Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
Wakuu,
IGP Simon Siro ameahidi kulipatia Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Magari mawili kukabiliana na uhaba wa magari. Magari hayo ni sehemu ya magari 50 yaliyokutwa bandarini DSM kufuatia ziara ya Rais MAgufuli bandarini hapo hivi karibuni.
Ahsanteni.
=========
Baada ya ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Rais John Magufuli bandarini na kukagua magari ya polisi ambayo yaliingizwa nchini mwaka 2015, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema kwamba magari mawili atayapeleka mkoani Pwani.
Ziara hiyo ya rais ilibaini uwapo wa magari zaidi ya 50 yakiwa bado yanaendelea kubaki eneo la bandari.
Rais alimwagiza IGP kuhakikisha anayakagua magari hayo na kuyatoa bandarini ili yakafanye kazi iliyokusudiwa.
“Kwa nini magari yanakuja hapa yanakaa miaka 10, wakati sheria inasema ni siku 21? alihoji Rais Magufuli.
Akiwa Kibaha jana, IGP Sirro alisema anatarajia kutoa magari mawili ya polisi Mkoa wa Pwani ili kupunguza changamoto ya uhaba wa vyombo vya usafiri kwa askari.
“Hayo magari ni ya Jeshi la Polisi na mawili kati ya hayo natarajia kuwapa polisi Mkoa wa Pwani,” alifafanua alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.
Sirro alisema kuimarika kwa hali ya usalama kwenye maeneo ya Kibiti, Ikwiriri na Rufiji kumetokana na ushirikiano uliofanyika baina ya jeshi hilo na wananchi wenye nia njema.
“Silaha zote ambazo wahalifu walikuwa wamezipora kwenye matukio mbalimbali wakati hali ikiwa mbaya kule Kibiti, tayari tumeshazipata zote na hali imeshaimarika vizuri hivyo napenda kuwaambia wananchi wote hivi sasa hali ni nzuri,” alisema.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo aliishukuru Serikali kwa kuanzisha Mkoa wa kipolisi Rufiji akisema hali hiyo imesaidia kuimarisha usalama ndani ya Mkoa wa Pwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna alisema ziara hiyo imeamsha ari ya utendaji kazi kwa askari wake na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa kwake.
Chanzo: Mwananchi