Mvumbuzi mkubwa kuliko wote katika historia ya ulimwengu. Ubora wa maisha ya binadamu wa sasa una deni kubwa na kazi ya Edison. Elimu yake ya darasani ilikuwa ndogo, lakini aliweza kujipatia haki miliki (patents) 1,093 za vumbuzi kubwa mbalimbali huko Marekani, zikiwemo zile za balbu ya umeme, kamera ya picha za sinema na kinasa sauti. Alipovumbua kinasa sauti mwaka 1877 wananchi walimwita mchawi.
Sifa yake kubwa iliyomletea mafanikio ni kwamba alikuwa king’ang’anizi. Uwezekano wa kushindwa hakuupa nafasi katika akili zake. Kila alipofikiria kuvumbua kitu aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuwaeleza nia yake. Hakuogopa kuwa akishindwa watu watamcheka. Kila alipofanya jaribio likashindikana aliendelea kufanya jingine na jingine na jingine mpaka alipofanikiwa. Idadi ya majaribio aliyofanya kabla ya kufanikiwa kuvumbua balbu ya umeme ni zaidi ya elfu moja.
Tunajifunza nini? Uking’ang’ania mafanikio una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Lakini ukibweteka na kungoja bahati una nafasi ndogo ya kufanikiwa. Hapa kwetu tunahimiza watu kulima vanilla, zao ambalo linaota vizuri na ambalo bei yake katika soko la dunia ni dola za Marekani 500 na zaidi kwa kilo. Ni dhahiri kuwa zao hili ni jawabu la umaskini katika jamii maskini.
Mkulima mmoja kutoka kata jirani ameweza kujipatia Tshs 150 milioni kutoka kwenye shamba lake dogo katika msimu mmoja. Watu wanaomzunguka ni maskini, lakini hawavutiwi kulima vanilla kama yeye. Sababu ni changamoto ya wezi.
Hawajui kuwa changamoto ikikukatisha tamaa itaua maendeleo yako. Aidha hawajui kuwa hakuna changamoto isiyo na jawabu.
Wakulima wa vanilla wenye mafanikio ni wale wanaong’ang’ana. Ni wale wanaochemsha bongo kutafuta jawabu la changamoto wanazokabiliananazo. Kama Thomas Edison asingechemsha ubongo na kung’ang’ana, maisha mazuri tuliyonayo yangechelewa sana. Labda hadi leo tungekuwa tunatumia kibatari wakati wa usiku.
Sumu ya maendeleo yoyote ni kukata tamaa.