IFM, MUM waenda Bodi kutaka asilimia 100


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
WANAFUNZI wanaokadiriwa kufikia 100 wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), jana waliandamana hadi Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), wakidai wapewe mikopo kwa asilimia 100.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti nje ya ofisi za Bodi hiyo, Msasani Dar es Salaam, wanafunzi hao walidai kwamba serikali imeidhinisha kupewa mikopo ya asilimia 100, lakini Bodi wameshindwa kutekeleza hali iliyosababisha wanafunzi wengine kushindwa kufanyiwa udahili.

Juma Hamis ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza IFM, alisema pamekuwepo na ongezeko kubwa la ada ambapo awali ilikuwa ikilipwa Sh milioni moja, lakini sasa imefikia Sh milioni 1.7, na serikali inawalipia Sh milioni moja tu.

“Ongezeko hili la ada nani atalilipa, hivi kwa mwanafunzi wa mkulima kule kijijini atatoa wapi hela hii jamani, serikali iliahidi itatoa mkopo asilimia mia, hivyo na sisi tunasubiri hivyo hivyo kama tulivyoahidiwa na si nusu,” alisema Hamis.

Alisema kutokana na hali hiyo, kuna wanafunzi ambao hawajafanyiwa udahili mpaka sasa kutokana na kushindwa kulipa Sh 800,000 ambayo inahitajika ili waweze kudahiliwa.

Kwa upande wake, Naibu Kiongozi wa msafara wa MUM, Hassan Jumanne alisema wanafunzi wa chuo hicho wamekuwa wakitaabika kutokana na wengi hao kukosa fedha ya kujikimu, ada na ya vifaa vya shule.

Akizungumzia hali hiyo, Mkurugenzi wa Mikopo wa Bodi hiyo, Lubambula Machunda alisema tatizo lililopo sasa linatokana na vyuo kupandisha ada wakati serikali ikiwa tayari imeshakaa na viongozi wa vyuo na kueleza bajeti halisi iliyopo.

“Kabla ya vyuo kupandisha serikali ilikaa navyo na kuwaeleza kwamba kwa mwaka wa masomo 2009/2010 itatoa mikopo kwa kiwango cha mwaka wa masomo

2008/2009 kutokana na ufinyu wa bajeti, lakini tunaona vyuo vinakazana kupandisha ada,” alisema Machunda.

Alisema makubaliano hayo yalitolewa baada ya serikali kukutana na wakuu wa vyuo na kabla wanafunzi hawajajaza fomu za kujiunga na vyuo hivyo kwa maana walikuwa wakifahamu ongezeko hilo la ada.

Alisema lengo la serikali ni kuwalipia ada wanafunzi wote wanaoenda vyuo vikuu, lakini

wanashangaa kuona vyuo vikipandisha ada bila kuangalia ufinyu wa bajeti. Alisema kutokana na tatizo hilo na hali iliyopo sasa

hivi hawawezi kutimiza madai hayo yaliyopo ya kulipa mikopo ya asilimia 100 na kuwataka wanafunzi hao waende Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambako huko baada ya mazungumzo, ilielezwa kuwa shauri lao litajadiliwa Jumatatu ijayo.
 
K

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,143
Likes
506
Points
180
K

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,143 506 180
mambo ya kienyeji enyeji tuu,vyuo vinajipandishia ada tuu bila kutoa taarifa na muda wa kutosha ili watu wajiandae,cha ajabu wanafunzi wao wote karibu 99% ada inatoka bodi ya mikopo...sijui watafukuza wangapi hapo?
 

Forum statistics

Threads 1,235,725
Members 474,712
Posts 29,232,447