Back
Top Bottom