Mlima kusema kweli, ni mama yetu wa asili
Hututunza kwa mengi,maji mvua na hewa
Kama mama anaungua, hima tuondoe hii balaa
Tutateketea bila kujua, haraka tuzuie ukiwa
Mlima sote twajua, ni mama yetu wa asili.
Aisee Idd Ninga, hii mistari koko mitano imenitoa jasho lita mbili!
Ni zoezi zuri kwangu hivyo endelea kunipa changamoto
Kikali kuliko nyundo, chachongwa tena maumbohausikii kishindo,kikubwa kunalipuka.
kikali kuliko nyundo,nalo jivu linaruka.
na moto upo marundo,sauti inasikika.
miale ipo mafundo,itachoma ikiwaka.
nani wakulinda lindo,na mlima una waka ?
Ilongailunga
hausikii kishindo,kikubwa kunalipuka.
kikali kuliko nyundo,nalo jivu linaruka.
na moto upo marundo,sauti inasikika.
miale ipo mafundo,itachoma ikiwaka.
nani wakulinda lindo,na mlima una waka ?
Ilongailunga
Kikali kuliko nyundo, chachongwa tena maumbo
kwanini yawe mafundo, kumiza yetu matumbo
basi tulitie pindo, tubomoe chetu chombo
hadidhi ya bwana tindo, Leo nakupa matambo
hakufwata zake nyendo, mkongwe mwenye kifimbo
kusuka pekee kindo, ukiri USO mayombo
hata yule mweka kando, hajui hana hujambo?
risala iso na mwendo, mechoka tena kitambo
Mkuu. Nawapenda sana washairi. Sijui kutunga lakini ninaposoma huwa najisikia raha sana..
Ila ninachokiona ili uwe mshairi basi meneno mengi ya kiswahili uyajue.
Hongereni sana pamoja na mleta uzi.
alaaaaaa,balaaaa
tungo zenyewe kwa fungo,alonaswa na urimbo.
tuvifungue vifungo,tulofungwa tangu tambo .
tena tuiteme nyongo,kwa sifa pia matambo.
na kilima kizimike,alowasha tumshike.
Ilongailunga
alaaaaaa,balaaaa
tungo zenyewe kwa fungo,alonaswa na urimbo.
tuvifungue vifungo,tulofungwa tangu tambo .
tena tuiteme nyongo,kwa sifa pia matambo.
na kilima kizimike,alowasha tumshike.
Ilongailunga
mweledi mshinda uga, sikia hii habari
uwache nao uoga, kilele ukitayari
usipande na maboga, usije tiwa shubiri
saambovu alo kiga, jamani hana hiari.