Idd Azzan: Nitashirikiana na Mtulia kuleta maendeleo Kinondoni

babutz

Member
Dec 24, 2016
68
80
“Dhamira ya Mtulia akiwa Chama kile(CUF) ilikuwa kuwatumikia wananchi wa Kinondoni ila kwa bahati mbaya sana kule alikokuwa( CUF) alishindwa kutekeleza adhima yake, Baada ya kuona anashindwa kutekeleza dhamira yake akaamua kuachana na Ubunge kupitia Vyama hivyo(Upinzani) na kuamua kujiunga na Chama chetu(CCM) ambacho ilani yake ndiyo imatekelezwa hivi sasa nchini.Baada ya Mtulia Kuhamia CCM, Chama Cha Mapinduzi kimeamua kumrudisha agombee tena ili atekeleze adhima yake ya kuwatumikia wana kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi” – Idd Azzan, Mbunge Mstaafu wa KInondoni

“Unapokuwa kiongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi ambacho ndio kimeshika Dola maana yake matatizo yetu na kero zetu zitaondoka kwahiyo mkimchagua Mtulia hivi sasa Mtakuwa mmemchagua Mtulia wa CCM atakayetekeleza Ilani ya CCM na yale ambayo aliyakusudia kuyatekeleza kipindi kile sasa yatakuwa ni Rahisi kweke kuyatekeleza kwasababu atakuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi”- Idd Azzan, Mbunge Mstaafu wa KInondoni

“Kuuchagua Upinzani ni sawa na kujenga Ukuta wa kujizuia na maendeleo, Viongozi wa Upinzani kazi yao kubwa ni kutukana na sio kuomba maendeleo, lakini unapochagua Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ni kama unatengeneza daraja ya shida zako zifike serikalini na shida zako zitatuliwe” - Idd Azzan, Mbunge Mstaafu wa KInondoni

“Mwaka 2015 tulipata fedha toka benki ya Dunia kwa ajili ya kuutanua mto Ng’ombe pamoja na kuujengea Kingo kwa kiwango cha Zege, hayo yalitakiwa yafanyike ila mfuatiliaji wa hayo hakuwepo, Mtulia alikuwa Upinzani na alishindwa kuniuliza mimi na mimi kumwambia Sikuweza. Ila sasa kwakuwa yupo CCM tutamwambia yote, Tutamwelekeza yote na tutasimama pamoja ili mto Ng’ombe uweze kutanuliwa na kujengwa kwa kingo za Zege ili kukomesha maafa yatokanayo na mvua kwa wananchi wa kinondonii, CCM Oyee”- Idd Azzan, Mbunge Mstaafu wa KInondoni

Hayo aliyasema januari 30, 2017 kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Kinondoni katika Uwanja wa Mwika Kata ya Ndugumbi akiwa anamnadi Mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Maulid Said Mtulia.

[HASHTAG]#ChaguaCCM[/HASHTAG]
[HASHTAG]#ChaguaMtulia[/HASHTAG]
[HASHTAG]#UshindikwaMtulia[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TukutaneKazini[/HASHTAG]
 

Attachments

  • IMG_1517404278981.jpg
    IMG_1517404278981.jpg
    14.4 KB · Views: 29

Similar Discussions

Back
Top Bottom