Elections 2010 Igunga: Je, Waziri Nahodha naye kaenda 'Kuongeza Nguvu' ya kampeni za CCM?

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Wana JF,

Nafuatilia siasa za Igunga. Hivi sasa mawaziri wamehamia huko. Hivyo imedhihirika kuwa wapinzani sasa wanapambana na serikali siyo CCM. Hivyo, ni kitu gani kitakachomzuia Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha kukipigia kampeni chama chake kama wanavyofanya mawaziri wengine? Tena, mawaziri wenzake wamejipambanua kabisa kuendesha kampeni hizo kwa kutumia mamlaka waliyonayo ya kiserikali. Imefika wakati wanajisahau hadi wanatoa kauli kama vile tutaweka bajeti maalumu. Kwamba, huyu ndiye nitafanya naye kazi. Serikali ni ya CCM. Kauli hizi siyo tu zinavunja sheria lakini pia, zinachochea uhasama na uadui mkubwa kwani zinaonyesha kuwa serikali inaendeshwa kwa misingi ya kibaguzi kutokana na itikadi ya vyama. Kama serikali inasema kuwa akishinda mpinzani serikali haitoi ushirikiano hapo tumefika wapi? Ama kama serikali inatamka wazi kuwa bajeti iliyopo ni ya chama fulani maana yake kuwa, wananchi wasio wa chama hicho bajeti hiyo haiwahusu? Basi kama hivyo ndiyo, serikali hii itafika wakati itakosa uhalali wa kukusanya kodi wa watu ambao hawatoki chama husika. Lakini, kubwa zaidi kauli hizi ndizo zinasababisha serikali kuchukiwa zaidi.

Hivyo sasa, tujiulize Nahodha kwa nafasi yake, je atajizuia kukisaidia chama chake? Je, yeye ni Malaika wa kuweza kulinda heshima yake ya Uwaziri wa Polisi asiingie kwenye lindi la akina Magufuli na Wasira ambao wametangaza wazi kabisa kuwa nyadhifa zao zipo pale kuitumikia CCM? Ngoja tuone!
 
Hilo mkuu limeonekana na kiukweli linakera sana na ni siasa za ubaguzi na ni dhahiri upinzani unapambana na serikali,na kwa kauli hizo natamani tulipe kodi kwa kufuata itkadi za vyama na matumizi tupange kwa itikadi za vyama.maana kauli hizi hazikubaliki hata kidogo,hii inanikumbusha kipindi cha nyuma wakati ilipotmkwa kwamba ukitaka kufanikiwa hata katika biashara chagua CCM.
Na kwa jinsi walivyobanwa hawa magamba kama uchaguzi ungelikuwa bado mwezi hivi basi hata mkuu wa kaya angepiga kambi huko.
Kiukweli inaumiza sana kuona ukikwaji wa sheria wazi wazi lakini hakuna anaechukuliwa hatua.ila yanamwisho haya!
 
Mkuu ni kweli kabisa unayoyasema, huyu Vuai amekwenga Igunga kupiga kampeni ia kuweka mazingira mazuri ya kuigiza masanduku feki ya kura, kuwahamasisha polisi kuwadhibiti Chadema ili CCM wachakachue matokeo.
 
Jamani inaonekana mapambano ya kuleta mabadiliko yanaanza na kuishia tu huku kwenye mitandao kwa mtu mmoja mmoja, lini tutapata ujasiri wa jumla kuchukua taifa letu toka kwa madhalimu hawa kwa kutumia mikono na miguu badala ya computer?
 
Njia ya kuchukua ndiyo hiyo ya kupiga kura za mabadiliko.


Jamani inaonekana mapambano ya kuleta mabadiliko yanaanza na kuishia tu huku kwenye mitandao kwa mtu mmoja mmoja, lini tutapata ujasiri wa jumla kuchukua taifa letu toka kwa madhalimu hawa kwa kutumia mikono na miguu badala ya computer?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom