Ifike hatua Tanzania tutoke usingizini sasa; tuinue soko la sanaa kwa kutengeneza filamu zenye hadhi

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
415
1,032
Tumekuwa tukiangalia movies zenye story za kiafrica na kizungu pia, kama
  • Hotel Rwanda
  • Tears of the sun
  • Sometimes April
  • Border
  • Sarafina
  • Shaka ilembe
  • Roots
Zipo nyingi sana kuzitaja zote hapa zitajaza space tu; sasa twende kwenye hoja ninayokusudia kuiandika hapa.

Sisi Tanzania tunastory nzuri sana,yani endapo serikali ikahamka kutoka ndotoni,na wakaamua kweli kuweka hizo story kwa mfumo wa movies watapiga pesa sana, mfano story kama Vita vya Maji Maji na wale wazee wa kichaga kukatwa vichwa.

Mapinduzi ya zanzibar. Story ya mtu wa kale. Kama kweli wakiamua kuzitengenezea movie kali zenye hadhi ya rates zitauzika all over the world.

Tanzania tuna fursa kibao za kupiga pesa ila vichwa vyetu vimejaa mipira ndo maana utashangaa BUNGENI wanazungumzia hamsa ni ujinga wa hadhi ya fly over.

Tubadilike banaaa
 
Nani aangalie movie ya kukatwa vichwa, Mapinduzi ya zanzibar, na Story ya mtu wa kale hapa bongo let alone Duniani? Bongo tu zitakosa soko. Wewe lini umeangalia movie za Herero and Namagua genocide?

Mambo ya movies hata wewe unaweza kufanya sio lazima serikali.
 
Nani aangalie movie ya kukatwa vichwa, Mapinduzi ya zanzibar, na Story ya mtu wa kale hapa bongo let alone Duniani? Bongo tu zitakosa soko. Wewe lini umeangalia movie za Herero and Namagua genocide?

Mambo ya movies hata wewe unaweza kufanya sio lazima serikali.
Hizo movies zetu zikitengenezwa vyema zina hadithi tamu sana
 
Mambo ya pesa na serekali haifanyi biashara.
Ila n wazo zuri sanaa sio lazima wazawa waigize izo movie maana sisi badoo tunapayuka sanaaa.
 
Serikali haiwezi kupoteza resources zake. Hizo ni kazi za watu na makampuni binafsi.
You can say that again. Umasikini umefanya sanaa isiwe dili Tanzania hasa muvi na muziki. Sijasema bongo muvi wala bongo flava... Nimesema muvi na muziki kwa ujumla.

Mtoa mada kataja

Hotel Rwanda
Tears of the sun
Sometimes April
Border
Sarafina
Shaka ilembe
Roots

Swali ni copy ngapi original zilinunuliwa? Jibu ni chache sana au hakuna kabisa.
 
Back
Top Bottom