IGP: Tunawasaka watu wanaofurahia na kukebehi mitandaoni baada ya askari kuuawa

gillard

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
227
165
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amesema jeshi hilo linawasaka watu wanaofurahia mitandaoni na kukebehi baada ya askari wake kuuawa.

IGP ameyasema hayo wakati Miili ya Askari nane wa Jeshi la Polisi ikiagwa leo Mkoani Pwani.

IGP Mangu amesema, tulitumue tukio hili kama changamoto, ili tupeane nguvu badala ya kukatishana tamaa. Kuna watu wameanza kukejeli kwenye mitandao baada ya hili tukio kutokea, mheshimiwa Waziri nakuhakikishia tutawasaka hao wanaoendeleza kejeli badala ya kutupa pole wanakejeli na wengine wanafurahia.

Na mtu wa namna hii anefurahia si mwingine isipokuwa ni mhalifu kama huyu aliyefanya tukio hili baya, nao tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria tutakapowapata.

Ila tu niombe wananchi tutumie tukio hili kama changamoto na tutiane nguvu ili mwisho wa siku tuweze kushinda hii vita ya uhalifu kwa sababu hakuna mtu anayependa uhalifu na wote tunapenda amani.

Haya watanzania wa mitandao nadhani mmesikia wenyewe.
 
IGP Mangu kwanza pole kwa msiba mzito,lakini sijapenda kauli ya CP Marijani kuwa tukio hili ni la kawaida wakati Polisi wetu 8 wanauwawa Mara moja.

Kwa hao wanatoa maneno ya kejeli hao angaika nao tu lakini Mimi ujumbe wangu kwako IGP ni kutafuta root cause ya tatizo ili tusiendelee kupoteza vijana wetu wa Polisi kila siku.

Tumechoka na haya matamko ya kila siku toka kwenu kuwa sasa tutawaonyesha kazi,sijui dawa ya moto ni moto,haya matamko tumechoka nayo.

Hatuwezi Kila siku tunazika Polisi waliouwawa kazini nasema lazima vijana wetu hawa tuwalinde wafanye kazi kwa moyo mmoja kulinda RAIA na Mali zao.
 
Polisi wa nchi hii bwana..Sasa tukio limeshatokea, badala ya kwenda kuwasaka watu wenye silaha walio ua polisi wanataka kudeal na watu wenye mitandao ambao wengi wao hata hawajui bunduki inafananaje.Hakuna anaefurahia kupoteza roho ya mtu. Polisi wetu wajifunze kukabiliana na wahalifu wenye silaha na sio kutumika na wanasiasa because we dont know when they will strike next!
 
IGP Mangu kwanza pole kwa msiba mzito,lakini sijapenda kauli ya CP Marijani kuwa tukio hili ni la kawaida wakati Polisi wetu 8 wanauwawa Mara moja.

Kwa hao wanatoa maneno ya kejeli hao angaika nao tu lakini Mimi ujumbe wangu kwako IGP ni kutafuta root cause ya tatizo ili tusiendelee kupoteza vijana wetu wa Polisi kila siku.

Tumechoka na haya matamko ya kila siku toka kwenu kuwa sasa tutawaonyesha kazi,sijui dawa ya moto ni moto,haya matamko tumechoka nayo.

Hatuwezi Kila siku tunazika Polisi waliouwawa kazini nasema lazima vijana wetu hawa tuwalinde wafanye kazi kwa moyo mmoja kulinda RAIA na Mali zao.

Well said Mkuu! Ni vema tujikite kutafuta mzizi/mizizi ya haya matatizo ya kuuwawa kwa polisi wetu, inasikitisha sana! Nashawishika kusema kauli ya CP marijani inafanana na kauli zingine za kisiasa, tukianza kuyachukulia kwamba hayo ni matukio ya kawaida tu tujenge ujasiri gani mioyoni mwetu!! Kwa nn hayo matatizo ya kawaida ya kuuwa askari wetu yasitokee mahali pengine nchini yatokee Pwani tu? Pengine haukuwa wakati muafaka kutoa matamko badala yake upelelezi wa kina!! Mungu ibariki Tanzania!
 
Then hiyo kesi mtu akikamatwa nayo inakua ni cyber crime au hahahaha ebu tuwe serious kidogo yaani no zolizowasiliana na ben saa8 hazijiafatiliwa unaenda mfatilia mtu anaye bluff mtandaoni kuhusu polisi kuuawa
Whaat
 
Mkuranga kunahitaji usalama wa taifa wengi kule na tujue ni akina nani wanaua viongozi maana haiwezekani wauaji wanataja idadi ya kuwaua watu na wanaikamilisha lakini polisi unakuta wanaanza maneno mengi baada ya tukio. Nadhani kile kikosi cha utekaji(inavyosemekekana) kiende kule kikamate wauaji wote hapo tutajua kweli tuna kikosi imara na tutaacha kuwasema vibaya viongozi.
 
Yale yale badala ya kutafuta sababu au chanzo ya kwanini watu wanafurahi walinzi kufa, unaanza kuleta vitisho kwa wanaofurahi!

Angalia uhusiano wako na jirani zako upo namna gani kabla ya kulaumu kwamba napopatwa na tatizo wao wanashangilia.
 
Si vizuri kusherehekea mtu anapofikwa na msiba hata kama ni adui yako. Lakini IGP anaposema atawashughulikia kwa mujibu wa sheria, sheria ipi!? Mwisho wa siku atajikuta anakamata watu na kuwatesa bila kutatua tatizo lililopo.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amesema jeshi hilo linawasaka watu wanaofurahia mitandaoni na kukebehi baada ya askari wake kuuawa.

IGP ameyasema hayo wakati Miili ya Askari nane wa Jeshi la Polisi ikiagwa leo Mkoani Pwani.

IGP Mangu amesema, tulitumue tukio hili kama changamoto, ili tupeane nguvu badala ya kukatishana tamaa. Kuna watu wameanza kukejeli kwenye mitandao baada ya hili tukio kutokea, mheshimiwa Waziri nakuhakikishia tutawasaka hao wanaoendeleza kejeli badala ya kutupa pole wanakejeli na wengine wanafurahia.
Na mtu wa namna hii anefurahia si mwingine isipokuwa ni mhalifu kama huyu aliyefanya tukio hili baya, nao tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria tutakapowapata.
Ila tu niombe wananchi tutumie tukio hili kama changamoto na tutiane nguvu ili mwisho wa siku tuweze kushinda hii vita ya uhalifu kwa sababu hakuna mtu anayependa uhalifu na wote tunapenda amani.

Haya watanzania wa mitandao nadhani mmesikia wenyewe.

Acheni kusaka raia wasiokuwa na hatia.

Sakeni waharifu wakati huo huo mkiondoa uharifu katika jeshi lenu pia.

Hakuna mtu atafurahia kifo cha askari. Mnapoteza nguvu kwa kupiga vichaka mkiacha target.

Wekezeni katika kukomesha uahrifu ndani na nje ya jeshi l apolisi.
 
Polisi wa nchi bwana..Sasa tukio limeshatoke, badala ya kwenda kuwasaka watu wenye silaha walio ua polisi wanataka kudeal na watu wenye mitandao ambao wengi wao hata hawajui bunduki inafananaje.Hakuna anaefurahia kupoteza roho ya mtu, polisi wetu wajifunze kukabiliana na wahalifu wenye silaha na sio kutumika na wanasiasa because we dont know when they will strike next!
Polisi wetu wamezoea kazi za kujipendekeza Kama hizi za mtandaoni wanadhani hili jambo ni la Ccm. Shida niionayo mm polisi wetu HAWANA MAHUSIANO MAZURI NA RAIA. wakivaa sare zao wanajiona miungu watu na kuwaonea Raia, badala ya kuwasaidia. Kama huamini muulize Bodaboda ama dereva yeyote.
Yamekuwa hayo tenaa
 
Back
Top Bottom