Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 305
Ndugu wanajamvi,
Najaribu kuangalia na kulinganisha utendaji kazi wa vyombo hivi vitatu muhimu vya serikali.
Jana tumemsikia IGP Mangu akikiri kuwa ni kweli kuna baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wameripotiwa kufanya uhakiki wa vitambulisho kwa askari wake kujua iwapo wamejiandikisha ama la.
Ni jambo zuri lakini sielewi kama IGP hajui kuwa jukumu la kuhakiki majina ya wapiga kura ni la Tume ya Uchaguzi (NEC).
Pamoja na Mangu kukiri sijasikia akiwakemea maofisa wanaofanya hivyo kama alivyofanya Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubiga kwa tuhuma kama hizo namnukuu, "Jeshi la Wananchi halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo maana tunaamini kazi hiyo ni ya Tume ya Uchaguzi".
Nilitegemea pia NEC itoe tamko kuhusu kitendo hicho cha jeshi la polisi lakini hadi sasa iko kimya huku ikijua kuna baadhi ya vyombo vinakiuka sheria za tume hiyo.
Hivi Chama cha waalimu (CWT), TUKTA, chama cha madaktari navyo vikiamua kuhakiki wanachama wao kama wamejiandikisha NEC watakaa kimya?
Angalizo, vurugu baadae vita ndani ya nchi mara nyingi husababishwa na vyombo vitatu yaani Jeshi la polisi, Jeshi la Wananchi na Tume ya Uchaguzi.
Ni matumaini yangu jeshi la polisi litajifunza weledi kutoka kwa wenzao wa JWTZ.