ICU mpya yazinduliwa Muhimbili

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamisi Kigwangalla amezindua chumba kipya cha kulaza wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika jengo la Mwaisela, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo wa huduma bora, umetajwa kuwa ni njia ya kuelekea kuondokana na kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Dk Kigwangallah alisema ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa, serikali itaondoa huduma ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na ndiyo maana inaendelea kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo ya taifa.

Alisema huduma hiyo itatolewa kwa gharama nafuu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alisema wizara inaangalia vizuri jinsi ya kuondoa utaratibu huo wa kupeleka wagonjwa nje. “Sasa muanze kujipanga hapa Muhimbili.

Endapo kutakuwepo na mgonjwa anayetaka kwenda nje idara husika ndiyo itampeleka baada ya kujiridhisha wao wameshindwa kumtibu. Hapa kazi tu haya ndiyo mabadiliko ya kweli ya serikali ya awamu ya tano tunayoyaleta. “

Tumeshaanza kuweka utaratibu tunahama kutoka kupeleka wagonjwa nje tunawaleta hapa,” alisema Naibu Waziri huyo. Alisema kila taasisi itakuwa na bajeti yao, wao kama wizara watakuwa wanapanga bejeti ya kuhudumia kila idara.

“Sisi tunataka kutoa lawama hiyo kwetu kama wizara ibaki kwenu hospitalini. Tunaondoa siasa iliyozoeleka kuwa viongozi ndio wanaopeleka wagonjwa wao nje,” alisema. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru alieleza furaha yake kushuhudia uzinduzi wa upanuzi wa huduma za tiba ya wagonjwa mahututi itakayokuwa ikifanyika hapo wadini baada ya kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wake pamoja na kufungwa kwa vifaa tiba vya kisasa.

Alisema uongozi wa hospitali hiyo umesimamia uboreshaji wa huduma ya tiba ya wagonjwa mahututi kwa upanuzi na uwekezaji wa vifaa vya kisasa katika wadi hiyo ya Mwaisela kama vile mashine za kupumulia na vifaa vya uchunguzi wa kihadubini kwa magonjwa ya tumbo na mapafu.

Pia ultrasound ya kisasa inayochunguza mishipa ya damu, vitanda vya kisasa kwa matumizi ya wagonjwa mahututi ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo ya kitaalamu.
 
Ni jambo jema hofu yangu kwa watalamu wasiowazalendo wanaoharibu vifaa vya serikali kwa makusudi ili waende kwenye hospital zao.
 
Back
Top Bottom