Igizo la lockdown: CHADEMA inacheza kamari

watz wa mitandaoni ni mazuzu sana kuliko wale wa vijiweni leo nimeprove
 
Dalili za kifo cha CDM, kurusharusha miguu! CDM imekosa kingozi mwenye maono
MANENO KAMA HAYO ALIANZA KUYASEMA STEVEN WASSIRA KUWA CHADEMA ITAKUFA KABLA YA 2015, AJABU YEYE NDUYE KAFA KISIASA
 
Hawa wazee wa kijijini machame wana akili kuliko genge lote la wabunge wa chadema waliojiweka lockdown.Wana argument za nguvu kuliko kamati kuu ya chadema inayopenda lockdown na wanaielewa loockdown kuliko mbowe na genge lake

Kweli wazee au au vijana ni shida tu iliysababishwa na CCM over 60 years now!
 
Hakuna karantini isiyoambatana na vipimo. Ndiyo sababu MwanaFA kwa mfano ilimchukua mpaka siku 28 kutoka. Mpaka pale kipimo cha mwisho kilipoonesha negative. Mtoto wa Mbowe pia jana tumeambiwa imemchukua siku 57 kujiridhisha yuko sawa. Hivyo utetezi huo haujakamilika mbele ya watu makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo sasa, lockdown yao ni ya uongo
 
Mbowe ni muhuni tu kama wahuni wengine. Binafsi nimeelewa Mbowe anatumia Cha Arusha ndiyo maana akili yake haipo sawa sawa.

Nawaambia kweli chadema Kama watapata hata viti vitano vya ubunge washukuru Mungu sana, wanamaamuzi ya kihayawani sana.

Wamekimbia kipindi muhimu na kwenye mijadala muhimu kwa taifa then wanajirudisha wakati mambo yamekwisha.

Mliowafukuza kwasababu hawakutii agizo la bwana wenu mbowe mmewaonea narudia tena mmewaonea kuthibitisha hili subiri adhabu yenu kutoka kwa wapiga kura wenu. Mnyika kibamba hatukutaki tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
We kura yako ni moja tu so haitishi hata kidogo labda mngekuwa kama laki mbili hivi angalau
 
Mods tafadhalini sana,ningependa kuwe na uzi "sticky" unaohusu maana au tafasiri ya maneno mbalimbali yanayotokea kulingana na matukio au nyakati. Uwe kama kamusi au "JFpedia" hivi,maana kuna tatizo kubwa sana la wanaJF wengi kutokuelewa au kupotosha maana ya misemo,maneno na tafsiri mbali mbali.
Kwa mfano,kuna tofauti kati ya "lockdown" na "quarantine",lakini kuna watu wanang'ang'ana kuonyesha kuwa vyote ni kitu kimoja.
Mods nitashukuru mkizingatia hili.
 
Takriban wiki mbili zilizopia mwenyekiti wa Chadema Mbowe aliamuru wabunge wa chama chake kuanza lockdown mara moja pale Dodoma na kwamba wasiende majimboni kabla siku 14 hazijaisha ili wasije kupeleka maambukizi majimboni kwao!

Kulikuwa na namna mbili za kuitafsiri hatua hii. Mosi, upinzani kuna kiongozi shupavu asiyetetereka kimaamuzi. Pili, kwamba hiyo ilikuwa kiki tu ya kutafuta airtime na umaarufu hasa kwa mwenyekiti.

Binafsi naiamini zaidi hoja ya pili (kiki) kwani ndani ya wiki moja tu baadhi ya wabunge hao walionekana wakizurura Dar na siyo karantini Dodoma! Mbunge wangu Sugu alipost mpaka picha akijinasibu kuwa yuko Dar anapiga supu ya pweza!

Leo tunaambiwa wamemaliza lockdown na wako tayari kurejea bungeni. Swali, kuna lockdown isiyoambatana na vipimo? Na je, kujiweka karantini na kisha kurudi kujichanganya na waliokuwa kwenye eneo lenye taarifa za maambukizi kama alivyosema katibu wao Mnyika leo, ni kujali afya zao?

Tatizo la kiki ni kuwa isipokuinua itakushusha. Kiki hii tayari imewagharimu chadema majimbo (wabunge) kadhaa. Pia waliotii amri ya mwenyekiti ni 15 tu! Hivyo takribani idadi kama hiyo au zaidi ilikaidi agizo hilo. Hii bila shaka inadhoofisha chadema kuliko kuiimarisha.

Kwa mtazamo wangu, kuelekea uchaguzi mkuu chadema inacheza kamari nyingi na haina muda wa kutafakari karata ipi itupwe na ipi ibaki mkononi. Mambo yatakayotokea mpaka Oktoba ni mengi hivyo Chadema wawe na utashi wa kuangalia lipi la kudandia na lipi la kuacha lipite.

Mathalani. Hivi karibuni vyama vyetu vikubwa zaidi ccm na chadema vyote vimepata kada walau mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za jinai/uhujumu uchumi. Wakati ccm wao wamejitenga na mtuhumiwa wao (silaha & ujangili) kama katiba yao inavyowaagiza chadema wao viongozi wao wako bize mitandaoni (twitter) kujieleza kwa niaba ya mtuhumiwa (mdude), impliedly wakikihusisha chama na tuhuma hizo.

Nawashauri chadema kuachana na kamari hizi na badala yake kujikita na maandalizi ya uchaguzi. Mfano, ccm wao wameanza kujiandalia media platforms kwa kutwaa channel 10 na magic fm. Chadema wana nini? Vipi corona ikiendelea na kampeni zikafanywa kwenye media! Wataitegemea TBC kisha waje kulia nayo baadaye? Huu ni mfano tu wa masuala ya muhimu kuhangaika nayo badala ya kutafuta ligi za kitoto na spika.
Hawatakuelewa wanasaccos subiri mapovu ya OMO!
 
Mimi hudhani kuwa ni rahisi zaidi upinzani kushinda kwenye jimbo ambalo mbunge anayemaliza muda wake ni wa kwao. Bali kutengeneza ombwe na kuacha jimbo kuwa "huru" ni kuisaidia ccm. Sitashangaa ccm wakiwaconvert hao "expendables" wa chadema kuwa wagombea wao.

Sent using Jamii Forums mobile app

sahihi kabisa
 
Takriban wiki mbili zilizopia mwenyekiti wa Chadema Mbowe aliamuru wabunge wa chama chake kuanza lockdown mara moja pale Dodoma na kwamba wasiende majimboni kabla siku 14 hazijaisha ili wasije kupeleka maambukizi majimboni kwao!

Kulikuwa na namna mbili za kuitafsiri hatua hii. Mosi, upinzani kuna kiongozi shupavu asiyetetereka kimaamuzi. Pili, kwamba hiyo ilikuwa kiki tu ya kutafuta airtime na umaarufu hasa kwa mwenyekiti.

Binafsi naiamini zaidi hoja ya pili (kiki) kwani ndani ya wiki moja tu baadhi ya wabunge hao walionekana wakizurura Dar na siyo karantini Dodoma! Mbunge wangu Sugu alipost mpaka picha akijinasibu kuwa yuko Dar anapiga supu ya pweza!

Leo tunaambiwa wamemaliza lockdown na wako tayari kurejea bungeni. Swali, kuna lockdown isiyoambatana na vipimo? Na je, kujiweka karantini na kisha kurudi kujichanganya na waliokuwa kwenye eneo lenye taarifa za maambukizi kama alivyosema katibu wao Mnyika leo, ni kujali afya zao?

Tatizo la kiki ni kuwa isipokuinua itakushusha. Kiki hii tayari imewagharimu chadema majimbo (wabunge) kadhaa. Pia waliotii amri ya mwenyekiti ni 15 tu! Hivyo takribani idadi kama hiyo au zaidi ilikaidi agizo hilo. Hii bila shaka inadhoofisha chadema kuliko kuiimarisha.

Kwa mtazamo wangu, kuelekea uchaguzi mkuu chadema inacheza kamari nyingi na haina muda wa kutafakari karata ipi itupwe na ipi ibaki mkononi. Mambo yatakayotokea mpaka Oktoba ni mengi hivyo Chadema wawe na utashi wa kuangalia lipi la kudandia na lipi la kuacha lipite.

Mathalani. Hivi karibuni vyama vyetu vikubwa zaidi ccm na chadema vyote vimepata kada walau mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za jinai/uhujumu uchumi. Wakati ccm wao wamejitenga na mtuhumiwa wao (silaha & ujangili) kama katiba yao inavyowaagiza chadema wao viongozi wao wako bize mitandaoni (twitter) kujieleza kwa niaba ya mtuhumiwa (mdude), impliedly wakikihusisha chama na tuhuma hizo.

Nawashauri chadema kuachana na kamari hizi na badala yake kujikita na maandalizi ya uchaguzi. Mfano, ccm wao wameanza kujiandalia media platforms kwa kutwaa channel 10 na magic fm. Chadema wana nini? Vipi corona ikiendelea na kampeni zikafanywa kwenye media! Wataitegemea TBC kisha waje kulia nayo baadaye? Huu ni mfano tu wa masuala ya muhimu kuhangaika nayo badala ya kutafuta ligi za kitoto na spika.
Wamemaliza lockdown? Wanarudi walikodhanibkuna korona, wamejiridhisha pako sawa sasa hivi au ndio kiki zenyewe zisizotumia akili..
 
Mbowe ni muhuni tu kama wahuni wengine. Binafsi nimeelewa Mbowe anatumia Cha Arusha ndiyo maana akili yake haipo sawa sawa.

Nawaambia kweli chadema Kama watapata hata viti vitano vya ubunge washukuru Mungu sana, wanamaamuzi ya kihayawani sana.

Wamekimbia kipindi muhimu na kwenye mijadala muhimu kwa taifa then wanajirudisha wakati mambo yamekwisha.

Mliowafukuza kwasababu hawakutii agizo la bwana wenu mbowe mmewaonea narudia tena mmewaonea kuthibitisha hili subiri adhabu yenu kutoka kwa wapiga kura wenu. Mnyika kibamba hatukutaki tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha Basi sawa
 
Back
Top Bottom