Habari wakuu.
Kwa yoyote mwenye uelewa kuhusiana na hii platform ya IDEA DEBATERS inayotrend sana mtandaoni. Naomba ufafanuzi zaidi ya namna inavyofanya kazi na usalama wake wa kuinvest izo pesa ukoje.
Asanteee
Nitajaribu kukuelezea kutokana na uelewa wangu, kwanza issue ya usalama wa pesa zako hakuna mtu atakupa jibu la uhakika maana pesa zako unaweka kwao na unakuwa huna mandatory nazo tena, kwahiyo Hadi unaamua kuweka pesa yako basi uwe umekubali yote, maana ume risk na chochote kinaweza kutokea
Me Kwa mara ya Kwanza naskia kuhusu hii issue alinambia jamaa yangu, baada ya kumskiliza niligundua kuwa ni kweli pesa IPO ila kuipoteza pia ni dakika sifuri, ila niliamua kujilipua Tu Kwakuwa nilikuwa na shida na pesa ya haraka
Hawa jamaa wao wanadai wanadeal na kutangaza matangazo mitandaoni, kwahiyo makampuni yanayofanya biashara za mitandaoni kama vile eBay, Amazon nk, yanatoa pesa kwa ajili ya watu kuangalia matangazo ya bidhaa zao na kupandisha rates za bidhaa zao hivo kupandisha thamani, kwahiyo we ukiingia Amazon unakuta bidhaa ina rate ya 5 star kumbe ni fake
Unachofanya ni kujiunga na hiyo IDEA kisha unatakiwa kuwekeza kiwango cha pesa ambacho we utakuwa unalipwa Kwa % kulingana na kiasi ulichowekeza na level uliyopo, kuna level 1,2,3,4,5 na 6
Kwa level 1 unatakiwa kuweka pesa kuanzia 10000-199999, unapewa matangazo ambayo wao huita Task, kwahiyo unapewa task 20 kila siku utazame, mfano ukiweka 50000 utaanza kulipwa 5% ya pesa yako, kwahiyo Kwa siku utaanza kupata 2500, na kwakuwa kesho utakuwa na 52500 kwahiyo utalipwa 5% ya kiasi hicho, Kwa lugha rahisi kila siku kiwango chako kitapanda
Na hiyo sio njia pekee ya wewe kujipatia pesa, njia ingine ni kupitia kualika watu wengine ili washiriki kwenye huo Mchongo na kila ambae utamualika kupitia link yako atakuwa anakuchangia, mwanzo ilikuwa kwa kila unaemualika wanakupa 2000 na aliealikwa anapata 1000, saiz hiyo offer imeisha ispokuwa utapata hela endapo huyo mtu ataweka pesa na kuwa anafanya task zake kila siku we unapata commission ya 12% ya pesa yake aliyowekeza, na yeye akiunga mtu mwingine we unaendelea kupata commission ya 4%
Njia ingine ya kupata pesa ni Kwa wewe kupanda daraja/levels, ukitoka level 1 kwenda 2 unapata 5000, na level 2 kwenda 3 unapata 10000 na 3 kwenda level 4 unapata 20000, kumbuka kuwa kuna vigezo vya kupanda hizo levels, kutokana na kiasi cha pesa unachoweka na idadi ya watu uliowaunga
Unaweza kutoa pesa Kwa kutumia account ya bank au simu ya mkononi na pesa yako utaipata kuanzia masaa 0-72, kwahiyo unaweza kutoa Leo hela yako ukaipata kesho ni kawaida, Hadi hivi sasa hakuna mtu aliepigwa kwahiyo kama utaamua kujiunga basi jiunge at your own risk
Kwa hayo machache kama umeelewa na kushawishika kujaribu basi weka pesa ambayo ni kama Ile ambayo unabetia, kwamba ukose au upate haina Athari hasi kwako, me nilianza na 130k trh 9 Hadi Leo nina 490k na kesho nategemea kuingia level 3 ili nianze kulipwa 7% ya pesa yangu Kwa siku
na kuna account tuliungana watu wa3 kila mmoja akaweka 250k na Juzi tumetoa 1.5M na kupiga mgao, lengo ilikuwa ni kurudisha pesa zetu na faida ndani ya muda mfupi ili ata tukipigwa tuwe hatuna hasara
Kama unataka kujaribu then jaribu kupitia hiyo link, hope Kwa maelezo haya unaweza kuwa umepata mwanga angalau