IGP MANGU, Jeshi la Polisi limekushinda; ulinzi mchana, usiku je?

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,763
7,753
Hali inayoendelea katika jeshi la polisi inasikitisha, wanainchi hawapati huduma kama inavyotakiwa polisi ni walinzi wa wanainchi lakini cha kusikitisha kwa sasa ukienda kituo chochote cha polis kuanzia saa 12jioni hauruhusiwi kufika unatishwa unafukuzwa, na matusi mengi hata kupigwa hata mchana wanajizungushia (warning tape dont cross).

Uzio wa hali ya hatari imefikia hatua mwanainchi wa kawaida huwezi fika unaogopa hata ukipita na gari karibu na kituo cha polis una pata usumbufu mkubwa.

Binafsi yamenikuta nikipita katika kituo cha polis mkuranga ambapo niliamuliwa kushuka katika gari na kulukishwa kichura jioni ya saa 1 ni udhalilishaji mkubwa tunaofanyiwa sehemu nyingi za vituo vya polis raia.

Rai yangu polisi kamwe hamutafanikiwa kwa kuweka uadui na raia jalibu kujenga mazingira rafiki na wanainchi wa kawaida.

Tupo katika Dunia 4G tafuta jinsi ya kulinda na kufanya interejensia yenu kwa mambo yanayoendana na wakati wa kisasa SIYO KUJIZUNGUSHIA UZIO NA KUTISHA WATU mimi si mtaalamu wa ulinzi ila Dunia ya leo hamtafanikiwa kwa kufunga vituo na kujificha ndani.

IGP MANGU CHUKUA HATUA HALI NI MBAYA SANA KATIKA VITUO VYA POLISI TAFUTA NJIA MBADALA YA ULINZI.
 
Last edited by a moderator:
Kamshitaki mahakamani kwa kushindwa kuhudumia wananchi kwa kodi zao ndio mlo wake humu hutopata msaada pole sana
 
Jeshi letu la Polisi limejikita zaidi kutumia nguvu na kudhibiti vitendo vya raia wasiokuwa na hatia wala silaha kuliko wale wahalifu wenye silaha . kwa mfano,
linapokuja suali la kuzuia mikutano ,maandamano ama shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani basi jeshi letu huwa ni namba one kwa jambo hilo. Polisi hutumia nguvu kupita kiasi pamoja na silaha za moto kwa mtu asiekuwa hata na jiwe mkononi! kisa yeye ni mpinzani na ambae kuandamani ni haki yake kikatiba! Mfano mwengine ni kwamba Katika uchaguzi wa 2015 pekee basi kumenunuliwa gari za washa washa 700 kwa polisi kwa ajili ya kudhibiti upinzani tu!Ona nguvu ya polisi ilotumika kuzuia mazishi ya mwanaharakati Alphonce mawazo kule Mwanza na Geita. Hali hii imewafanya hadi wale polisi wetu kuamini ya kwamba Mpinzani wa CCM ni mhalifu namba moja kuliko jangili ama jambazi ambae anahatarisha maisha ya wananchi! Umefika wakati kwa jeshi letu la polisi kubadilika sasa. Yaani kwa jeshi hili la polisi basi ni bora kuwa na mbwa atakulinda vyema wewe na mali yako kuliko polisi wetu.
 
Last edited:
Mkuu vituo vya Polisi vilikuwa wazi 24x7,kilicho badirisha mfumo nzima siku za karibuni kilitokana na uvamizi wa magaidi walio uua Polisi,Raia na kuiba silaha katika kituo cha SITAKISHARI, mkuu kumbuka Polisi nao ni binadamu,sasa unafikiri baada ya tukio hilo la kigaidi vituo vya Polisi vingebaki na mfumo wao wa hawali? Jibu ni hapana.
 
Mkuu nakubaliana nawe kuwa Polisi nao ni binadamu, bali kila mtu anautaalamu wake katika fani husika. Sasa tuseme wananchi wanalindwa mchana tu na usiku ni kila mtu kivyake? Kiukweli ni ushauri tu watumie mbinu nyingine za kiintelijensia kubaini matatizo. Kwa sasa ikifika usiku hata kama upo karibu na kituo cha polisi ukivamiwa hakuna msaada wowote maana kituo kimefungwa mpaka kesho.
 
Hapo umenena!!!
 
Mkuu ulikuwa unamaanisha vituo vidogo kwenye kata, mambo yalivyo siku hizi labda Polisi wa vituo vidogo wapewe SSB radio na marungu, kwa usalama wao wasipewe silaha za moto, majambazi siku hizi wana ujasiri wa ajabu wanaweza kuvamia Polisi kwa lengo la kuwanyanganya silaha za moto.
 
Adui mkubwa wa amani,uhuru na umoja wa wananchi katika nchi maskini ni Wanasiasa.
Hawa ni zaidi ya magaidi na majambazi.
Wanasiasa wa nchi za kiafrika ni wahalifu wakubwa sana.
Hawa wanasaka maisha kwa faida zao na familia zao kwa migongo ya vyama vya vya siasa. Ndio maana hawaaminiani hata kidogo. Kila mwanasiasa anajua dhamira aliyonayo ni mbaya kwa mustakabali wa maisha ya wananchi ndio maana hataki kuona mwenzake anaingia madarakani na yeye akakaa pembeni.
Kwa mwanasiasa wa Afrika kukaa pembeni na kuachia madaraka ni bora taifa liangamie wote wakose.
Tumeona kule Zanzibar watu wanaofanya kazi pamoja kama rais na makamu wake kwa miaka mitano lakini leo hii Dr. Shein hataki kumwachia mzanzibar mwenzake na Muislam Mwenzake madaraka. CCM inatumia uovu kumlinda mtu mmoja na kukosa mabilioni ya MCC kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wasio na dawa hospitalini. Hawa ndio maadui wa wananchi na sio polisi wala majambazi wala magaidi. Walionunua magari ya washawasha mia saba ni serikali ya CCM kama zilivyo serikali adui wa wananchi zilizotapakaa barani Afrika sio polisi walionunua magari hayo.
Askari Polisi aache kunua gari yake anunue gari za washawasha kwani anagombea nini wakati tayaria ana ajira. Wanasiasa ndio tatizo kwani pamoja na madaraka lakini tukumbuke kuwa huko wanajipatia mahela mengi na mishahara mikubwa kwa hiyo mara nyingi wanaweza kuwa wahalifu wakubwa almradi tu wabakie madarakani au waingie madarakani na kuendelea kupata madaraka yao na mishahara yao minono.
Ndio maana wanamuogopa maalim Seif sio kwa sababu yoyote bali kulinda siri za wizi wao kwenye baraza la mawaziri. Mwenye akili atajua kua hakuna nia ya uadilifu kwenye serikali ya CCM na Magufuli ndio maana hawataki mtu atakayehoji na kupinga wizi na ufisadi unaofanywa na mawaziri kama alivyokuwa ameeleza marehemu Deo Filikunjombe kuwa mawaziri ndio wanaotafuna nchi hii.

Kwa hiyo tukitaka jeshi zuri la polisi ni lazima tuwe na wanasiasa wazuri na wanaopata madaraka kwa halali. Lakini hawa wanasiasa waliopo ktk nchi nyingi za kiafrika ni maadui wa amani na waroho wa madaraka tuu. Mfano Zanzibar. Shein na CCM yake ndiye anayen'gang'ania madaraka na sio Polisi at the end atalazimisha kubaki madarakani na kuamuru polisi kulinda uharamia wake. Kulingana na sheria polisi sio wanasiasa kwa hiyo itabidi wamlinde yeyote atakayeapishwa kama moja ya kazi zao za msingi.

Hilo la kurushwa kichura usiku sio sawa lakini mara nyingine kulingana na hali tete kwenye baadhi ya maeneo sioni tatizo. Kwani wahalifu wamekua wakiwavamia na kuwaua polisi kwa lengo la kupora silaha. Kama wamezungusha utepe nadhani hakuna haja ya kulazimisha kupita.
Kulazimisha itakua ni kosa.
Na ukumbuke tu kuwa Polisi na sera za polisi wa kitanzania ni kuwa lipo na linatamnulika kama Jeshi sio watoa huduma tu kama walivyo manesi na watumishi wengine hivyo panapohitajika kutumia mbinu na harassment za kijeshi watazitumia tu mana ndivyo ilivyo.
Na hilo suala la kurusha watu kichura halipo maeneo yote kwa hiyo kumlaumu IGP Mangu sio sahihi.
Ni vyema ukamlaumu mkuu wa hicho kituo au RPC wake.
 
Last edited:
Vituo vyote vya polisi vifungwe cc camera,mashtaka yaanze kurekodiwa kwenye kompyuta watoke kwenye vikaratasi, polisi wa barabarani wavae kamera ili kudhibiti mapato,marekani polisi wa kawaida wanavaa vijikamera sisi tunaweza kuanza na hawa wanaokula rushwa zaidi. Adhabu kali zitolewe kwa polisi walev tumeona walev wanapewa lindo hasa vijijini nk. Yote kwa yote jeshi lijifunze mambo mapya ya kidijitali wasizidiwe na wahalifu amba kila kukicha wanabuni mbinu
 
Mkuu wa jeshi la polic akishushwa cheo anahamia upinzan,hapo habadilishw mpaka astaafu.Kiukwel jeshi la police limekosa uelekeo.Tena hapo mkuranga ni jibu.
 
Mkuu vituo vya Polisi vilikuwa wazi 24x7,kilicho badirisha mfumo nzima siku za karibuni kilitokana na uvamizi wa magaidi walio uua Polisi,Raia na kuiba silaha katika kituo cha SITAKISHARI, mkuu kumbuka Polisi nao ni binadamu,sasa unafikiri baada ya tukio hilo la kigaidi vituo vya Polisi vingebaki na mfumo wao wa hawali? Jibu ni hapana.
Kwahiyo hawana njia mbadala? Kazi ya polis ni kulinda RAIA na Mali zao.
 
Wakuu wa usalama sio wabunifu.nikweli kabisa kulikimbia tatizo sio suluhisho dawa ni kutafuta njia ya kupambana nalo na kulishinda.
 
Vituo vyote vya polisi vifungwe cc camera,mashtaka yaanze kurekodiwa kwenye kompyuta watoke kwenye vikaratasi, polisi wa barabarani wavae kamera ili kudhibiti mapato,marekani polisi wa kawaida wanavaa vijikamera sisi tunaweza kuanza na hawa wanaokula rushwa zaidi. Adhabu kali zitolewe kwa polisi walev tumeona walev wanapewa lindo hasa vijijini nk. Yote kwa yote jeshi lijifunze mambo mapya ya kidijitali wasizidiwe na wahalifu amba kila kukicha wanabuni mbinu
Adui mkubwa wa amani,uhuru na umoja wa wananchi katika nchi maskini ni Wanasiasa.
Hawa ni zaidi ya magaidi na majambazi.
Wanasiasa wa nchi za kiafrika ni wahalifu wakubwa sana.
Hawa wanasaka maisha kwa faida zao na familia zao kwa migongo ya vyama vya vya siasa. Ndio maana hawaaminiani hata kidogo. Kila mwanasiasa anajua dhamira aliyonayo ni mbaya kwa mustakabali wa maisha ya wananchi ndio maana hataki kuona mwenzake anaingia madarakani na yeye akakaa pembeni.
Kwa mwanasiasa wa Afrika kukaa pembeni na kuachia madaraka ni bora taifa liangamie wote wakose.
Tumeona kule Zanzibar watu wanaofanya kazi pamoja kama rais na makamu wake kwa miaka mitano lakini leo hii Dr. Shein hataki kumwachia mzanzibar mwenzake na Muislam Mwenzake madaraka. CCM inatumia uovu kumlinda mtu mmoja na kukosa mabilioni ya MCC kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wasio na dawa hospitalini. Hawa ndio maadui wa wananchi na sio polisi wala majambazi wala magaidi. Walionunua magari ya washawasha mia saba ni serikali ya CCM kama zilivyo serikali adui wa wananchi zilizotapakaa barani Afrika sio polisi walionunua magari hayo.
Askari Polisi aache kunua gari yake anunue gari za washawasha kwani anagombea nini wakati tayaria ana ajira. Wanasiasa ndio tatizo kwani pamoja na madaraka lakini tukumbuke kuwa huko wanajipatia mahela mengi na mishahara mikubwa kwa hiyo mara nyingi wanaweza kuwa wahalifu wakubwa almradi tu wabakie madarakani au waingie madarakani na kuendelea kupata madaraka yao na mishahara yao minono.
Ndio maana wanamuogopa maalim Seif sio kwa sababu yoyote bali kulinda siri za wizi wao kwenye baraza la mawaziri. Mwenye akili atajua kua hakuna nia ya uadilifu kwenye serikali ya CCM na Magufuli ndio maana hawataki mtu atakayehoji na kupinga wizi na ufisadi unaofanywa na mawaziri kama alivyokuwa ameeleza marehemu Deo Filikunjombe kuwa mawaziri ndio wanaotafuna nchi hii.

Kwa hiyo tukitaka jeshi zuri la polisi ni lazima tuwe na wanasiasa wazuri na wanaopata madaraka kwa halali. Lakini hawa wanasiasa waliopo ktk nchi nyingi za kiafrika ni maadui wa amani na waroho wa madaraka tuu. Mfano Zanzibar. Shein na CCM yake ndiye anayen'gang'ania madaraka na sio Polisi at the end atalazimisha kubaki madarakani na kuamuru polisi kulinda uharamia wake. Kulingana na sheria polisi sio wanasiasa kwa hiyo itabidi wamlinde yeyote atakayeapishwa kama moja ya kazi zao za msingi.

Hilo la kurushwa kichura usiku sio sawa lakini mara nyingine kulingana na hali tete kwenye baadhi ya maeneo sioni tatizo. Kwani wahalifu wamekua wakiwavamia na kuwaua polisi kwa lengo la kupora silaha. Kama wamezungusha utepe nadhani hakuna haja ya kulazimisha kupita.
Kulazimisha itakua ni kosa.
Na ukumbuke tu kuwa Polisi na sera za polisi wa kitanzania ni kuwa lipo na linatamnulika kama Jeshi sio watoa huduma tu kama walivyo manesi na watumishi wengine hivyo panapohitajika kutumia mbinu na harassment za kijeshi watazitumia tu mana ndivyo ilivyo.
Na hilo suala la kurusha watu kichura halipo maeneo yote kwa hiyo kumlaumu IGP Mangu sio sahihi.
Ni vyema ukamlaumu mkuu wa hicho kituo au RPC wake.
GT umechambua vizuri sana. Siasa ni maisha. Siasa nzuri maisha mazuri. Angalia tu siasa na sera mbaya za bushi na Blair zilivyoitumbukiza dunia kwenye lindi la umwagikaji damu
 
Vituo vyote vya polisi vifungwe cc camera,mashtaka yaanze kurekodiwa kwenye kompyuta watoke kwenye vikaratasi, polisi wa barabarani wavae kamera ili kudhibiti mapato,marekani polisi wa kawaida wanavaa vijikamera sisi tunaweza kuanza na hawa wanaokula rushwa zaidi. Adhabu kali zitolewe kwa polisi walev tumeona walev wanapewa lindo hasa vijijini nk. Yote kwa yote jeshi lijifunze mambo mapya ya kidijitali wasizidiwe na wahalifu amba kila kukicha wanabuni mbinu
hizo cctv zitadumu? Watazinyofoa tu kuiba na kwenda kuuza. Mali za umma bongo kamwe haziwez kuwa salama CHINI YA CCM
 
Wakifanya kazi yao kikamilifu tunalalamika wakilegeza tunawaambia hawafanyi kazi kwa nn polisi polisi tu jaman
 
hadi urushwe kichura ina mana wewe ni mhalifu na kuna kitu cha tofauti cha kijinga umefanya. hongera sana MANGU KWA KUWAFINYA WAHALIFU HAWA
 
Hali inayoendelea katika jeshi la polisi inasikitisha, wanainchi hawapati huduma kama inavyotakiwa polisi ni walinzi wa wanainchi lakini cha kusikitisha kwa sasa ukienda kituo chochote cha polis kuanzia saa 12jioni hauruhusiwi kufika unatishwa unafukuzwa, na matusi mengi hata kupigwa hata mchana wanajizungushia (warning tape dont cross) uzio wa hali ya hatari imefikia hatua mwanainchi wa kawaida huwezi fika unaogopa hata ukipita na gari karibu na kituo cha polis una pata usumbufu mkubwa.
Binafsi yamenikuta nikipita katika kituo cha polis mkuranga ambapo niliamuliwa kushuka katika gari na kulukishwa kichura jioni ya saa 1 ni udhalilishaji mkubwa tunaofanyiwa sehemu nyingi za vituo vya polis raia.
Rai yangu polisi kamwe hamutafanikiwa kwa kuweka uadui na raia jalibu kujenga mazingira rafiki na wanainchi wa kawaida.
Tupo katika Dunia 4G tafuta jinsi ya kulinda na kufanya interejensia yenu kwa mambo yanayoendana na wakati wa kisasa SIYO KUJIZUNGUSHIA UZIO NA KUTISHA WATU mimi si mtaalamu wa ulinzi ila Dunia ya leo hamtafanikiwa kwa kufunga vituo na kujificha ndani. IGP MANGU CHUKUA HATUA HALI NI MBAYA SANA KATIKA VITUO VYA POLISI TAFUTA NJIA MBADALA YA ULINZI.
Huo ukaribu na raia ndio uliowaletea uvamizi wa vituo hata huko Mkuranga.
 
Back
Top Bottom