Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 14,184
- 22,586
Tunaishi kwenye dunia hii moja, wote kwa pamoja, tunaishi kwa pamoja pia mzunguko wetu wa maisha ni mmoja!
Lakini kuna watu ni kinyume chake, wao wana mzunguko wao, maisha yapo kivyao, tabia kivyao!
Ibrahim ajibu, huyu mtu ana dunia ya peke yake!
Ni mmoja kati ya namba kumi bora kwa sasa kwa upande wa wazawa na wageni pia! (baadhi)
Huwa namshangaa sana ajibu anauchukulia mpira kirahisi!
Yaani anaufanya kama mzaha na masikhara kwake, na mpira unamtii bila shuruti!
Mpira unampenda ajibu ila yeye anauona rahisi mno,anaufananisha na kunywa maji! Mtu wa ajabu huyu! Mvivu wa mazoezi, lakini bado mpira unamtii!
Nijikite kwenye Mada zaidi..
Nimeskia ajibu kashaanza mazungumzo na club yake ya zamani simba!
Well sio jambo baya yeye kurudi alipotoka! Na wala sio jambo zuri yeye kurudi alipotoka zaidi ya yeye kuwa vizuri kimaslahi!
Kama ninavyosema ajibu anauchukulia mpira kimasihara sana na ndo maana mpaka sasa yupo yanga jambo baya zaidi hajali kuhusu maslahi yake yeye anauchukulia mpira kama starehe!
Halitokua kuwa jambo la ajabu yeye kuongeza mkataba yanga!
Ingekuwa vipi kama mbwana samatta angeendelea kubaki simba mpaka Leo?
Sio ajabu sasa angekuwa ndanda! Au mwadui!
Kwanini? Sababu mpira ni short career Leo unacheza baada ya miaka kumi tayari mpira unaanza kukukataa!
Wakati mwingine huwa nafikiri sababu ya wachezaji wetu wengi kutokucheza nje ni sababu ya uongozi unaowasimamia
lakini pia hakuna wakala asiyetaka kumsimamia mchezaji mzuri!
Jambo la msingi ni kwenda na wakati, muda haukusubiri!
Kwa sasa soka la ulaya limejaa wachezaji aina ya ajibu.
Wasiotumia nguvu nyingi.
Akili nyingi..
Wenye jicho mbele ya goli!
Na kizuri zaidi ajibu ni kiungo!
Anaweza kutumika nyuma ya striker na akafanya vizuri! Ukizingatia kwa sasa viungo wa aina hiyo wapo wachache!
Ni wakati sasa wa ajibu kufikiria career yake na maisha yake pia nikimaanisha maslahi!
Mpira ni pesa na pesa iko miguuni kwake!
Naunga mkono ajibu kurudi Simba (sipo kishabiki hapo)
Leo hii mchezaji kama samatta
Akifikisha miaka 30 anaweza kuanza kusomea kozi ya ukocha huko kwa wazungu huku anamalizia soka lake!
Baada ya muda pale Genk anaweza kupewa team ya vijana akaanza nayo huku anapiga pesa huku anatengeneza jina kwa kupitia taaluma nyingine ya ukocha!
Yote haya yanakuwa ukiwa ulaya tofauti na huku kwetu Africa!
"Pancho boy "