Ijue maana ya #HapaKaziTu

Ijue maana ya #HapaKaziTu

Na ndio maana hawataki kutoa elimu bora kwa waTz, wanataka tuendelee kuwa wajinga ili waendelee kututawala kijinga
 
Nini maana ya #HapaKaziTu ?

Ukisema HapaKaziTu kuna watu watakuuliza unasema hivo mbona hauna ajira? Kazi na ajira ni vitu viwili tofauti ingawa kwa kiasi Fulani vinaweza kufanana kwakuwa kila aliyeajiriwa anafanya kazi lakini si kila afanyae kazi ameajiriwa.

Dhana ya HapaKaziTu inaambatana na uwajibikaji kwenye kila jambo. Ili kuleta maendeleo ya kasi Watanzania tunapaswa kuwa na Rais mwenye uwezo MKUBWA wa kufanya kazi kwa bidii, kujituma kwa moyo wote na uzalendo wa hali ya juu.

Wananchi nao wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kwa kuiga mfano wa kiongozi wao. Tunaposema kazi tunakusudia kazi yoyote aifanyayo mtu kama kulima, kujenga, kuongoza watu n.k na wala siyo kuajiriwa tu.

China na Japan zilipata maendeleo makubwa walipoamua kufanya kazi kwa bidii kwenye kilimo, viwanda, uvuvi na hata kwenye utumishi wa umma.

Ili tupate MABADILIKO ya kweli tunahitaji vitu viwili;

1. kiongozi mchapakazi atakayefanya kazi kubwa ya kupambana na MAFISADI wote nchi nzima

2. Raia wanaojituma kweli kweli

Hii ndiyo maana ya kaulimbiu ya #HapaKaziTu , kila mtu atafanya kazi kwa bidii popote alipo kuanzia wanafunzi shuleni, waliojiajiri kwenye miradi yao hadi watumishi wa umma ofisini.

Hakuna asiyehitaji MABADILIKO, lakini mabadiliko ya kweli yatakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na kukomesha UFISADI.

Tumchague Dr. John Magufuli tupate MABADILIKO ya kweli kwa kufanya kazi na kujituma

#HapaKaziTu


Kauli mbiu mpya kila siku ningependa kujua

Maisha bora ilifia wapi maana hakuna mrejesho

Kilimo kwanza je ??
 
Ni kauli ya kimadharau sana baada ya kudanganya maisha bora kwa kila mtanzania kushindikana
 
Uvivu na ujinga hautolewi na hapa kazi tu bali elimu elimu elimu futa tongotongo kwa macho yako

Kwani shule, zile za kata, vyuo, UDOM hakikuwa katika ilani ya JK lakini kimejengwa, au umejenga wewe na familia yako
 
watanzania ni wamoja sasa unataka nimtenge huyo mwenye elimu ndogo? cha msingi tutofautishe kwa hoja zetu utajua na wewe pia tutakupa elimu bora na bure usijali

Mimi nimesoma mpaka chuo kikuu, familia yangu ya hali ya chini ila nimesoma, sasa unaposema elimu, elimu ipo ni kama bure, ila nyie mnaposema elimu bure bila mikakati manfail, hal ya kuwa mikakati ya kukitunza CDM hamna, mnawachangisha raia tu
 
Acha kung'ata maneno ,je kwaualisia je mtu ambaye hana ajira nae akubaliene na huo usemi ? Coz tukichukulia kazi kwa wigo mfinyu m2 anaye zurura mitaani naye atasema kafanya kazi ya kuzurura.
 
…kwa ufafanuzi huo nidhahili hamjaeleweka na hakuna dalili ya kueleweka, watu wanataka "MANADILIKO"… .
 
Kwani shule, zile za kata, vyuo, UDOM hakikuwa katika ilani ya JK lakini kimejengwa, au umejenga wewe na familia yako
nani kakudanganya kuwa elimu ni majengo tu au unaielezeaje elimu ya shule za kata pia hata vyuo vikuu baadhi hasa kwa kozi za science hapa tz?
 
Hapa kazi tuu. Sera safi na mipango murua tutaazima kwa malofa.
 
nani kakudanganya kuwa elimu ni majengo tu au unaielezeaje elimu ya shule za kata pia hata vyuo vikuu baadhi hasa kwa kozi za science hapa tz?

Sasa bila majengo utasoma wapi? Maana mpaka sasa naona watu wanalalamika kuna shule zinasoma chini ya miti, sasa kama shule si majengo si wasome tu chini ya miti.

Na kuhusu vyuo, hata huko nje vipo vyuo vinatoa elimu nzuri na ya kawaida, na ndio maana hua tunachagua, chuo cha UDSM hapa Tz kime rank katika top ten na muda mwingine top five, miongoni mwa vigezo huangaliwa, ni kiwango cha elimu katika masomo ya sayansi. Sasa unaposema elimu mbovu unakosea, yapo mapungufu kwa kuwa bado tunaendelea, development is a gradual change mzee
 
Back
Top Bottom