Iddi Simba kufikishwa Mahakamani; Tafsiri yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iddi Simba kufikishwa Mahakamani; Tafsiri yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 29, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,044
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Nimeiona habari kubwa kwenye ITV usiku wa leo; Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Iddi Simba amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Ni Iddi Simba ambaye alilazimika kujiuzuru uwaziri kwa kashfa ya sukari. Ni Iddi Simba ambaye huko nyuma aliipigania sana sera ya Uzawa.  Na kadhia iliyomkumba sasa inahusu kafsha ya UDA. Ni lililokuwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam. Iddi Simba amesomewa mashtaka 8 ikituhumiwa kudanganya, kughushi na kulitia hasara ya shilingi milioni 320 Shirika la Usafiri Dar es Salaam ( UDA).  Tafsiri yangu;

  Huu ni mwendelezo wa mwanzo uliotiliwa mashaka. Kuna watakaoanza kuamini, kuwa zama za kulindana zimeanza kufikia ukingoni.


  Iddi Simba ni kigogo. Ni Mzee wa Dar es Salaam. Ni Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam. Leo amefikishwa kwenye Mahakama ya katikati ya Jiji la Dar. Bila shaka, kuna ambao hawakuamini kumwona Idi Simba kwenye runinga akikalia kwenye benchi la Mahakamani.


  Naam, tunaziona ishara la wimbi kubwa linalokuja, si dogo hata kidogo. Yumkini naye anasafisha njia ya wengine kufuatia. Na tusubiri tuone.


  Maggid Mjengwa
  Iringa
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo


  0788 111 765   
 2. T

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,710
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  IDDI simba ana tofauti gani na waliokuwa mawaziri wawili YONA na MRAMBA?
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,172
  Likes Received: 4,505
  Trophy Points: 280
  Mjengwa,
  Hii habari ipo toka mchana humu JF tatizo lako Mjingwa ukiwa humu JF unakuwa mbinafsi sana uchangii thread yoyote zaidi ya kwako kama saizi umetupia thread yako kama promo nakuondoka...unashindwa hata kutoa Like
   
 4. M

  Mdomo Mwepesi Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Harakati zake za kupigania sera ya uzawa zilikuwa ni jitihada za kutaka kuficha maovu yake aliyokuwa akiyafanya au kufikria kuyafanya. Huyu ni mtu hatari -mchana ni binadamu na usiku ni "dracula".
   
 5. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 3,699
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hakuwashirikisha wenzake kwenye huo mchongo.
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,535
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Huyu ndiyo aliuza NBC kwa makaburu akiwa mwenyekiti wa board, ni kawaida yake ni raia wa Burundi aliyevaa utanganyika sasa atajuta kuifahamu Tanganyika lazima anyee debe babu huyu anjifanya tajiri kumbe jangiri
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,564
  Likes Received: 398
  Trophy Points: 180
  Tangu lini kufikishwa mahakamani ikawa ni jambo la kushtua. Cha kushtua ni hukumu inayotolewa. Kila siku tunasikia msururu wa "vigogo" mahakamani, lakini hatujabahatika kusikia hukumu zao za mwisho!
   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 9,187
  Likes Received: 1,382
  Trophy Points: 280
  basi naye tutamchinia
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,410
  Likes Received: 708
  Trophy Points: 280
  Huyu Idd Simba sasa madhambi yake aliowafanyia watu wengine yanamrudia; alikula fedha za EPA na akanunua shares kwenye benki ya Mafisadi [ BANK M] lakini wakina Maranda na Farijallah alioshirikiana nao katika wizi, wao wamefungwa lakini yeye yuko nje.!! Now time has caught up with him.
   
Loading...