UN yatahadharisha juu ya ongezeko la njaa Myanmar

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Umoja wa Mataifa umesema leo Ijumaa kuwa unahitaji kwa dharura fedha zaidi ili kuwasaidia watu nchini Myanmar kufuatia hofu kuwa watu wapatao milioni 6.2 huenda wakakabiliwa na njaa ifikapo mwezi Oktoba.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Myanmar, Stephen Anderson, amesema karibu asilimia 90 ya watu wanaoishi katika makaazi duni mjini Yangon wanalazimika kukopa pesa ili kununua chakula.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani limesema lina upungufu wa asilimia 70 ya dola za Kimarekani milioni 86 zinazohitajika katika kipindi cha miezi sita ijayo, wakati nchi hiyo ya Asia inakabiliwa na changamoto kadhaa.

Shirika hilo la WFP limesema Myanmar inalemewa na idadi kubwa ya maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19, ongezeko la njaa na kupanda kwa gharama ya maisha.

Myanmar imetumbukia katika machafuko na uchumi wake kuporomoka baada ya jeshi la nchi hiyo kuchukua madaraka kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia, Aung San Suu Kyi, mnamo Februari Mosi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom