Ifahamu nchi yetu tanzania na watu wake!!

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Pamoja na kwamba nchi yetu ya Tanzania inasifika kwa mambo mengi, ikiwemo vivutio vingi vya utalii, madini, maziwa na bahari n.k

Pia kuna jambo ambalo limekuwa la upekee kwa watanzania, yaani mataifa jirani huwa wanapofika Tanzania huwa wanashangazwa sana na Umoja na Mshikamano tulionao sisi watanzania, namna tunavyoshirikiana, tunavyopendana na kuwa wamoja kama taifa ilihali tuna mrundikano wa makabila takribani 120

Lakini upekee huo unaowashangaza wageni wengi upo tofauti kidogo kwenye eneo moja tu, ambalo ni mpira wa miguu

Ni kwenye mpira wa miguu ndipo watanzania tumegawanyika na kupalaganyika, huyu atasema hivi na huyu atasema vile, tunapingana sana na kubishana sana, hatuna kauli moja kuhusu mpira wa miguu

Ni kama hatujui tunataka nini na hatutaki nini, na hata tukijuwa tunachokitaka bado tunashindwa kutambua wakati gani ni sahihi wa kutaka hicho kitu.

Sisi tulioko uhamiaji huwa tunapowakaribisha wageni na huwa tunawaambia yafuatayo kuhusu mpira wa miguu

Karibu Tanzania, nchi ambayo timu ya taifa ikifungwa, anakuwa amefungwa mchezaji aliyecheza vibaya kwa mechi hiyo au aliyefanya kosa likasababisha tukafungwa

Wanasahau mpira ni mchezo wa makosa, huwezi kufungwa bila kukosea, wanasahau kuwa kuna wachezaji bora walifanya makosa makubwa kwenye mashindano makubwa yaliyopelekea timu zao kupoteza mechi, mfano ni Zidane kwenye fainali ya kombe la dunia 2006

Karibu Tanzania, nchi ambayo timu ikishinda mechi, aliyeshinda ni mchezaji na sio timu, aliyefunga bao la ushindi na kucheza vizuri ndiyo Taifa Stars, na sio wachezaji 11 waliovuja jasho kwa dakika zote walipokuwa uwanjani

Wanasahau wahenga walishasema, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, mpira ni teamwork, inapotokea timu imeshinda maana yake idara zote uwanjani zilitekekeza majukumu yao ipasavyo,

Waliokuwa kwenye ulinzi wamelinda vizuri, waliokuwa kwenye ushambuliaji wameshambulia vyema, na hata idara ya kiungo imetekeleza majukumu yao ipasavyo, hata inapotokea mchezaji anaibuka kuwa nyota wa mchezo usifikiri ingewezekana kuwa nyota bila wenzake kumsaidia

Karibu Tanzania, nchi ambayo watu hawaheshimu taaluma za makocha na wakufunzi bali mapenzi binafsi na hisia zilizojaa mihemko

Ni Tanzania pekee ambayo kikosi cha wachezaji 11 wanaoenda kucheza mechi, kikitoka tu unasikia watu wanasema mbona fulani hayupo, hii mechi tushafungwa, kocha hamna kitu humo,

Anayeyasema hayo unakuta hajui hata kupiga danadana au kutuliza mpira, hata kama anajuwa hayo basi hana taaluma ya ukocha, na ukute hajawahi kufundisha hata timu ya mtaani kwao, Lakini ukimkuta anaongea unaweza kudhani huyo ni Pep Guardiola au Vicente Del Bosque, au Sir Alex Ferguson

Wanasahau kwamba, jambo la kwanza linalozingatiwa kwenye upangaji wa kikosi ni performance nzuri ya mchezaji wakati wakiwa mazoezini, kisha mbinu za kocha, aina ya mpinzani wako unayeenda kukabiliana nae n.k

Sijui ni kwa bahati mbaya au ni mukusudi, hata wale wenye taaluma ya ukocha, nao wametawaliwa na mapenzi binafsi na hisia zilizojaa mihemko, tumewapa dhamana ya kuwasikiliza ili walisemee jambo kwa utaalamu Lakini unashangaa mtu badala ya kujikita kwenye hoja za kiufundi nae anaanza kulaumu kama sisi tusiokuwa na taaluma ya mpira, mwisho wa siku tunashindwa kutambua tatizo ni nini maana tatizo ni sisi wenyewe

Karibu Tanzania, nchi ambayo inaamini katika hamasa kuliko mipango na maandalizi ya kimkakati

Sir Alex Ferguson alipokuwa anakabidhiwa ratiba ya EPL, alikuwa anakaa na jopo lake, wanafanya tathimi na mchanganuo wa ratiba kisha anapoint mechi ambazo anaamini atazishinda, kisha zile ngumu ambazo si rahisi kupata alama 3, zinafanyiwa mikakati,

Kwahiyo anapoenda kuanza ligi alishajuwa ana point ngapi kutoka kwa wapinzani aliowaona ni rahisi, kama kwenye tathimi wamepata point 50 za uhakika, basi point zinazosalia zinabebwa kimkakati, anajuwa mpinzani huyu lazima tugawane point, akinifunga kwake basi mimi nitamfunga kwangu, isiwezekane akachukua zaidi ya alama 3 kwenye mechi 2

Lakini kwa Tanzania ni tofauti, utashangaa zinaundwa kamati za hamasa wakati ambao imebaki mechi moja au mbili kuamua uelekeo wa timu,

Unashangaa tunahamasishwa kujaa uwanjani, na maneno mengi ambayo kimsingi yanaishia nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja yanafanyika mambo yanayodhihirisha kuwa hamkuwa na mipango wala mikakati na ubora wa kupata matokeo chanya

Wakati Ujerumani wanachukua kombe la dunia mwaka 2014, haikuwa bahati mbaya, walikuwa na mikakati na mipango ya miaka 3 kabla, yaani baada ya Hispania kutwaa ubingwa wa dunia ndipo Ujerumani walianzia mipango pale

Wakasambaza vijana wengi kwenye mataifa mbalimbali balani ulaya, Ujerumani ikapata mechi nyingi za kirafiki, ndilo taifa lililocheza mechi nyingi kuliko mengine mpaka kufikia kwenye mashindano ya kombe la dunia, bajeti ikaongezeka, mwisho wa siku Ujerumani ikabeba ubingwa wa dunia

Hiyo ndiyo mipango na mikakati, mipango ambayo huwezi kuona Tanzania tunaiwazia hata robo yake, sisi tumekaaa kibarazani tukisubiri maajabu badala ya uwezo

Na hii ndiyo Tanzania, nchi ambayo ina wachambuzi wengi wa facebook na whatsapp lakini hawalipwi
 
Wewe mwenyewe ulivyoongea haijulikani kama ni kocha, shabiki, mchambuzi au afisa habari maana sehemu zote umejiweka
 
Inaonekana kabisa wewe ni shabiki wa simba yaani.. ukweli ni kwamba simba imefungwa na siyo taifa Stars..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom