Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tumemsikia IGP Sirro akijitetea kuhusu tuhuma zinazopewa Jeshi lake la Polisi kuhusu kuwakamata mfululizo wabunge wa chama cha Chadema kuwa ni uonevu. Akijibu tuhuma hiyo amejibu kuwa Jeshi lake la Polisi halina upendeleo na halifanyi uonevu bali linawakamata raia wote waliofanya makosa ya jinai bila kujali nyadhifa zao katika jamii na bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Kutokana na kujitetea kwake IGP wetu Sirro nami ningependa kumuuliza maswali yafuatayo:-
1. Jeshi lake limemkamata Tundu Lissu kutokana na Press conference aliyofanya na aliyoeleza kuwa Bombardier yetu imekamatwa nchini Canada kutokana na kudaiwa fidia na kampuni moja ya ujenzi ambayo ilivunjiwa mkataba wake wa ujenzi wa barabara hapa nchini miaka ya nyuma na aliyekuwa Waziri wa ujenzi wa wakati huo ambaye hivi sasa ni Rais wetu.
Katika Press conference iliyoitishwa baadaye na msemaji wa serikali Zamaradi Kawawa na akakiri kuwa kweli Bombardier yetu imezuiliwa huko Canada kutokana na kudaiwa fidia ya shilingi bilioni 87. Je kosa la Tundu Lissu lililosababisha kukamatwa kwake ni lipi iwapo serikali yenyewe imekiri kukamatwa kwa Bombardier yetu?
2. Tukio lingine ni la kukamatwa kwa Mbunge Esther Bulaya wa Bunda kwa kwenda kwenye Jimbo la Mbunge mwenzake wa Chadema John Heche wa Tarime na kushiriki harambee ya ujenzi wa shule ya Nyamongo, ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ni "makosa" kwa mbunge wa Jimbo lingine kwenda kwenye Jimbo lingine la mwenzake na kushiriki harambee kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo husika!
Sasa nimuulize IGP Sirro, mbona hujamkamata Mbunge Kingu wa CCM ambaye alifanya "the same thing" kwa kwenda kwenye Jimbo la Singida Mashariki la Tundu Lissu wa Chadema ba akaendesha harambee ya ujenzi wa shule?
Nimuukize swali jingine IGP Sirro, mbona Jeshi lake la Polisi halijamkamata Mbunge wa viti maalum wa CCM Tulia Ackson ambaye alienda Jimbo la Mbeya mjini la mbunge Sugu wa Chadema kwa kushiriki harambee ya ujenzi wa soko la Sido lililoungua hivi karibuni?
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu Jeshi la Polisi linapaswa liwe fair na kuwa neutral na lisijiegemeze kwenye chama chochote cha siasa.
Hata hivyo ni jambo lililo wazi kuwa Jeshi letu la Polisi limejiegemeza upande wa chama tawala katika utekelezaji wa majukumu yake na hilo jambo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kulikanusha.