IGP Simon Sirro aibukia Moshi mauaji ya Kibiti

IGP Simon Sirro aibukia Moshi mauaji ya Kibiti

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema mauaji ya polisi, viongozi na raia katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Ikwiriri ni ya muda na kusisitiza majibu yake yako mbioni kupatikana.

Sirro ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi) katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wakati wa kufunga mafunzo ya upandishaji vyeo kwa maofisa na askari 222 wa Jeshi la Uhamiaji nchini.

Kauli ya Sirro imekuja huku kukiwa na mfululizo wa mauaji ya polisi na raia katika maeneo hayo ambapo zaidi ya watu 35 wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwamo polisi 13.

Hadi sasa, licha ya polisi kufanya operesheni kubwa katika maeneo hayo, bado halijaweza kubaini chanzo cha mauaji hayo na kwa nini wanawalenga polisi na baadhi ya watu na nani wanayatekeleza.

Tukio la hivi karibuni kabisa lililotokea Jumatano iliyopita, ambapo watu wasiojulikana waliwashambulia kwa risasi na kuwaua polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani huko Kibiti.

Akizungumza katika sherehe za kuhitimu mafunzo kwa maofisa na askari hao 222 wa Jeshi la Uhamiaji, Sirro amesema japokuwa nchi ni salama, lakini inakabiliwa na kitisho cha usalama eneo hilo.

“Tuna shida Kibiti Ikwiriri lakini wanasema sisi ni wengi wao ni wachache. Tusikubali hata siku moja makabila yetu, madhehebu yetu, majimbo yetu yatugawanyishe,” amesema Sirro na kuongeza;-.

“Umoja wetu ndio nguvu yetu. Suala la Kibiti ni la muda mfupi. Tunakwenda na tutapata majibu. Hatutakubali kikundi cha watu wachache wafanye Kibiti, Ikwiriri, Rufiji yasikalike,”.

Akizungumzia changamoto zinazolikabili Jeshi la Uhamiaji, Sirro aliyekuwa mgeni rasmi amesema moja ya changamoto kubwa ni uingiaji wa wahamiaji haramu wanaopitia njia zisizo rasmi kuingia nchini.

“Hili litawezekana kwa kuimarisha intelijensia. Mnapopanda vyeo sio mfurahie tu kupanda cheo mjue majukumu yanaongezeka pia. Idadi ya mnaoenda kuwaongoza sasa itaongezeka,”amesema Sirro.

“Kazi yenu Uhamiaji na sisi polisi hazitofautiani sana na mara nyingi tumekuwa tukifanya kazi za operesheni pamoja. Changamoto tunayokutana nayo ni usimamizi wa kazi”alisisitiza na kuongeza;-

“Askari anakosea huchukui hatua. Konstebo anafikia mahali anamtuma Koplo amletee soda na anakimbia anakwenda kumletea soda. Mnaona ni sawa hii?”alihoji na kujibiwa “Hapana”.

“Heshima yetu sisi askari ni kutokuwa waoga na unakuwa sio muoga kwa sababu kazi unaifahamu, unakuwa sio muoga kwa sababu unatii sheria na unasimamia sheria na hubabaiki,”amesema.

“Ninawaelekeza suala la uoga, suala la ulegelege katika awamu hii tusiipe nafasi,”ameongeza kusema na kusisitiza maofisa hao kufanya kazi kwa weledi pasipo kuwasumbua au kuwazungusha wananchi.

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mafunzo hayo ni ya kwanza katika historia ya jeshi lake baada ya Jeshi hilo kufanya maboresho ya kimuundo na sheria.

“Jeshi la Uhamiaji limefanya maboresho yakiwamo ya kimuundo na sheria ili kuliingiza Jeshi la Uhamiaji katika tume ya polisi na Magereza. Hatua hii imechangia kuwepo kwa mabadiliko,”amesema.

“Uhamiaji lina askari na watumishi wasiozidi 3,000, hawatoshi kutokana na ongezeko la majukumu ya uhamiaji. Ili kufanya kazi kwa ufanisi linalihitaji kuwa na askari wasiopungua 10,000,”amesisitiza.

Kamishina Jenerali hiyo amesema Taifa kwa sasa linakabiliwa na changamoto ya wahamiaji haramu wanaoingia kupitia njia zisizo rasmi, lakini akasema wanapata ushirikiano mkubwa toka polisi.
 
Chanzo cha mauaji hayo ni nini?
 
Rais akiwa Mkoa Wa Pwani wiki iliyopita alisema Wauaji wa Kibiti wameshaanza kuisoma namba na wanahenyeshwa tayari lakin Mkuu wa Jeshi la Polisi anasema Mauaji ni ya Muda tu na dawa Yao inachemka hii inaashiria kuna Mmoja Kati ya IGP au Rais katudanganya!

Inawezekana wanaofanya Mauaji Kibiti sio wakaazi wa Kibiti Bali huwa wanaenda pale kufanya Mauaji na kurudi Kwmy Maeneo Yao ya kuishi!
Nakumbuka wa Marekani walishusha Makombora na mabomu Mengi sana Afghanistan kumsaka Osamah wakidhan yupo Mapangoni Kumbe Mwenzao alikuwa zake Abbotabad Pakistan kwny Makazi ya kawaida, walipoacha kukurupuka wamarekani na kuwekeza kwny Intelijensia for 10 years ndipo walipomnasa na kumuua!

Vyombo vya Dola na Wanasiasa wanajaribu ku under estimate nguvu ya Adui na hili ni kosa kubwa sana, hii ni vita ya Muda mrefu nao wanapaswa kufahamu na kujipanga hivyo, kusema ni vya Muda mfupi ni kujihadaa
 
Hivi uhamiaji si ina mkuu wao, Sirro ni nani ndani ya idara ya uhamiaji? Kama uhamiaji ipo chini ya polisi basi imejulikana kwa nini idara hiyo inafanya kazi chini ya kiwango.
 
Hivi uhamiaji si ina mkuu wao, Sirro ni nani ndani ya idara ya uhamiaji? Kama uhamiaji ipo chini ya polisi basi imejulikana kwa nini idara hiyo inafanya kazi chini ya kiwango.
Ndani ya Jeshi la Polisi Kuna idara tofauti,Uhamiaji,FFU,CID,Ufundi,Cyber crime, Communication,HR,Utawala n.k
 
Ndani ya Jeshi la Polisi Kuna idara tofauti,Uhamiaji,FFU,CID,Ufundi,Cyber crime, Communication,HR,Utawala n.k

Acha Uongo, uhamiaji si Idara ya Jeshi la Polisi

Uhamiaji Kama Polisi ni Idara zinazojitegemea na zipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 
Siro ana busara sana.. Fuatilia maongezi yake uone anavyo ongea na watu bila kujali cheo chake
 
Back
Top Bottom