Igunga.. Kunaweza kukaongeza idadi ya ujinga

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,489
907
View attachment 37000
Nina shaka sana, kwani WANA JF, huyu Rostam, kwenye speech yake toka.. matukio-michuzi: kauli ya mbunge wa igunga Mh Rostam Aziz wakati akijiuzulu leo, si ndiye aliyesema siasa ndani ya ccM ni uchwara, si yeye aliyejivua nyadhifa zoote ndani ya chama hicho, si ndiye yeye aliyejitamba kwamba ni sampuli ya wafanya biashara nguli wa kimataifa, sasa mbona huyu baba tena yuko miongoni mwa hao aliowaita wanafanya siasa uchwara.. mie nakaribia kutoelewa sana siasa za kwetu zikoje.. tena wakati anajiondoa kwenye chama, hakuvaa kijani ya aina yoyote, ila leo anaonekana front table, baba wa watu akivinjari na katuvalia kijani.. nadhani kuna tatizo kubwa ndani ya vichwa vya wenye chama hiki.. Hivi huyu mwenzetu, hajali kabisa ni gharama na usumbufu kiasi gani ameuingiza kwa chama chake, tena kwenye wakati huu mgumu ambao chama chake kinajikongoja na matatizo mengi yanayokiyumbisha chama na serikali, ikiwemo mfumuko wa bei za vyakula vya masingi, mafuta na migao ya umeme.. na yeye hapo hapo anakunjuka na kuachia ubunge kiasi cha kuleta hamaki ndani ya chama chake na wanajibanabana kupambana kukirejeshea chama heshima kwa ushindi huko jimboni, kisha yeye anakenua, anapiga nne, anachekelea, na tena wanamwanika mbele kabisa.. aih ni aibu si kwa chama bali pia taifa na zaidi ya yote kumdhalilisha rais wetu mstaafu aonekane naye bogas.. hapana no.. yako mabaya aliyoyafanya rais wetu huyo mstaafu, ila yako mengi mazuri pia ameyafanya, sidhani ni busara chama kumdhalilisha namna hiyo, kumweka MEZA moja mbele na mtaabishaji wa wao ndani ya chama.
tena huyo mbaba, aliyekuwa mweshimiwa, haoni ni hasara gani Tume ya uchaguzi itaingia kupoteza fedha za walipakodi kugharimia uchaguzi huo, jamani mie sielewi kama hii ni siasa au ujinga na upumbavu.. ni kweli chama twala kinaweza kuwa na mapungufu kadhaa ila si kwa kiwango cha upofu wa kushindwa kuliona hata HILI..
BE SMART TZ
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom