Igunga, Tabora: Majambazi 6 wavamia msikiti na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia msikiti mkuu wa Igunga mjini, Mkoa wa Tabora na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu vya dini ya kiislaam.

Mlinzi aliyejeruhiwa ni Juma Mussa (55),mkazi wa Mtaa wa Nkokoto ambaye amelazwa wodi namba nane katika Hospitali ya wilaya ya Igunga.

Akizungumza kwa shida akiwa wodini hapo mlinzi huyo alisema tukio hilo limetokea juzi saa 8.00 usiku ambapo watu hao walifika msikitini hapo kisha kurusha jiwe kwenye eneo alilokuwa amekaa.

Alisema baada ya kuona jiwe hilo aliamua kusimama ambapo jambazi mmoja aliruka uzio wa msikiti kisha kuingia na kuanza kumshambulia kwa mapanga kichwani.

Mussa alisema kwamba wakati akishambuliwa aliona watu wengine wakifungua milango ya msikiti huo huku mmoja wao akimwambia mwenzake kuwa "wewe maliza kabisa huyo mlinzi".

Hata hivyo mlinzi alisema kwamba aliendelea kuomba msaada wa kupiga kelele ili aweze kusaidiwa hali iliyosababisha majambazi hao kukimbia kusikojulikana.

Mhasibu wa msikiti mkuu wa Ijumaa wilaya ya Igunga, Issa Feruzi, alitaja vitu vilivyoibiwa ni Misahafu minne, feni moja, saa kubwa, vitabu vya hitma juzuu 30, kitabu cha mapato na matumizi, Daftari za Tabligh nne, vipaza sauti, miswala miwili, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 374,000.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Igunga, Melchades Magongo, alikiri kumpokea Juma Mussa.

Alisema kwamba akipokewa akiwa na majeraha kichwani ambayo yanaonyesha alikatwa na kitu chenye ncha kali.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari mshtakiwa mmoja amekamatwa na polisi.

Alisema kwamba vitu vilivyoibiwa vimekamatwa na vinashikiliwa polisi na kueleza kwamba hakuna jambazi atakayetoka salama Igunga kwa kuwa polisi wamejipanga kikamilifu kukabiliana na matukio kama hayo.

Chanzo: TanzaniaDaima
 
Wasomewe ALBADIR hao "manyang'au"

Mkuu hio Ngoma itapigwa kimyaa kimyaa
Siku moja kuna kibaka alipitia baskeli yaMaalim alikua akisalisha na viatu vya waumini msikitini, wilaya ya urambo mkoa tabora,hakumaliza siku 3
Alionekana akiendesha baskeli akiwa uchi kavaa kibaragashia tu huku nyuma kavipakia viatu akielekea ktk huo mskiti huku akiimba kaswida
Tokea hio siku niliwainulia mikono
WANYAMWEZI
 
Mkuu hio Ngoma itapigwa kimyaa kimyaa
Siku moja kuna kibaka alipitia baskeli na Maalim alikua akisalisha na viatu vya waumini msikitini, wilaya ya urambo mkoa tabora,hakumaliza siku 3
Alionekana akiendesha baskeli akiwa uchi kavaa kibaragashia tu huku nyuma kavipakia viatu
:oops::oops: du! Kumbe albadir ina react haraka sana!
 
Daah sijui walikua na lengo gani hawa majambazi , unaweza kujiuliza bila majibu, ila Jambazi haachi kitu, huenda walicho kikusudia walikikosa wakaamua kusepa hata na vitabu tu.
 
isije ikawa ni Mashekhe wanao swalisha huo Msikiti wanapigania maslai yao binafsi wameshindwa kuelewana wakaona bora wafanye undava undava wote wakose.....
 
Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia msikiti mkuu wa Igunga mjini, Mkoa wa Tabora na kumjeruhi mlinzi kisha kupora baadhi ya vitu vikiwemo vitabu vya dini ya kiislaam.

Mlinzi aliyejeruhiwa ni Juma Mussa (55),mkazi wa Mtaa wa Nkokoto ambaye amelazwa wodi namba nane katika Hospitali ya wilaya ya Igunga.

Akizungumza kwa shida akiwa wodini hapo mlinzi huyo alisema tukio hilo limetokea juzi saa 8.00 usiku ambapo watu hao walifika msikitini hapo kisha kurusha jiwe kwenye eneo alilokuwa amekaa.

Alisema baada ya kuona jiwe hilo aliamua kusimama ambapo jambazi mmoja aliruka uzio wa msikiti kisha kuingia na kuanza kumshambulia kwa mapanga kichwani.

Mussa alisema kwamba wakati akishambuliwa aliona watu wengine wakifungua milango ya msikiti huo huku mmoja wao akimwambia mwenzake kuwa "wewe maliza kabisa huyo mlinzi".

Hata hivyo mlinzi alisema kwamba aliendelea kuomba msaada wa kupiga kelele ili aweze kusaidiwa hali iliyosababisha majambazi hao kukimbia kusikojulikana.

Mhasibu wa msikiti mkuu wa Ijumaa wilaya ya Igunga, Issa Feruzi, alitaja vitu vilivyoibiwa ni Misahafu minne, feni moja, saa kubwa, vitabu vya hitma juzuu 30, kitabu cha mapato na matumizi, Daftari za Tabligh nne, vipaza sauti, miswala miwili, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 374,000.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Igunga, Melchades Magongo, alikiri kumpokea Juma Mussa.

Alisema kwamba akipokewa akiwa na majeraha kichwani ambayo yanaonyesha alikatwa na kitu chenye ncha kali.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari mshtakiwa mmoja amekamatwa na polisi.

Alisema kwamba vitu vilivyoibiwa vimekamatwa na vinashikiliwa polisi na kueleza kwamba hakuna jambazi atakayetoka salama Igunga kwa kuwa polisi wamejipanga kikamilifu kukabiliana na matukio kama hayo.

Chanzo: TanzaniaDaima
hayo majambazi mbona yana vituko hivyo? yaani yanaiba misahfu hayamuogopi Mungu?
 
Back
Top Bottom