Ijengwe shule moja ya computer kila Kata

Kingdom123

Member
Aug 13, 2020
25
49
Ili kukabiliana na changamoto moja kubwa iliyosahaulika ya ujinga juu ya matumizi ya computer kwa vijana wengi wa Kitanzania, napendekeza angalau kuwe na shule moja tu kila kata itakayowekwa computer hata 100 ambapo itawekwa ratiba ya ushirikiano kwa shule zote ndani ya kata wanafunzi kwenda kufundishwa katika shule hiyo.

Yaani shule hiyo itahudumia shule zote kwa ratiba maalum. Naona hii ni bora kupunguza gharama za kuwezesha kila shule kuwa na darasa lake.

Wizara ya Elimu na Serikali iliangalie hili. Angalau watoto watoke na ujuzi wa computer katika kipindi hiki cha teknologia.
 
Computer mia moja kwa pamoja uziweke Vikindu wahuni watahama nazo baada ya wiki tu.
 
Ili kukabiliana na changamoto moja kubwa iliyosahaulika ya ujinga juu ya matumizi ya computer kwa vijana wengi wa Kitanzania, napendekeza angalau kuwe na shule moja tu kila kata itakayowekwa computer hata 100 ambapo itawekwa ratiba ya ushirikiano kwa shule zote ndani ya kata wanafunzi kwenda kufundishwa katika shule hiyo.

Yaani shule hiyo itahudumia shule zote kwa ratiba maalum. Naona hii ni bora kupunguza gharama za kuwezesha kila shule kuwa na darasa lake.

Wizara ya Elimu na Serikali iliangalie hili. Angalau watoto watoke na ujuzi wa computer katika kipindi hiki cha teknologia.
pia ili wataalam wa IT tupate ajira za kuzifanyia maintenance na installations
 
hizo gharama za ujenzi na tendering process zinatosha kabisa kuwezesha kila shule kua na computer hata ikibidi zile za mtumba
 
Kuna mradi wa mabeberu ulitoa tablet kwa kila mtoto kwenye kila kaya baadhi ya vijiji ya handeni na wakawafungia na solar.
Zile tablet zimejazwa nyimbo za Dayamond na bongo movie.
 
Yaani niache kujenga barabara za rami chato, niweke bajet huko kwenye comfuta hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Hivi hamjui kama mambo yamebadilika
 
Back
Top Bottom