Igunga itumike kama PILOT study | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga itumike kama PILOT study

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Aug 17, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana, tulishuhudia malalamiko mengi ya vyama vya upinzani hususan CHADEMA juu ya uchakachuaji wa matokeo ikiwemo ngazi ya ubunge. Ni miaka minne tu sasa tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu.

  Ni matumaini yangu kuwa CHADEMA watakuwa wamekaa na kubaini namna ya kudhibiti wizi na uchakachuaji wa kura in an affordable and feasible way. Nitakishangaa sana chama changu hiki kama baada ya uchaguzi wa Igunga, kutakuwa tena na malalamiko ya kuibiwa kura au kupokonywa ushindi.

  Najua katika achaguzi uliopita, katika baadhi ya maeneo ilibidi kutumiwa nguvu za ziada kulinda ushindi wa CHADEMA. Ni matumaini yangu kuwa chama kimesha-analyse na kujua ni katika situation gani unatakiwa kutumia mbinu gani kujilinda.

  Igunga itakuwa kielelezo kizuri cha ku-apply the best techniques za kulinda kura kwa sababu naamini magamba watakuwa wanafanya kila mbinu kuhakikisha wanalibakiza jimbo. Haimaanishi kuwa CDM hawataweza kushindwa kihalali (chochote kinawezekana), lakini tunataka kuona Igunga inakuwa mfano kuwa "hatuko tayari tena kuibiwa kura au kupokonywa ushindi kirahisi".

  Na katika hili, naomba uongozi wa juu na wabunge wasijihusishe moja kwa moja katika kulinda kura, bali wawaelimishe wanachadema wa kule cha kufanya, then wao wawe wana-overcheck kwani mwaka 2015 hawatakuwa majimboni, so wanatakiwa waangalie kama mbinu wanazopendekeza ni applicable at the grassroot. Hata hivyo wawe makini maana team nzima ya CCM itakuwa huko.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  UKO SAHIHI MKUU, kuendelea kulalama kuibiwa kura after every election haitakuwa na tija, tutegemee CDM wawe na mikakati thabiti hasa baada ya experience ya kilichotokea mwaka jana. na kuhusu viongozi/wabunge kutojihusisha ktk "ulindaji" kura bali waelimishwe watu (common people) hiyo isiishie Igunga tu bali nchi nzima,,haitakuwa ajabu kuona 2015 tunafanya uchaguzi ktk katiba na tume ya uchaguzi hii hii ya sasa ambayo haijawahi kuwa fair and free!
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu umenena ukweli kabisa. Cha msingi ni wananchi wapiga kura kuweza kupewa semina elekezi ya jinsi ya kulinda kura zao na kulinda matokeo baada ya kumaliza kupiga kura. Hizi mbinu zote wapewe kipindi cha kampeni!
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwel mkuu. Hivi sasa tupo katika zama za sayansi na teknolojia. nadhani kuna kila sababu za kubuni mbinu za kisayansi (ikiwemo sayansi ya jamii), kulinda kura
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri, japo ni mapema sana. Japo unawashauri CDM kutumia Igunga kama Pilot at the same time CCM nao wanaitumia kama pilot ya wizi wa kura. Mkuu PILOT hizi zitakuwa nyingi sana, kabla ya 2015 tutarajie chaguzi ndogo 10 au 12 za ubunge.
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndugu hayomawazo hayako kwa ccm ambao ndiyo wanao haribu uchaguzi.
   
Loading...