Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,162
- 5,692
Safi mleta mada swali langu hv hatuwezi kupata mashine inayoweza kubagua ama kutenga nafaka zilizoathirika na hiyo sumu!!??
Asante nakaweka nor soonMkuu basi hata ungeweka kapicha kanako onyesha tofauti kati ya mbegu yenye kuvu- sumu (mycotoxin) na mbegu ambayo haina hiyo kuvu-sumu.
Tayari mkuuAsante nakaweka nor soon
Wala dona ndio wahanga wakubwa wa hili janga.
Dokita Ndodi Mungu anakuona kwa upotoshaji wako.
Mimi napiga sana ugali ila dona na udaga ule wa Kisukuma mniwie radhi.Ah..ah...ina madhara makubwa sana hiyo Mkuu.
Ya haraka ni sumu inaua ila ya taratibu ni kuharibu kinga ya mwili na saratani.
Wale wapeenzi wa udaga tuwasiliane.
.... tena dona; ni hatari.Ndio maana sipendi ugali
Utafiti kuhusu sumu kuvu hasa aina ya aflatoxin ulianza kushika kasi miaka ya 1960 baada ya kutokea mlipuko wa vifo vya bata mzinga (turkeys) huko nchi za ulaya baada ya kupewa vyakula vyenye aflatoxin ambavyo baadaye iligundulika vilitengenezwa na karanga kutoka Brazil, na huo ugonjwa kujulikana kama Turkey X Disease...mabadiliko ya tabia nchi huweza kusababisha kuongezeka na kusambaa kwa fungus na wadudu wanaoshambulia mazao na pia ukame ambao huweza kuathiri mazao kuhimili kupambana na wadudu waharibifu na fungasi wanaozalisha aflatoxin kwenye mazao..Kuna swali najiuliza hapa naomba kusaidiwa.
Je hii sumu kuvu ipo tangu lini? kama ipo tangu zamani je madhara yake hayakugunduliwa tangu zamani au ndo watu walikua wanakufa bila taarifa? au madhara yake yamekuzwa kipindi hiki cha dot com? maana imeanza kutiliwa mkazo sana miaka ya karibuni hapa...au mabeberu wanatumia sumu kuvu kututishatisha kama ilivyo koona? maana mababu na mabibi zetu walipiga sana dona kabla ya mashine za kukoboa kuwasili nchini kwetu....nadhani naweza kupata majibu kwa wenye uelewa juu ya suala hili la sumu kuvu...shukran
Shukran mkuuUtafiti kuhusu sumu kuvu hasa aina ya aflatoxin ulianza kushika kasi miaka ya 1960 baada ya kutokea mlipuko wa vifo vya bata mzinga (turkeys) huko nchi za ulaya baada ya kupewa vyakula vyenye aflatoxin ambavyo baadaye iligundulika vilitengenezwa na karanga kutoka Brazil, na huo ugonjwa kujulikana kama Turkey X Disease...mabadiliko ya tabia nchi huweza kusababisha kuongezeka na kusambaa kwa fungus na wadudu wanaoshambulia mazao na pia ukame ambao huweza kuathiri mazao kuhimili kupambana na wadudu waharibifu na fungasi wanaozalisha aflatoxin kwenye mazao..