Igunga: Dk Slaa aionya CCM, ikikata rufaa itaumbuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Dk Slaa aionya CCM, ikikata rufaa itaumbuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by p_prezdaa, Aug 26, 2012.

 1. p_prezdaa

  p_prezdaa JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Chadema yatingisha

  Sunday, 26 August 2012 | Mustapha Kapalata, Igunga

  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chamacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wananchi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa ushiriki wao katika kufanikisha kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga jana.

  YAFANYA MKUTANO MKUBWA IGUNGA KUSHUKURU WAPIGAKURA,DK SLAA AIONYA CCM IKIKATA RUFAA ITAUMBUKA

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara ikiwa ni mara ya kwanza tangu Mahakama Kuu Kanda Tabora kutengua ubunge wa Dk Dalaly Kafumu wa Chama Cha Mapinduzi, huku kikiionya CCM kuwa kitaumbuka iwapo kitakata rufaa kwa uamuzi huo wa mahakama.

  Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Sokoine, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema CCM kisithubutu kukata rufaa kwani kitaumbuka kwa kuwa kilicheza faulo nyingi katika uchaguzi huo.

  Alisema ameshangazwa na kauli ya CCM kusema kuwa kitakata rufaa katika kesi hiyo wakati kisheria, kwa kesi za uchaguzi na pia katika hatua hiyo chama hakina nafasi yoyote bali mgombea au mwanachama wa chama husika, ndiye anayeweza kwenda mahakamani kufungua kesi na kupinga.

  Katika mkutano huo uliofurika maelfu ya wanachama na washabiki wa wa chama hicho, Dk Slaa alisema kuwa Chadema kitakiangusha vibaya CCM hata ikiwa uchaguzi katika Jimbo la Igunga utarudiwa.

  Huku akitoa mifano mbalimbali ya jinsi baadhi ya wanachama wa CCM walivyokuwa wakitoa rushwa, Dk Slaa alimtuhumu Mweka Hazina wa chama hicho, Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi kwamba alikuwa kinara wa kutoa rushwa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga Oktoba mwaka uliopita.

  "Chadema imejipanga kwa rufaa hiyo ya CCM ikiwa ni pamoja na kufungua kesi nyingine dhidi ya vigogo wa CCM, walioshiriki katika kampeni za uchaguzi huo,"alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa pia alimponda Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akieleza kuwa mdomo wake umemponza kwa sababu alikuwa akizungumza mambo ambayo hakujua madhara yake.

  Wakati akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Mary Nsimbo Shangali wa Mahakama Kuu alisema moja ya hoja saba zilizotolewa na Chadema ambayo mahakama iliikubali ni ile ya Mukama kudai Chadema kilipeleka makomandoo katika uchaguzi huo na kupanga kuuvuruga.

  Dk Slaa alisema: "Mukama alikurupuka kwa kutamka maneno bila kufanya utafiti hali iliyosababisha CCM kupoteza jimbo."

  Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa suala la CCM kuingiza silaha ndani ya nchi, bila kibali wala leseni na kuwapatia vijana wake mafunzo katika kambi za Ilemo, Iramba mkoani Singida linamhusu mwenyekiti wa chama hicho na siyo mtu mwingine.

  Alidai kuwa wakati wa uchaguzi wa Igunga, vijana hao walikuwa wakipewa mafunzo ya kijeshi akisisitiza kuwa suala hilo linamhusu mwenyekiti wa chama hicho akimtaka atoe majibu na ufafanuzi juu ya hilo.

  Dk Slaa alisema kuwa siku ya jana ilikuwa ni kwa ajili ya wananchi wa Igunga kusherehekea na kupongezana kwa mshikamano waliouonyesha wakati wote wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, huku akitoa pongezi kwa mawakili waliosimamia kesi hiyo kwa kuiwakilisha vyema Chadema katika kesi hiyo.

  Naye upande wake aliyekuwa mgombea wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Igunga Oktoba mwaka uliopita, Joseph Kashindye aliwashukuru wananchi walioiunga mkono Chadema akieleza kuwa wameonyesha ushirikiano mkubwa uliokipa ushindi chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

  Kashindye aliwashukuru pia wananchi wa Igunga kwa kukichangia Chadema Sh6 milioni zilizosaidia kulipia gharama za kesi hiyo pamoja na malazi kwa mashahidi mbalimbali waliotoa ushahidi kwenye kesi dhidi ya CCM iliyotolewa hukumu wiki iliyopita kwa kutengua ushindi wa Dk Dalaly Kafumu wa CCM.

  "Mahakama imetenda haki kwa kuwa imetoa hukumu ya haki…, nimeamini kuwa haki ya mtu haipotei. Awali nilidhani kuwa mahakama ni mali ya CCM kumbe si kweli," alisema Kashindye na kushangiliwa na mamia ya watu waliofurika katika uwanja huo.

  Kashindye aliponda ahadi zilizokuwa zikitolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwamba ndizo zilizofanya CCM kushindwa kesi.

  "Watu wa ajabu sana, wametoa ahadi za kujenga madaraja, kusaidia chakula wakati hilo ni jukumu la Serikali," alisema Kashindye akionyesha kushangaa.

  Alibainisha kuwa wakati kesi hiyo ikinguruma mahakamani, alikuwa akitafutwa na wanachama wa CCM, lakini kutokana na kujua mbinu zao, aliamua kujichimbia kusikojulikana.

  Dk Kafumu aliibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana kuziba nafasi ya Rostam Aziz ambaye alijiuzulu kwa madai kwamba anaachana na siasa chafu ndani ya CCM.

  Katika uchaguzi huo kulikuwa na upinzani mkubwa kati ya Dk Kafumu na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye ambaye hakuridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, hivyo kuamua kupinga matokeo hayo mahakamani. Kesi hiyo ilifunguliwa Machi 26, mwaka huu.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  m4c for life!!
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  ccm wakikumbuka kipigo cha Arumeru Mashariki hawana ubavu wa kupambana na CDM kwenye uchaguzi mdogo sasa hivi. Watajitahidi kwa mbinu zote hata za kukata rufaa ili kuchelewesha uchaguzi.
   
 4. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ccm sasa mbinu walio nayo ni ya kupandikiza watu chadema tu kwa wingi hawana mbinu nyingine sisi wananchi tuwe makini kuwasaidia chadema dhidi ya mapandikizi maana kazi ya utambuzi wa watu wabaya haiwezi kubainishwa na viongozi peke yao hawatoshi hizi mahakama na jeshi la polisi waalimu madaktari na watumishi kwa ujumla hao sasa hawarubuniki kirahisi ila polisi wakubwa hao ni ccm kabisa kuna vijana wanjifanya ni M4C kumbe wao ni mali ya watu kwenye chama hao wananunulika na kufanya kazi za watu tuwe makini chadema tuisaidie ishinde
   
 5. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  maana hata mahakamani wanaenda ili mradi wapoteze muda tu na kutafuta namna ya kulaumu majaji
   
 6. m

  majebere JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Bla bla nyingi tu huyu mzee. Igunga haitakuja kuchagua CDM.
   
 7. C

  CAT5 Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu wewe majembe kama ni mpenzi wa mpira kuna statistics zinaonyesha
  P,W,L,D.GD n.k sasa naomba utumie GD ktk mechi iliyopita kati ya huyo
  ccm na cdm kwa hapo igunga pamoja na ukiukwaji wote mkubwa uliofanyika akiwemo na DC
  kuwa na vikao hadi nyumba kwa nyumba ilishiaaje?
  Washauri CCM uone hata kesho CDM haitapigia kampeni kwa uchaguzi wowote utaorudiwa
  hapo kwa mgombea wake na jibu utajiju mwenyewe.
   
 8. U

  Udaa JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  M4c ukijimlisha na madudu wanayoyafanya sisiem wenyewe,2015 kiulain magogoni.mjengoni kama ndo usipime.
   
 9. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo kwa kushinda kesi,ndio mwl Kashindye ameamini Mahakama ni huru na si mali ya CCM?
  Je,kule kwa Lema anasemaje?
  Sijamuelewa hata kidogo.
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Unakaa huko madongo kwinama lakini bado unapenda kutusemea watu wa Igunga? au ndo kujifurahisha kwenu?
   
 11. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mnakata rufaa ya nini wakati mlishindwa kumpeleka magufuli kutoa ushaidi.
   
 12. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kama kawaida nautaka uwakala CDM
   
 13. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Majebere una matatizo wewe Igunga ya sasa sio ya zamani uchaguzi ukifanyika CCM hata wakiiba kura haziwezi kutosha wananchi wamebadilika sana ndugu.
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,157
  Trophy Points: 280
  Huyo kafumu historia yake alikuwa kwenye sehemu yenye sifa na kutokuwa na uadilifu wa maadili ya kazi haswa Mikataba mobovu na hakika hapendwi na watu wa Igunga na uhakika wamefurahishwa kutolewa kwake...
   
Loading...