IBARA YA 46A YA KATIBA YA TANZANIA.

IBARA YA 46A YA KATIBA YA TANZANIA.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
21,854
Reaction score
26,093
Bunge la Tanzania linaweza
kupitisha azimio la kumtoa Raisi
madarakani kwa mujibu Wa Ibara
ya 46A ya katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania.
Kwa kufuata utaratibu ufuatao;
1. Raisi lazima awe ametenda kati
ya yafuatayo;
A. Ametenda mambo ambayo
yanavunja. Katiba au sheria ya
maadili ya utumishi Wa umma.
B. Ametenda vitendo ambavyo
vinakiuka Maadili yanayohusu
sheria ya uandikishwaji Wa vyama
vya siasa
C. Amekua na mwenendo
unaodhalilisha kiti cha uraisi
2. 20% ya wabunge wote wasaini
kwenye azimio na iwasilishwe kwa
spika siku 30 kabla ya siku ya
bunge kuanza.
3. Spika atamruhusu mtoa hoja
kuwasilisha hoja, mbunge mtoa
hoja atasilisha hoja yake.
4. Baada ya mbunge kuwasilisha
hoja, bila kuijadiri hoja hiyo bunge
litapiga. Kura kuunga mkono hoja
au kupinga.
5. Wabunge wasiopungua 2/3
wakipiga kura ya kuunga mkono
hoja, basi Raisi atasimamishwa na
kuondolewa Ikulu huku ikiundwa
kamati maalumu ya uchunguzi,
kuchunguza tuhuma
anazotuhumiwa nazo Raisi.
6. Kamati ya uchunguzi hiyo
itakua na watu wafuatao;
A. Jaji mkuu (kwa sasa ni kaimu
jaji mkuu)
B. Jaji mkuu Wa Zanzibar
C. Wajumbe 7(wabunge)
wanaoteuliwa na spika.
7.kamati Ya uchunguzi, ndani ya
muda usiozidi siku 90, watatakiwa
kurudisha ripoti kwa spika. Ripoti
itakua inahusu uchunguzi
uliofanywa kuhusiana na tuhuma
anazotuhumiwa Nadia, na kamati
lazima imhoji Raisi.
8. Ripoti Ya uchunguzi
ikiwasilishwa bungeni, na baada
ya kuwasilishwa bungeni, bunge
litaijadiri na baada ya kujadiri
bunge litapiga kura.
9. Baada ya kupiga kura, wabunge
wasiopungua 2/3 wakipiga kura
ya kuwa tuhuma dhidi ya Raisi
zimethibitishwa, basi Raisi
ataondoka rasmi madarakani.
10. Baada ya maazimio ya bunge,
bunge litamtaarifu mwenyekiti wa
tume ya uchaguzi ili mwenyekiti
Wa tume aitishe uchaguzi Wa
Raisi.
 
Sasa wabunge kaz kwenu. Kwani zimebaki siku ngapi hadi bunge lianze?
 
Back
Top Bottom