Idara ya maji Mbeya Mji

mwanamakole

Member
Dec 3, 2015
86
125
Hii ni kero kubwa kwa eneo husika.

Eneo ni Iyunga-Inyala Zone 9. bomba limekuwa likipasuka na kutiririsha maji yanayoharibu barabara iliyogharamiwa na raia wa eneo husika, fundi wenu wa eneo hilo ni mara nyingi kwa vipindi tofauti amekuwa akilitengeneza lakini baada ya mda mfupi linaachia, sababu aliyoisema ni kwamba bomba la eneo hilo ni dogo (Diameter) na maji yana pressure kubwa inayopelekea kuachia mara kwa mara.
Hoja ni kwamba: Je hivi ni kweli mmeshindwa kudhibiti tatizo hili? tangu 2011 tatizo limekuwa sugu.
Bili za maji mmeongeza, kwa nini hamboreshi miundo mbinu?
Mara kadhaa mmepigiwa simu na watu tofauti mnaahidi kutengeneza lakini jitihada zenu hazionekani na barabara inazidi kuharibika.

mwaombwa tatueni hili tafadhali!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom