mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,183
- 1,083
Tuna kila sababu ya kuchukua tahadhari dhidi ya maadui wa kijamii,kiuchumi na kiutamaduni wanaolinyemelea taifa letu.Utajiri uliokithiri kila pembe ya nchi yetu vimewafanya majirani wenye husuda kupanga mbinu nyingi za kudhoofisha mipango ya maendeleo hivyo kulifanya taifa letu kuwa ombaomba na maskini sana duniani.
Pamoja na unyonyaji unaofanywa na mabepari wa kutoka mataifa ya mbali,Tunazungukwa na marafiki wa mashaka ambao wamekuwa wakiwinda nyendo zetu waziwazi na kwa kificho kupitia mapandikizi ya mamluki katika sekta nyeti hivyo kutimiliza matakwa yao kwa urahisi..Fitina zao,Husuda zao,Faraka zao,Chuki zao,...Havifichiki vikichunguzwa na kubainishwa.
Kama nchi hatupaswi kubweteka kabisa na kujisahau,Wazalendo thabiti Idara nyeti zinazohusiana na masuala ya ulinzi na usalama wa taifa letu wapaswa kufungua jicho la 3,4,5,6,7 ili kubaini janja,mbinu na mikakati ya kudhoofisha uhai wa taifa kiuchumi {Biashara,Viwanda,Kilimo,Elimu,Mazingira ya uwekezaji,Sera na Sheria}.
Yapo madhara mengi yatakayolikumba taifa kwa mdororo endelevu ambao utalifanya taifa kuendelea kuburuta mkia katika vigezo vya kujikwamua toka ktk lindi la ufukara,maradhi,umaskini,Upumbavu,bonde la kipato kati ya walio nacho na wasio nacho....