Ijue likizo ya hedhi Zambia

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Nchini Zambia kuna sheria za wafanyakazi zinazowaruhusu wanawake walio katika hedhi kuchukua siku moja ya mapumziko inayojulikana kama
'Mothers day'

Wanawake nchini Zambia hawalazimiki kufanya maandalizi yoyote kabla ya kupumzika siku hiyo, lakini wanaweza kupiga simu siku hiyo kusema wanachukua Mothers day na muajiri anayewanyima wafanyakazi wake siku hiyo anaweza kushtakiwa.

Sheria hiyo haina masharti, wanawake wanaweza kuchukua siku hiyo kwa matakwa yao wenyewe na sio lazima watoe kithibitisho chochote cha kimatibabu, hatua inayowalazimu wengine kuhoji kuhusu sheria hiyo.

'Nadhani ni sheria nzuri kwa sababu wanawake hupitia mengi wakati wanapokuwa katika hedhi'', alisema Ndekela Mazimba ambaye anafanya kazi katika idara ya mahusiano ya uma.

Bi Mazimba hajaolewa wala hana watoto lakini huchukua siku yake ya Mothers Day kila mwezi kutokana na uchungu/maumivu anayopata wakati anapoingia katika hedhi hasa kwa siku ya kwanza hai inayowafanya wanawake wengine kulazimika kulala siku nzima wakigugumia
period-e1483542362853.jpg

Hata hivyo kumekuwapo na msigano wa mawazo miongoni mwa walengwa wa sheria hiyo na jamii kwa ujumla huku wengine pia wakiitumia vibaya kwa kudanganya (kisingizio ikiwa una mingo zako) na wengine wakiikosoa kwamba inaongeza uvivu na kupunguza tija kwa taifa

Ikumbukwe pia kwamba Zambia ni moja ya nchi zenye likizo nyingi ikiwemo LIKIZO YA SIKU YA MAOMBI
Zambia-holiday-mothers-day-women-
 
Ingekuja huku hiyo sheria pasingetosha.Kiswahili saa nyingine hakina staha eti mothers day,mtu anakutamkia tu neno lilivyo.
 
na ugumu huu wa maisha mkuu
Si ndio vizuri,ili wanawake wakae nyumbani kwa kukosa kazi,we unadhani nani atakubali kumwajiri mtu wa kukaa nyumbani siku 10 kwa mwezi,siku 2 kila wiki + 2 za hedhi =10.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom