EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,356
Takriban wiki mbili zilizopia mwenyekiti wa Chadema Mbowe aliamuru wabunge wa chama chake kuanza lockdown mara moja pale Dodoma na kwamba wasiende majimboni kabla siku 14 hazijaisha ili wasije kupeleka maambukizi majimboni kwao!
Kulikuwa na namna mbili za kuitafsiri hatua hii. Mosi, upinzani kuna kiongozi shupavu asiyetetereka kimaamuzi. Pili, kwamba hiyo ilikuwa kiki tu ya kutafuta airtime na umaarufu hasa kwa mwenyekiti.
Binafsi naiamini zaidi hoja ya pili (kiki) kwani ndani ya wiki moja tu baadhi ya wabunge hao walionekana wakizurura Dar na siyo karantini Dodoma! Mbunge wangu Sugu alipost mpaka picha akijinasibu kuwa yuko Dar anapiga supu ya pweza!
Leo tunaambiwa wamemaliza lockdown na wako tayari kurejea bungeni. Swali, kuna lockdown isiyoambatana na vipimo? Na je, kujiweka karantini na kisha kurudi kujichanganya na waliokuwa kwenye eneo lenye taarifa za maambukizi kama alivyosema katibu wao Mnyika leo, ni kujali afya zao?
Tatizo la kiki ni kuwa isipokuinua itakushusha. Kiki hii tayari imewagharimu chadema majimbo (wabunge) kadhaa. Pia waliotii amri ya mwenyekiti ni 15 tu! Hivyo takribani idadi kama hiyo au zaidi ilikaidi agizo hilo. Hii bila shaka inadhoofisha chadema kuliko kuiimarisha.
Kwa mtazamo wangu, kuelekea uchaguzi mkuu chadema inacheza kamari nyingi na haina muda wa kutafakari karata ipi itupwe na ipi ibaki mkononi. Mambo yatakayotokea mpaka Oktoba ni mengi hivyo Chadema wawe na utashi wa kuangalia lipi la kudandia na lipi la kuacha lipite.
Mathalani. Hivi karibuni vyama vyetu vikubwa zaidi ccm na chadema vyote vimepata kada walau mmoja aliyekamatwa kwa tuhuma za jinai/uhujumu uchumi. Wakati ccm wao wamejitenga na mtuhumiwa wao (silaha & ujangili) kama katiba yao inavyowaagiza chadema wao viongozi wao wako bize mitandaoni (twitter) kujieleza kwa niaba ya mtuhumiwa (mdude), impliedly wakikihusisha chama na tuhuma hizo.
Nawashauri chadema kuachana na kamari hizi na badala yake kujikita na maandalizi ya uchaguzi. Mfano, ccm wao wameanza kujiandalia media platforms kwa kutwaa channel 10 na magic fm. Chadema wana nini? Vipi corona ikiendelea na kampeni zikafanywa kwenye media! Wataitegemea TBC kisha waje kulia nayo baadaye? Huu ni mfano tu wa masuala ya muhimu kuhangaika nayo badala ya kutafuta ligi za kitoto na spika.