Idadi ya waliokufa Myanmar kufuatia mapinduzi ya Februari mosi yafikia 550

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Kundi la kutetea haki za binaadamu nchini Myanmar limesema idadi ya watu waliofariki kutokana na kamata kamata inayofanywa na jeshi imefikia 550 wakiwemo watoto 46 tangu kulikofanyika mapinduzi ya serikali Februari mosi. Kundi hilo limesema takriban watu 2,751 wamekamatamwa au kushitakiwa.

Hata hivyo vitisho vya vurugu na kuwakamata waandamanani kunakofanywa na jeshi, kumeshindwa kuwadhibiti waandamanaji wanaojitokeza barabarani kila siku nchini humo wakilitaka jeshi hilo liachie madaraka na kuurejesha utawala wa kiraia uliochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Ijumaa iliyopita polisi waliokuwa wamevalia nguo za kawaida waliwakamata watu watano baada ya kuzungumza na muandishi habari wa shirika la kimataifa la CNN katika soko la Yangon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…