IGP Sirro amvalisha cheo cha Kamishna wa Polisi CP Hamduni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,562
Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Sirro leo amemvalisha cheo cha Kamishna wa Polisi CP Hamduni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi kanda maalumu ya Dar es salaam.

CP Hamduni kwa sasa ndiye Mkurugenzi mkuu wa Takukuru.

1.jpg
2.jpg

Kazi Iendelee!
 
... kule Israel vyeo kama hivi ni lazima uwe umefanya a distinguished mission for the betterment of the Nation of God sijui huku kwetu kinaangaliwa nini. Natafakari sipati jibu.
 
Kha! Unaweza thibitisha hili!? Au ndio umeingia kwenye lile kundi la kusambaza habari zisizo na uhakika

.....niliandika uzi huuukafutwa....

MHESHIMIWA RAIS NA IGP;
MAMBO SASA ANA MCHANGO MKUBWA KATIKA UHALIFU UNAOENDELEA DSM;
Mh. Rais, jana ukiwa unahutubia wazee wa Dsm ulionyeshwa kuguswa na kukerwa na wimbi la uhalifu mkubwa unaoendelea Dsm hadi kufia kutoa tamko kali na kumwagiza IGP kuwa alisimamie jambo hili.
Naomba nikusaidie mahali pa kuanzia kushughulikia tatizo hili ukianza na kiongozi husika wa Kanda maalum.
1. Ni muda sasa huyu mkuu analea huu uhalifu kwa maslahi yake binafsi na nitayataja, hili wimbi la wizi wa vifaa vya magari na pikipiki halitakaa liishe kwani wahusika wakuu wa uhalifu huu wanalindwa na mkui huyu, lile zoezi la kamatakamata ni danganya toto, vifaa vinakusanywa kwa wahusika then wanaitwa waandishi wa habari kupiga picha na kuchukua habari lkn mwisho wa siku vinarudishwa kwa wahusika...ukienda muda huu utavikuta vichache mno vingine vimerudishwa.
Wahalifu hawa ndio wanaomjengea nyumba ya ghorofa pale Makongo na hoteli yake mpya.
Hivyo usitqrajie huu ihalifu kuisha leo.
2. Askari wanaotumika kukamata wahalifu mara wakamatapo wahalifu hupigiwa simu kuwaachia wahalifu hao, kitendo hiki kinawavunja moyo askari nao kwasasa wameamua kula sahani moja nao kuwa wakiwakamata wanamalizana nao kwa kupewa kitu kidogo.
3. Umiliki wa silaha kiholela bila kufuata utarqtibu.
Mheshimiwa, leo hii ukiitisha ukaguzi wa silaha kwa waliomilikishwa kuanzia 2020 na 2021 hasa watu asili ya Asia karibu 99% wote hawajafuata utaratibu, hupitia kwa MKUU na mkuu hutuma vi MEMO kwa ma OCD kuwa wapitishiwe maombi yao bila kujadiliwa na kamati za usalama kama ilivyo utaratibu, hili liko wazi ni kufanya utafiti mdogo sana utagundua kuwa utaratibu haufuatwi, hili litatuletea matizo huko mbeleni au tayari limeanza kuleta madhara kwa watu wasio na sifa kumilikishwa ailaha kiholela kwa maslahi ya mtu mmoja.
4. Ma RPC wa Mikoa ya kipolisi Ilala, Kinondoni na Temeke wamepokwa majukumu yao, MKUU huu ana watu wake binafsi wa kiupelelezi na wanaingilia majukumu ya RPC wakinyanyua midomo wanatukanwa na kudhalilishwa nao, hili linashusha ari ya utendaji, IGP fuatilia itapata taarifa za ajabu kuhusu hili, aiwezi kuandika kila kitu najua wewe ni mtendaji makini.
5. Tatizo lingine kubwa huyu MKUU akotofautiana kidogo na kiongozi wa kimkoa mara moja anamhamisha mfano mzuri ni RPC Bkombe wa kinondoni aliyemhamisha kwa kutofautia kauli tu, na kwa vile rank yao ni moja alimwona ni tishio kwa kazi yake.

USHAURI
Nashauri kanda maalum na ivunjwe kwani hawana kazi zaidi ya wengi wao kurandaranda mjini na kujihusisha na wahalifu na kuingiliwa majukumu ya kimikoa na ibaki mikoa ya kipolisi Ilala, Temeke na Kinondoni.
Mtafutie kazi nyingine Mambosasa na ndani ya mwezi Dar itatulia na hutasikia uhalifu.
Ukiaangalia hata body language ya Mambosasa wakati akiongelea uhalifu utajifunza kitu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom