Iboreshwe kwanza TTCL kabla ya ATCL

Iboreshwe kwanza TTCL kabla ya ATCL

LAAM RASHIDI

Member
Joined
Sep 12, 2016
Posts
44
Reaction score
66
1-Najiuliza sana ni watanzania wangapi kati ya milioni 50 tuliopo tunaweza kulipa nauli ya ndege kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine au kutoka nchini kwenda nje ya nchi? Ukweli ni wachache sana!

2-Najiuliza sana ni watanzania wangapi kati ya milioni 50 tuliopo tunaweza kununua vocha ya sh.500 kila siku na kuziweka katika simu zetu? Ukweli ni wengi sana tunaweza kumudu kuweka vocha kila siku!

3-Mheshimiwa Rais wangu kulikuwa na haja kubwa sana kuanza kuifufua kwanza kampuni yetu ya kizawa ya simu (TTCL) kabla hata ya kuifufua ATCL,ni ukweli uliowazi biashara ya mitandao ya simu inakua kila uchwao leo duniani kote,kampuni za nje zimewekeza hapa nchini na zinajiendesha kwa faida siku zote,watanzania tunatamani sana kutumia mtandao wetu kuliko kuendelea kuitumia hii ya kigeni,Mheshimiwa kulikuwa na haja kubwa sana kuiboresha TTCL kabla hata ya ATCL,mapato yangepatikana maradufu kwa kuwa wananchi wengi wangeitumia huduma ya kampuni lakini pia tungetengeneza ajira kwa vijana wengi sana watakaojishughulisha na uuzaji was bidhaa za TTCL mf.vocha za simu nk.

TTCL inahitaji kuendeshwa na vijana waliopo katika biashara hii kwa muda mrefu sana,vijana wenye mtazamo wa kibiashara na vijana wazalendo waliopo nchini.

Mf.KELVIN TWISA,EPHRAIM MAFURU ni aina ya vijana tuliowaona wakifanya makubwa kule waliko.

Mheshimiwa Rais TTCL ni kampuni tukiisimamisha vyema kabisa itatuingizia mapato mengi sana kupitia kwetu wananchi kuliko hata ATCL.
 
Wazo la msingi japo ni vyema kwenda kwa pamoja japo kwa TTCL yamepaki mambo machache ya 'shrewd corporate management' kwa ushindani na makampuni makubwa ya Telecoms duniani.
 
Kwakuwa ndege zimeshanunuliwa, kwahiyo kwa mtazamo wako unataka ziuzwe zile ndege mbili kisha tuboreshe TTCL kwanza? Kuwa makini wewe kwani umejiuliza kuhusu ushindani wa soko la biashara ya mitandao ya simu nchini sambamba na ushindani wa soko la biashara ya usafiri wa ndege hapa nchini. Mambo sio rahisi hivyo.
 
TTCL inahitaji management makini ya kiushindani na makampuni makubwa duniani.
SERIKALI INGEJUA NI JNSI GANI RAIA WANAVYOISUBIRI KWA HAMU TTCL IRUDI KWENYE CHATI.....ILI RAIA WAANZE KUITUMIA KAMA MTANDAO WAO NAMBA MOJA....MAANA WATU WAMECHOKA NA UJAMBAZI WA HAYA MAKAMPUNI BINAFSI UNAVYOTUFANYIA....
 
ATCL na TTCL mimi naona ni majini tu, hata ulilishe vipi litataka zaidi na zaidi. TTCL wamepewa mkongo wa taifa wa mtandao halafu utakuta bado biashara inawashinda sababu customer care mbovu. Tulikubali tu soko huria, huu uzalendo wa kutumbukiza kodi zetu kwenye mashimo yaitwayo TTCL na ACL ufike mahali uishe.
 
Live kabisa yani
 
ATCL analipa zaidi ya milioni 100 sh kila Bombadier kwenda Hazina kila mwezi,hadi amalize deni,kwani ndege zimenunuliwa kwa pesa za serikali.Inatia moyo.
Lakini jambazi TTCL amezoea vya kunyoga vya kuchinja hakamati meta.Tulishasema huko nyuma TTCL ni Ebola,uza nyama yule au wamilikishe wananchi kwa mtindo wa hisa.
 
ATCL na TTCL mimi naona ni majini tu, hata ulilishe vipi litataka zaidi na zaidi. TTCL wamepewa mkongo wa taifa wa mtandao halafu utakuta bado biashara inawashinda sababu customer care mbovu. Tulikubali tu soko huria, huu uzalendo wa kutumbukiza kodi zetu kwenye mashimo yaitwayo TTCL na ACL ufike mahali uishe.

TTCL ilifilisiwa na wawekezaji!mkataba ulikuwa kuboresha kampuni na kuongeza(increase) wateja kutoka walipopokea ikiwa na wateja(line) 150000(laki moja na nusu) mwaka 2000 kuwa na wateja laki nane(800000) baada ya miaka minne lakini juzi serikali imepokea ikiwa na line 79000(seventy nine thousand only)!!!!!!! What a shame. Kwa hiyo msilaumu wafanyakazi wa ttcl ila wawekezaji na serikali.
 
Pole ndugu yangu, yawezekana wewe upo karibu sana na TTCL(e.g. mfanyakazi), hivyo kuna mengi unayajua ambayo wengi hawayajui. Lakini utendaji kazi wa shirika letu hili bado ni tatizo, hata kabla ya wawekezaji kuletwa. Nakumbuka mzee wangu alitamani sana kuweka landline, tena kipindi hicho walikuwa na promotion ya kuunganishwa kwa sh 54,000/-, hiyo ilikuwa 1998-1999. Urasimu alioupata ulikuwa ni mkubwa sana kiasi kwamba akakata tamaa na kukosa hiyo huduma. Huu ni mfano wa namna wafanyakazi wa TTCL walivyosaidia kulipeleka shimoni hili shirika.

Mfano mwingine ni shirika la reli. 'Madereva' wa treni za mizigo wanangusha baadhi ya mabehewa na kuiba mafuta halafu wanajisifia mtaani. Ikafika kipindi shirika halijiendeshi kwa ufanisi ikabidi serikali itafute mwekezaji. Wafanyakazi wale wale waharibifu wakawa wa kwanza kupinga na kutoka povu. Maneno mengi kuonyesha kuwa kabla ya wawezekezaji mambo yalikuwa mazuri, kumbe uongo mtupu. Tanesco nao walifanya hivyo hivyo walivyoletewa wawekezaji toka SA.Hivi ndivyo hali ilivyo kwa mashirika mengi ya umma.

Kwahiyo wafanyakazi na uongozi wa shirika mnastahili lawama kwa kulifikisha shirika hatua ya kuhitaji uwekezaji. Mfano mna huduma ya TTCL mobile, mbona hamuitangazi na ina miaka kadhaa toka ianzishwe? Mtasingizia bajeti wakati unaweza ukaweka tangazo facebook bure? Ukaelezea huduma zako mtandaoni bure? Ukaweka video Youtube bure? Watu tunaijua vizuri huduma ya Tigo ya 'Halichachi' ambayo hata mwezi haina, lakini hatuijui TTCL mobile na vocha zake zinakopatikana ijapokuwa mmekubwa sokoni kwa miaka. Shirika ambalo limezidiwa wateja na Halotel ya juzi huwezi kulichukulia serious.
 
Back
Top Bottom