Ifahamu Sifongo iliotiwa Siki aliyopewa Yesu akiwa Msalabani

Km sifongo siki ni sumu na wao walikuwa na lengo la kutaka afe haraka kwanini hawakupaka kwenye ule mkuki waliomchoma nayo ubavuni? Sumu kupitia mdomoni huchelewa kidogo kuua kuliko ile iliyowahishwa kwenye damu. Na je km lengo ni kuua fasta si pale kuna mkuki kwann wasimchome moyoni fasta hamalizi hata sekunde?
Unatuuliza sisi?Nahisi lengo la mtesi ni kukukomoa.Yaani kukufanya ujisikie kudunishwa?Maana nafikiri maji yalikuwepo na hayo ndo hukata kiu kuliko kinywaji chochote, kitendo cha kumpa siki iliyochanganywa sifongo nahisi ilikuwa nia ovu .
 
Wanasema.

Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote.

Anayeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani kufanyika popote.

Hakuuumba ulimwengu huo.

Kaumba ulimwengu ambao dhambi inawezekana kufanyika.

Hata katika ulimwengu ambao dhambi inaweza kufanyika, aliweza kuumba watu ambao wanaweza kuishinda dhambi mara zote.

Hajaumba watu hao.

Kaumba watu ambao wanaweza kushindwa na dhambi.

Halafu watu hao wakishindwa na dhambi, kwa sababu Mungu kaumba ulimwengu ambao dhambi inawezekana kufanyika, na watu wanashindwa na dhambi, Mungu huyo atawahukumu watu hao kwa kuwachoma katika moto wa milele.

Ni kama Baba anayeweza kumsomesha mtoto wake shule (Mungu anayeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani) akaamua kumkataza mtoto wake asisome shule (Mungu huyo akaumba ulimwengu ambao dhambi inawezekana kufanyika) halafu mtoto akishindwa kujua kusoma na kuandika kwa sababu (mtu akifanya dhambi) baba amuadhibu mtoto vikali (Mungu awaadhibu watu kwa moto wa milele).

The premise and narrative is illogical.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Baba mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kumkataza mtoto wake kwenda shule, halafu baba huyo huyo amuadhibu mtoto huyo, kwa kuwa hajui kusoma.

Huu ndio ujinga ninaokataa katika dini.
Tatizo unafikiri mawazo yako ni mawazo ya Mungu.Ukigundua awazavyo Mungu sivyo uwazavyo wewe na njia zake sio zako basi utamwelewa .Kwa sasa endelea kupambana naye kwa uwezo alokupa maana ushafeli kumwelewa,ili usiwe na utetezi mbele yake siku ikifika.
 
Tatizo unafikiri mawazo yako ni mawazo ya Mungu.Ukigundua awazavyo Mungu sivyo uwazavyo wewe na njia zake sio zako basi utamwelewa .Kwa sasa endelea kupambana naye kwa uwezo alokupa maana ushafeli kumwelewa,ili usiwe na utetezi mbele yake siku ikifika.
Unahakikishaje Mungu yupo kweli, na habari za kuwapo kwake si hadithi za watu tu?

Hujathibitisha hili.

Thibitisha Mungu yupo kabla ya stories nyingi za Mungu hivi, Mungu vile.
 
Back
Top Bottom