Kuna Dada yangu mmoja alikuwa anamdai kaka mmoja kila siku anampiga Chenga akimpigia simu hapokei.
Siku moja Dada akapiga yule kaka kampa simu yake Mke wake ili aongee na Dada umwambie mwenye simu hayupo.
Mke kupokea tu Dada akaamua kumkomesha.
Dada: hello we nan? Mbona unapokea simu isokuwa yako.
Mke wa jamaa: una shida gani mwenye simu katoka.
Dada: akija mwambie Niko hospital leo mtoto tumboni kasumbua sana, na siku za kujifungua zinakaribia.
Mke wa jamaa:aliporomosha matusi 1500
Dada: kakata simu
Baadae sasa Mke kafunga mizigo yake hadi kwao, wachungaji wakaitwa, mme kakana hana mahusiano na Dada na kweli hakuwa na mahusiano nae.
Msimamizi wa ndoa katumwa kwa dada kupeleleza kama kweli ana mimba , Dada kamjibu mwambie alete hela yangu. Hii njia itanisaidia lazama alipe.kweli baada ya week akalipa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]