Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,085
- 38,460
Huwezi ukaenda una shida hata ya RB wanataka pesa, hivi karibu niliibiwa mbao sehemu. Nafika bila aibu anataka alfu 30 akakamate mwizi, nikawambia na bajaji, nawajua wahusika, ni aibu sana nikaondoka wakati naondoka akaniita mmoja akadai nimpe namba ya simu atanipigia anasubiri askari warudi toka mahakamani.
Inasikitisha sana jeshi la polisi kufikia hatua hii, pale kituoni nimekuta mama mmoja aliibiwa na housegirl anaomba wakamkamate, mama anambiwa ana alfu kumi analiaaa yeye mamantilie faida alfu 4 hiyo hela apate wapi, mmoja anamjibu kamkamate utuletee kama huna hela.
Huu ni ujinga na upuuzi tutausambaza kila sehemu, hatuwezi kuwa na mapolisi wamejaa njaa hawangalii hata wa kupiga.