Igunga na changamoto zake

Kwaroz

Member
Aug 30, 2009
55
10
Kwa kipindi cha wiki kadhaa saa tumesikia habari za kufurahisha na kuchukiza ndani ya Igunga lakini kwa wanamapinduzi au wanaharakati tunaona kwamba sasa tunaelekea kwenye kutatua matatizo ya msingi ya jamii zetu kwa kila mwanajamii kuona kwa macho tena mchana kweupe kuwa kuna kitu si cha kawaida kinatendeka.

mkuu wa wilaya
tukianza na taratibu za kisheria unaona wazi kuwa anamakosa tena makubwa kwa kukiuka taratibu na shreria za uchaguzi pia amekiuka katiba ambayo ameahidi kuilinda tena alishika kitabu kitakatifu katika kuapa siku alipoapishwa lakini kwa sasa tunaona kwa maswali ya ziada alitakiwa kujibu.

askari polisi
sikujua kwamba akishikwa muheshimiwa akifanya makosa ni kumdhalilisha na akishikwa mwanajamii kama alivyoshikwa muheshimiwa kuwa si kosa, kwa nini nchi hii aizingatii utawala wa sheria? wakishikwa wao ni nchi ya utaratibu na tukishikwa sisi ni tofauti kabisa na maneno yao. ni wahalifu wangapi wanashikwa kwa stahili ya mkuu wa wilaya mpaka jeshi la polisi wanatoa zawadi kwa raia wema? nini maana ya polisi jamii au m imi sijaelewa na sielewi maana yake na mahudhui yake ndani ya jamii yetu.

vyombo vya habari
naona kuna utitiri wa vyombo vya habari havitaki kwenda mbali zaidi ya taarifa za wanasiasa na kwenda kuchimba nini chimbuko au kuna kosa lipi ambalo limetendeka tulisshughulikie ili hata kesho mwingine akifanya ajue madhara yake lakini wapi kila chombo cha habari kinasema jinsi kinavyoona kuwa ni sahihi. pia hata jukwaa la kujieleza ndani ya vyombo vya habari si sawa wanatulazimishe tuwasikilize wao tu na si upande wa pili.

mabadiliko
jana nilikuwa napitia kwenye yutube na bahati nzuri nimekuta kuna habari zaidi za kiuchaguzi Igunga na habari zingie ambazo sijawahi zisikia katika vyombo vya habari nawashauri wanaharakati unaweza angalia hapo kwa kuandika neno Igunga utapata habari ambazo hatujawahi hati ambiwa au hazijaandikwa kwenye magazeti wala kusikika kwenye redio au TV.

nawakilisha
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
Ya Igunga anatakiwa aarifiwe Moreno Ocampo kabla hali haijawa tete tuzuie umwagaji wa damu za watanzania kabla haujatokea inatisha namie nimeona habari za makambi na mafunzo kwa vijana inatisha sana
 

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
6,723
12,476
Igunga imeweka historia ya jinsi unafiki ulivyo: wanamponda RA baada ya muda
wanamtumia kwenye kampeni huku wakimzuia Nape kwenda huko ili RA asichukie!
It's like a movie...
 

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
886
60
Kweli yametukuta wana ccm wenzangu inabidi tufike mahali tuanze kuangalia wapi tulipopotea ili tujijenge upya kwa kipindi hiki cha miaka mitatu na nusu iliyobakia ili tuendelee kukaa madarakani kwa muda mrefu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom