IFM - Huu ni Uzembe

IFM - Huu ni Uzembe

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
1,031
Reaction score
302
Nilikuwa mahali, kwa bahati mbaya kuna wanafunzi wa IFM walikuwa wanaongea nikawa nawasikia. Inaonekana wapo kwenye mitihani kwa sasa. Lakini walikuwa wanaongea jinsi usimamizi wa mitihani ulivyokuwa wa kizembe hapo IFM.

Inaonekana wanafanyia mtihani kwenye vyumba vyenye computer, hao wasimazi kwa vile hawapo serious na kazi yao, wanafunzi wanaweka notes zao zote kwenye hizo computer na wanawasha hizo computer wakati wa mtihani na kucopy majibu.

Sasa inawezekana hao walimu labda wameongwa na baadhi ya wanafunzi ili wafanye hivyo. Najiuliza mambo mawili, kwanza kwanini mtihani ufanyike kwenye chumba cha computer wakati mtihani sio wa computer, pili wakati hawa wanafunzi wanajiachia kuwasha hizo computer na kucopy majibu hao walimu wanakuwa wamekaa wapi!!.

Tafadhali IFM mrekebishe hili haraka na msituletee makanyaboya huku mitaani.

 
Mkuu kuna kitu hujaelewa .... rectors wa CBE na IFM ni ndugu wa damu, yanyotokea CBE ndio hayo hayo yanayotokea IFM....
1. Ishu ya usimamizi wa mitihani watu wanaingia na simu wanagoogle, nini compyuta wapo wanaoingia na notice hizo hizo za mwalimu wao...
2. Kwa CBE walimu walikuwa wanaweza kuwapa wanafunzi mitihani hadi kesho yake ndio mkaja kufanya
3. Wasimamizi wanahongwa pesa kuleakisha pepa au hata kutuma mtu wa kuwafanyia maswali

Wabishe nije na majina ya walimu na wanafunzi waliohongwa jina kwa jina..hivi ni vyuo vya watoto wetu kukua wala si kujifunza wale wenye akili wachache ndio angalau....Mwl.

Njoo huku nkuoneshe hata namna ACCOUNTING yako inavyovujishwa hapo CBE..... mnafumbia macho uozo mtupu, kisa mnawaogopa wanafunzi na kutaka hela za rushwa, kama kufundisha hakulipi nendeni mkafanye kazi nyingine

Wakijibu nitarudi na namna wanavyoleakisha na kusahihisha Supp kwa kudai wanafunzi hongo..NACTE Kama haipo vile
 
Mbona toka zamani wanafunzi wanaokopi maswali ndo wako makazini na mavyeo makubwa tu? Unashangaa mkuu? Na ndo masna miaka ya 1990 IFM walikuwa wanatunga mitihani migumu hakuna mfano wakijua wanafunzi watakopi majibu. Sasa hasara ni kwa hao wasio na wa uwezo wa kukopi. Unapata lower second yako kisha ukiingia kwenye soko la ajira unapigwa chini anapewa mwenye Upper ama first class ya kukopi!!!!!!!
 
Shughulikia WA esrow kwanza ndugu,

Kuna mwanafunzi waESCROW alisomaga hapo PGD .. alitoa rushwa ya maana tu ili afaulu baadhi ya masomo.... tunashughulikia wote kwa mpigo... hatutaacha kumwadhibu mwizi wa boda boda kwasababu kuna wezi wa magari...wote wezi tu
 
Huo ni uzembe wa hali ya juu...kwa jinc hiyo tunazid kulididimiza taifa kwa kua na wasomi fake..
 
Mtoa mada muongo hakuna kitu kama hicho
 
Wasomi feki.viongozi feki alafu mtegemee maendeleo hii nchi kupata maendeleo sijui
 
Njooni kwenye interview muone watoto walivyo maboya! Hawajui hata hesabu za kujumlisha lkn ndo wamemalizia bcom sasaivi. Elimu yetu ni Majanga sana aisee.
Siku hizi kazi za wanavyuo ni kuchanga pesa na kuunga mkono wagombea urais wanaonunua uongozi km lowasa aka mamvi
 
Huu ni uongo na uzushi inaonekana mleta mada wewe naye ni mwanafunzi na wanafunzi wenzako waliofanyia lab wamekudanganya kuwa walifanikiwa kufanya hivyo ili kukurusha roho ukapata wivu..... narudia tena HAMNA kitu kama hicho maana kwanza notes hazikai computer lab na internet ya computer lab imefungwa wanafunzi hawawezi kutumia unlessnni wa IT na computer science ambao ma wenyewe kuna muda wao wa ku access
 
Njooni kwenye interview muone watoto walivyo maboya! Hawajui hata hesabu za kujumlisha lkn ndo wamemalizia bcom sasaivi. Elimu yetu ni Majanga sana aisee.
Siku hizi kazi za wanavyuo ni kuchanga pesa na kuunga mkono wagombea urais wanaonunua uongozi km lowasa aka mamvi

hamna Bcom ifm acha uongo nenda banks huoni vijana wanavyochapa kazi
 
Ila mbona ikija kwenye issue ya interview wanafunzi wa IFM ndio wanaoperform vizuri au na huko pia wanacopy!!!?
 
Back
Top Bottom