ICC na watawala wa Afrika

mnyamiwono

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
708
71
Habari ndugu wanajamvi!

Naamini kabisa mko safi na imara kabisa katika ujenzi wa Taifa hili, hongereni saana!

Naomba sasa tujadili uzi huu kwa manufaa ya Taifa letu na Afrika kwa ujumla kama tulivyozoea kuimba Mungu ibariki Afrika ,Mungu ibariki Tanzania.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa nyingi katika vyombo vya habari na kwa watawala wenyewe wa Afrika wakidai eti mahakama ya ICC inawaonea viongozi wa Afrika na inavyosemekana kuanzia kesho jumamosi na jumapili wanakutana addis ababa ,Ethiopia.

Moja ya ajenda muhimu ni kuujadili mkataba wa ROMA na kuona ni jinsi gani ya kujitoa kama wanachama wa ICC kwa ujumla wao.

Sasa hebu tujiulize watawala hawa wanaitakia mema Afrika ya waafrika kweli?

Mbona wanahofu na mahakama hii pasipokutueleza kuwa mahakama hii ilimuonea mtu Fulani au kiongozi Fulani wa Afrika?

Kagame, amseveni, Kenyatta, Mugabe, Albashiri ndio wanaoonekana vinara wa mpango huu, sasa tujiulize kuna nini nyuma ya pazia la utawala wao?

Hivi wanataka kutowajibika popote endapo watatenda makosa ya uvunjaji wa haki za kibinadamu katika nchi zao?,na pia kwa kufanya hivo watawaliwa watakuwa wanatendewa haki kweli?

Kwani kwa mtazamo wa kawaida ICC ni mtetezi wa wanyonge na wahanga wa vita vya kiutawala barani Afrika.

USHAURI WANGU:

Watawala hawa waachane na mjadala huo kwani hauna tija kwa watawaliwa wa Afrika,zaidi wajadili namna ya kufuta mikataba ya kibepari yenye kuiba maliasili kutoka Afrika ikiwemo Tanzania ili kuwaletea wananchi wao Ustawi katika maisha yao.

KARIBUNI WANAJAMVI!.
 
Hili suala jinsi linavyoendeshwa haiingii akilini kwa mtu yoyote yule mwenye akili timamu. nashindwa kuelewa,hivi hapa kinachoogopwa ni nini. Hivi kama mtu anatuhumiwa na kosa lolote na kwa bahati nzuri anatakiwa akapewe muda wa kusikilizwa na competente court in my view solution ni kwenda na ku-clear jina lake napindi akionekana hana hatia basi anakuwa amejisafisha hata mbele ya jamii inayomzunguka. Kitendo cha kuogopa kwenda mahakamani na kutoa sababu za kiujanja ujanja kunazua maswali mengi hadi kufikia kuamini kuwa hizo allegations zina ukweli ndani yake. Suala la kujiuliza ni kwamba je,Kenyatta asingeupata urais wa Kenya,bado angekataa kwenda ICC? Hapa jibu lipo wazi kuwa asingeweza kukataa maana ingekuwa pia ni rahisi ku-issue arrest warrant na angekamatwa kama mtu wa kawaida. Ni wazi kuwa anataka kutumia kinga ya urais kukataa kwenda mbele ya haki. Ikumbukwe pia kuwa makosa anayotuhumiwa nayo yalitendeka wakati bado hajawa rais. viongozi wa kenya wanasikika wakisema kuwa vijana wao hawawezi kusikiliziwa kesi zao nje ya kenya. Swali hapa ni je,wakati wanasain mkataba wa Roma unaounda mahakama hio walijua wazi kuwa mahakama hio haipo kenya hivyo hata kama kunamtuhumiwa mkenya walijua tangu mwanzo kuwa angepelekwa ICC na hakukuwa na tatizo. Why now...? Ok,sababu zote walizoziona wakatiwanasain mkataba ule,leo zinaonekana hazina maana kwa kuwa viongozi wao ni victims...? na je,ingekuwa kati ya watuhumiwa wote hakuna viongozi wa kuu yaani ni raia wa kawaida,bado wangehitaji kujitoa? Ukiwaangalia Kenyatta,Kagame,Mugabe,Museveni na Al Bashiir wote wanafanana kwa namna fulani ki utawala wao. AU wanatakiwa kuwa makini sana wasije wakaingizwa kwenye mchezo wasioujua...
 
Ajabu yake ni kwamba, viongozi/marais tu wa kiafrica ndio hawaitaki ICC, wananchi karibia wote wanaipenda, sasa sijui hao viongozi wanamuwakilisha nani kwenye kukataa icc. ajabu kweli viongozi wa africa, ni aibu kubwa mno.
 
kitendo cha viongozi wa bara hili eti kupitisha hoja ya kuzitenga nchi zao na ICC ni cha aibu na cha kukemewa na kila aliye mwafrika. Kwa kifupi viongozi wengi wa kiafrika ni madikteta, majambazi, wagandamizaji wa haki za raia wao, wauaji na ni kama genge la wahalifu wanaojaribu kujiwekea wigo wa kuikwepa hukumu.
Wanalalama eti wanaandamwa wakati baadhi yao wenyewe ndiyo wamejisajili kule! Haiingii akilini hata chembe kwa raia mwema asiye na hatia na aliyesingiziwa jambo kugwaya kwenda mahakamani!
Genge la wahuni hawa wasio na haya wala soni wanalalamika eti wanaandamwa wenyewe tu wakati wenzao wa nchi za magharibi wana mifumo yao imara ya kuwawajibisha wanapokosa kama ilivyotokea mara kadhaa kule Japani, Ufaransa, Italia ambako karibuni tu muhuni anayefanana na manyang'au yetu haya alikiona cha moto; jambo ambalo ni ndoto kutokea katika nchi zetu hizi!
Njia ya pekee ya kuwaadabisha wahalifu hawa ni kuwakatia kabisa misaada ili serikali zao za kihuni zikose pumzi na kuangukia pua.
Narudia tena na tena kinachofanywa kule Adis Ababa ni ubakaji wa haki zetu na wahuni na wahalifu tuliowakabidhi dhamana ya kutuongoza.
 
ajabu ni kwamba, hata wakijiondoa bado wanashitakika tu ICC, arrest warrant zitatolewa tu hivyo hawatakuwa wamekwepa chochote. ni aibu sana kwa africa kujitoa icc, tutadharaulika mno.
 
ajabu ni kwamba, hata wakijiondoa bado wanashitakika tu ICC, arrest warrant zitatolewa tu hivyo hawatakuwa wamekwepa chochote. ni aibu sana kwa africa kujitoa icc, tutadharaulika mno.
Utadharaulika na nani mkuu? Tatizo hii mahakama inabagua mataifa na nchi za kufuatilia. Waende Uingereza na Marekani wakafanye hivyo hivyo hakuna hata mtu atakayewaonyeshea kidole
 
Utadharaulika na nani mkuu? Tatizo hii mahakama inabagua mataifa na nchi za kufuatilia. Waende Uingereza na Marekani wakafanye hivyo hivyo hakuna hata mtu atakayewaonyeshea kidole
marekani na uingereza wamefanya nini?fafanua zaidi ili ujibiwe kulingana na vifungu vya sheria. walifanya makosa hayo lini na wapi, na ilikuwaje. unaposema africa ndio iko targeted, mbona karibia referrals zote kule zilipelekwa na waafrica wenyewe hiyo tu ya kenya ndio prosecutor suo motu alianzisha. pia, watu wanapelekwa pale kama kutakuwa na ushahidi kwamba wao wamevunja vifungu vya kwenye icc statute kwenye makosa yale matatu genocide, crimes against humanity na war crimes. kwa hao wamarekani ungeweza kuwakamata kwenye war crimes and crimes against humanity lakini wao wajanja, wanapigana vita kisomi sana kiasi kwamba wakiwa kwenye battle ground hawavunji sheria za kivita. kama ni kwenye crimes against humanity whether you mention afghanistan, maeneo yote yale wanaua raia, wale raia wanakuwa wamefanywa shield na taliban so they are not targeting civilians deliverately. hakuna kosa lolote walilovunja kwenye icc statute. ukija kwenye iraq war, ramsfed na bush walifanya makosa yale kabla icc statute haijawa in power hivyo hawashitakiki.

ukienda israel, maeneo yote wanapiga ndiko rocket zinakokuwa zinarushwa na ndiko combatants wao wanakuwa wamejificha, its justifiable kisheria collateral damage kama hizo.
 
Ajabu yake ni kwamba, viongozi/marais tu wa kiafrica ndio hawaitaki ICC, wananchi karibia wote wanaipenda, sasa sijui hao viongozi wanamuwakilisha nani kwenye kukataa icc. ajabu kweli viongozi wa africa, ni aibu kubwa mno.

Kikwete na serikali yake wasijejiingiza kichwa kichwa kusaini makubaliano ya kujitoa kwenye Rome Statutes bila ya ridhaa ya waTanzania ambayo inaweza kupatikana kwa kura ya maoni ya wanannchi na sio kupitia bunge la magamba!!!Kuikataa mahakama ya ICC ni kuendeleza ufisadi wa watawala wa Afrika; na sisi nchini mwetu hatuna budi kupinga kujitoa huko ICC kwani huko ndiko liliko kimbilio letu la mwisho dhidi ya ufisadi.
 
Africa nyeusi haijakombolewa!!leo viongozi wetu wanalalamika kwa kuwajibishwa kwao kutokana na kuua raia wasio na hatia!
 
Nisamehe kama sijakuelewa hapo mkuu ina maana Crime against humanity ukitumia usomi wako kuua iwe kwa AK47 au Grenade unakuwa umeua kisomi au aje? Hiyo mahakama ilipaswa kuwa kioo cha ustawishaji amani duniani. Hatutaki mambo ya usomi au nini kuua binadamu ni kuua kule kule.
 
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1381588008.974583.jpg
    95 KB · Views: 717
mkuu, kuna sheria zinazoguide beligerence, zipo sheria kabisa zinazosimamia nini unaweza usifanye ukiwa kwenye uwanja wa mapambano. wamarekani na waislrael ndio wanafuata sheria hizo wakiwa uwanjani. kama wasingefuata wangeshashitakiwa kwa makosa ya kivita. sio kuua kote kutashitakika ICC, ni kuua kule tu ambako kuko na elements za makosa matatu (kwa sasa) ya icc statute. kama element za makosa hayo hazijakidhi mtu hawezi kushitakiwa pale. mojawapo ya makosa ya kivita ni kutumia raia kama cover/ngao wakati huohuo unawashambulia adui, usifikiri adui yako atanyamaza kimya kukushambulia palepale kwenye raia wakati wewe unaendelea kummaliza na ukiwa na ngao/cover ya raia. kwamfano; tz ikiwa inpigana na marekani, wanajeshi wa tz wakakaa pale manzese ddarajani wakawa wanashambulia majeshi ya marekani yaliyoko kibamba, usifikiri marekani itakubali imalizwe kwa kuogopa kupiga mazese wasijekupiga na wananchi. kuna mazingira wanaweza kushambulia hata maeneo ya raia. mfano wake ni yale yanayotokea gaza na afghanistan.

ili kosa la crime against humanity lishitakike, there need to bee "a widespread and systematic attack against civilian population", yaani mashambulizi kwa raia ambayo ni ya mpangilio/yalipangwa systematically na ni widespread (sio mauaji ya mtu mmojammoja tu, yawe halaiki). angalia kwenye allegation zako zote, unaweza kusema mashambulizi hayo yalikuwa widespread/halaiki and systematic/yalipangiliwa ili kosa la crime against humanity litimie?..utapata jibu mwenyewe.

kwa kumalizia, watu wengi wamesema ramsfed na bush walitakiwa kushitakiwa na icc kwa kushambulia iraq,wakati saddam anavamiwa, icc statute ilikuwa bado haijawa in power, na hata kama ingekuwa in power, crime of aggression ambayo ni moja ya makosa manne ya icc statute halijaanza kufanya kazi hadi mwaka 2017 kitakapokaliwa kikao kingine. kwasasaivi, nchi ikivamia nchi nyingine icc haina nguvu bado.

hata hivyo, ni discussion ndefu sana, siwezi kuelewesha sana, ni darasa refu sana.
 
Jamaa naona ametukana matusi yote, ila yuko sahihi sana, kama tungekuwa tunaheshimiana sisi kwa sisi kwanza.

 
[h=2]maraisi wa AU wnaiogopa nini ICC?[/h]
maraisi wa africa wanapodai kuwa ICC ipo kwa ajiri ya kuwafedhehesha viongozi wa africa, ni waongo na tusiwaunge mkono. Kuna wakati mahakama ya dunia iliyopo the Hague, iliwasaka sana askari wa NAZI wa ujerumaji wakajibu mashtaka ya kuwauwa wayahudi. Wengi wa askari wa nazi wamefia jela au kujiuwa wenyewe. katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa DR Kurt Waldheim naye ni mmoja wa viopngozi aliyepewa arrest warrant ili akajibu hujuma zake za kushiriki kuwauwa wayahudi na alifungiwa kusafiri popote duniani.Hitrler ana arrest warrant mpakam leo ipo katika out going mail.

Slobodan milosevic raisi wa zamani wa Yugoslavia alikamtwa na mahakama ya dunia na kufufungwa maisha mpaka kafia gerezani . magenerali wa yugoslavia wengi wapo na arrest warrant. Iweje Leo hawa maraisi wa African unity wapoteze muda kukutana pale Ethiopia kulalamika kuwa AU ijitoe katika signartori wa ICC, eti ni wabaguzi wa rangi wanawawinda tuu viongozi wa africa tuu?

hawa maraisi wa Africa ambao wamezoea kutawala mabunge yasiyo na nguvu, na mahakama zisizo na nguvu wala huru wanaona ICC kama vile ni chombo kinachowapunguzia nguvu za umwinyi. Hivyo wanataka kukitosa.

NB: watanzania tuiombe UN, USA na EU wafanye dili na viongozi wa africa unity ya kuwa: kama ICC ikitoswa tuu basi na wao nao waunge mkono kila mapinduzi ya kijeshi yanayowaliza viongozi wa africa.
 
Ni upuuzi...out of mataifa 54 yaliyo wanachama wa AU 34 walisaini mkataba ya Rome uliopelekea kufungua ICC...kwani lengo lake lilikuwa kuwashughulikia waafrika tu?
 
ICC NI WAHUNI TU WANAKAMATA WAAFRIKA TU, mbona wasikamate Bush aliua kule Iraq au Obama kaua maelfu Libya na syria
 
Maana yake nini kutuletea mabango ya mwaka jana huna mpya au hiyo cnn ya 6:36 OCT 12 ni mazingaombwe tu

Kama africa ingelikuwa haiitaji ICC, mauaji ya Rwanda, Burundi, Kongo yasingekuwa kwenye historia ya Afrika. Mauaji ya wenyewe kwa wenyewe yangekuwa ni ya kufikirika lakini yametokea kweli ndani ya bara hili. Bila mahakama za kimataifa kama ICC, waliofanya mauaji rwanda wangekuwa mtaani.
Lakini cha kujiuliza zaidi Afrika mbona haipigi hatua kimaendeleo? Angalizo: maendeleo utakayotaja ni basic kwa kuwa watu wapo na rushwa inasonga. Yako mikononi mwa watu si bara kama bara mfano miundo mbinu, shule hospitali nk. Ila kuna watu matajiri
 
ICC NI WAHUNI TU WANAKAMATA WAAFRIKA TU, mbona wasikamate Bush aliua kule Iraq au Obama kaua maelfu Libya na syria

Kwani walishikwa mkono wasaini,embu jaribu kufikiria nje ya box,bila ICC hawa watawala wa waki Africa wangeuwa watu wangapi??tuna mahakama gani tunayoiamini Afrika inayoweza kuwashtaki maraisi wetu??????
 
Kwani walishikwa mkono wasaini,embu jaribu kufikiria nje ya box,bila ICC hawa watawala wa waki Africa wangeuwa watu wangapi??tuna mahakama gani tunayoiamini Afrika inayoweza kuwashtaki maraisi wetu??????


WENGI WAO NI WATUHUMIWA WATARAJIWA



Kenya Leader Should Not Attend ICC Trial, AU Says - THE EAST AFRICA TIMES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…